View attachment 2668869
Ikifika mwezi wa 7 , kuna ‘mbuzi’ wawili au watatu watatolewa kafara, hii ni kwa decoding binafsi ya mtiririko wa matukio takriban matano hadi kumi niliyoya -observe, na inanipelekea kuamini hivyo.
1.) Haya majibu yanayotolewa na serikali kupitia Gerson Msigwa , Kassim Majaliwa na Hamza Johari yanatolewa kwa ajili ya nani? Maana tumeambiwa hizi kelele hazibadilishi chochote, sasa ya nini kutujibu wapiga kelele?
2.) Ni lini iliwahi tokea hapa Tanganyika pakawa na such an intense persistence, consistence na insistance ya kupinga matendo ya serikali kwa muda wa mwezi mzima bila kupumua, we are breathing bandari, day in , day out , hadi lini tutakuwa ignored?!
3.)Rais akiongea kwa sasa sauti yake inatetemeka, anaogopa nini, anaongea as if anataka kulia kwanini? Tangu lini mkuu wa nchi akatoa kauli irresponsible na ya kimipasho kama ile dhidi ya hoja serious kama za kuuzwa kwa Tanganyika, kwamba anaweka pamba masikioni?! Siasa ni Taarab?!
4.)Hadi majumbani watoto wanatuuliza tuufafanue mkataba huu wa bandari, imagine, kwa aibu kali inabidi tuwaeleze kwamba tumeuzwa kwa waarabu na waZanzibari, na huo ndio ukweli, wala sio udini au ubaguzi, ni ukweli tu., narudia kuziweka hoja hapo chini.
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?