MUME WANGU ANANIZALISHA MFULULIZO KILA MWAKA, NIMECHOKAAA
Duniani Vioja haviishi sasa hata hili kweli , jamani naomba ushauli nifanyaje maana nashindwa kuamua chochote
kaka mwaka 2006 niliolewa na msomali mmoja hivi hapa Mombasa Kenya.... yuko na pesa za kutosha hatuna shida sawa lakini tangu anioe amekuwa ni mtu wa kunizalisha kila mwaka, niliolewa 2006 lakini mpaka sasa nina watoto 8, na nina miaka 38.
Imefika wakati watoto hata hawajulikani yupi mkubwa yupi mdogo
sasa hivi nimemkimbia nalala kwenye chumba cha watoto, alivyoona hivyo ameacha kulala nyumbani, mala anachelewa kurudi...
Mimi nimeshachoka jamani imefika mda sina nguvu kutokana na kuzaa mfululizo, eti jamani nifanyaje? Nakosa uamuzi maana nikienda kulala chumbani hataki tutumie kinga, matokeo yake mtoto hata hajakuwa vizuri mimba nyingine inaingia, nawapenda watoto ila hii imekuwa too much naomba unisaidie nifanyaje
Wanawake wanataka nini Jamani wazae shida wasizalishwe shida ..............