Tuliwaonya vijana wanunue magari yanayotumia mafuta kidogo hawakutusikia

Tuliwaonya vijana wanunue magari yanayotumia mafuta kidogo hawakutusikia

Mkuu kama ulikua hauna taarifa ulaya au nchi zilizoendelea hakuna hela za pembeni kama unalipwa $800 dawa ni kupunguza tu matumizi tofauti na kwetu unaweza kua unalipwa 900,000 lakini siku ukaotea dili ukapiga 5m au hata 10m aisee hapo sasa ndo unaenda unakunja crown athlete 2GR...na kama kawaida unavimba...😂😂😂
Hela ya pembeni huku kwenu ndio mnaita deal ni wizi. Ulaya hela ya pembeni ipo kwenye extra job or extra hours na iinalipa sana.
 
Hela ya pembeni huku kwenu ndio mnaita deal ni wizi. Ulaya hela ya pembeni ipo kwenye extra job or extra hours na iinalipa sana.
Hahaha mkuu sio moja kwa moja kuna sehemu niliwahi kuwepo extra hours ilikua 900,000 pure legit nje ya mshahara..pia hela ya pembeni inaweza ikawa commission au hata msaada kwa mtu i.e kihalali mtu anatakiwa alipie 40m yeye mwenyewe anakwambia anakupa 20m ingine potezea unafanyaje...?umlazimishe alipe yote nkt kasema hana...?
 
Acheni mawazo ya kimasikin WaTz... Ni heri ununue gari ya Mamillion ya pesa kwa wiki ukaitumia ×4 hizo siku 3 ukapanda daladala... Kuliko ununue IST VITZ PASSO PORTE SPACIO na hizo vidude vingine [emoji28] ni aibu ni ushamba na kujishusha thamani ya kujiamini mjini [emoji23] sometimes mnakosa fursa kwasabab ya mitazamo hasi au negativity, sometimes mnakosa connection kwasabab hamjiamini mnatokea kinyonge mbele za watu, Ladies and Gentlemen FIRST IMPRESSION MATTER popote pale duniani... Vijana msiogope kununua magari ya CC kubwa au Mamillion ya pesa kwani ukiliendesha weekend pekeake ni dhambi au litaoza..?
Mimi mwaka fulani nikiwa na maisha ya kawaida sana nikiwa early 20's nikanunua gari fulani yaan gari likionekana sehem kilamtu anasema Yes hilo ndio gari sasa na huyo ni mwanaume, ilikua full tinted nikishuka kilamtu alikua haamini kama ni langu mwanzo watu walihis nimeazima au nauzia sura tu, siku zikazid kwenda miez mwanaume nipo nalo wakaanza majungu litamshinda tu huyu dogo mafuta na service... You know what..? Nilipata ma deal mengi ya pesa kwasabab ya status ya gari langu tu, watu wanakushirikisha ktk ma deal ya pesa ndefu wanakupa connection kwasabab ya unavyo ji brand... From there nikaanza hadi kujenga na kufungua miradi ya hapa na pale...
Kwahio ktk maisha ukitaka kuanza kujenga nyumba jenga nyumba kilamtu akiiona anasema waoooh... Ukitaka kununua gari nunua gari mtu akiliona anakupisha road, traffic akiliona anakupungia mkono wa safar njema... Maisha yenyew mafupi halafu mnaanza kuogopeshana kuishi
Well said
 
Mara nyingi wanaoponda IST huwa hawajawahi miliki hata starlet namba A..wivu tu au hawana kabisa lkn wanalalamikia mafuta
Kuna mambo lazima uwe na misimamo nayo, mfano kununua vitz mwanaume...hapana tembea kwa miguu ukiendelea kujikusanya ununue gari ya kiume...au hata usinunue kabisa[emoji23][emoji23]
 
Yaani vijana wa siku hizi wabishi na wapenda sifa za kijinga. Utamkuta kijana anakunja laki 8 kwa mwezi baada ya kodi, makato na tozo Yani kitaa hatuna amani fujooooo.

Tukawaonya na kuwashauri acheni kununua magari yanayotumia mafuta mengi baneni matumizi kwa kununua IST, Passo, vitz na zingine. Tukaambulia matusi na kejeli kutoka kwa hawa vijana uchwara hasa waliopanga Sinza. Ooh nyie vijana wa zamani wa seventeee na eiteez mnawivu wanga na wachawi. Ohh mnatuonea wivu. Tukala kimya.

Sasa hivi wamepaki ma crown yao wanang'ang'ania na sisi kupanda daladala na mwendo Kasi. Na Kila wakijaribu kuuza macrown yao wanakosa soko.
waliopanga sinza [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom