Tulitumia Bunge kutaka kufuta vyama vya siasa matokeo yake vyama vimeimarika Bunge limekufa

Tulitumia Bunge kutaka kufuta vyama vya siasa matokeo yake vyama vimeimarika Bunge limekufa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kazi Bunge nikuisimamia Serikali iliyopo madarakani itende Kwa maslahi ya Taifa. Kazi hii imegeuka siyo main objective tena bali lengo kuu la bunge lililopo chini ya uongozi wa sasa na ujao nikushirikiana na Serikali. Kushirikiria maana rahisi nikutengeneza pertnership na kwenye partnership always lazima mkubali kuachana na baadhi ya nguvu na mfanye kazi pamoja( you surrender some of your powers..) . Ni Kwa bahati mbaya sana kwamba kwa miaka sita bunge limeamua kwa kauli moja kuacha kazi yake ya msingi kabisa yakuikosoa Serikali na kuamua kushirikiana na Serikali bila serikali kutangaza rasmi kwamba ni nguvu gani imeamua kuiacha (ku-surender) kwa Bunge.

Nasema Bunge limeacha njia kwa sababu watia nia wote wa CCM kwa kiti cha spika wameahidi kushirikiana na Serikali means ndoa hii ni Moja na kwamba mwenyekiti wa chama kupitia katiba ya chama na kura yake yakupitisha mgombea spika ni wazi kwamba ataabudiwa kwa nafasi yake kwenye chama pamoja na kuahidiwa ushirikiano kwenye Bunge.

Hiki ni kifo cha wazi Cha bunge. Wakati Bunge limekufa ,vyama vya siasa vimekua Kwa kiasi kikubwa na kuiarika na kuchukua kwa aslimia kubwa jukumu la bunge la kuikosoa serikali. Ni mwaka Sasa hakuna ukosoaji uliofanyika Bungeni na hata uliofanyika Kwa bahati mbaya ukafanywa na spika uipelekea kumweka pembeni ingie mtu anayeweza kushirikiana na serikali siyo kuikosoa.

Baada ya Bunge kufa matarajio ya Wananchi kupata sheria mbovu ni makunwa Zaidi na uwezekano wa kuondoa utengamano wa kitaifa mkubwa.

Swali lakujiuliza,Bunge litazaliwa lini? Maana kufa Kwa Bunge siyo mwosho wa Bunge Bali ni mwanzo wakuzaliwa Bunge jipya, but when
 
Mungu ni mwema na anachukia uovu, Wana ccm maneno kama hayo yapo midomoni kwao ila sio kwa vitendo🏃.
 
binafsi naamini 2025 ndo mwisho wa mauza uza ya ccm, mungu ibariki CDM, mungu ibariki Tanzania.
 
Tuanze na hoja hii. Ahadi ya kwanza ya mgombea Ubunge kwa wananchi ni kushirikiana nao kuwaletea maendeleo ktk nyanja zote. Nao wanamchagua wakiamini atawawakilisha ktk kuleta maendeleo hayo ktk jimbo lao. Ili yapatikane uwakilishi wake ni kuwasilisha shida na kushawishi serikali kubadili maisha ya watu ktk jimbo lake. Kama ni demokrasia, uzalishaji mali n.k. yote lengo ni maendeleo ya nchi na watu. Unawezaje kufanya hayo bila kushirikiana na serikali yenye mfuko ktk kufanikisha hayo? Ukiikosoa serikali tayari umeshirikiana nayo. Ukiipongeza kwa lolote jema ililofanya, umeshirikiana nayo. Ukipinga lisilo jema kwa watu wako umeshirikiana nayo na ndiyo kuisimamia serikali.
 
Back
Top Bottom