Tume mgogoro Ngorongoro: Serikali isitishe ujenzi wa Nyumba kwa ajili ya Wananchi wanaohamia Msomela, Kitwai (B) na Saunyi badala yake wapewe pesa

Tume mgogoro Ngorongoro: Serikali isitishe ujenzi wa Nyumba kwa ajili ya Wananchi wanaohamia Msomela, Kitwai (B) na Saunyi badala yake wapewe pesa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mapendekezo ya Tume ya Rais iliyofanya tathimini kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari, Ngorongoro Eng. Musa Iyombe amesema uamuzi wa Serikali kujenga nyumba kwa wakati huo ulikuwa sahihi hata hivyo imebainika kuwa utekelezaji wake ulikuwa na dosari zinazohitaji kufanyiwa kazi.

Tume inapendekeza kuwa Serikali isitishe uamuzi wa kujenga Nyumba kwa ajili ya Wananchi wanaohamia katika eneo la Msomela, Kitwai (B) na Saunyi badala yake itoe kiasi cha fedha ambacho kitakuwa kimejadiliwa na kukubalika ili Wananchi waweze kuondoka kwa hiari na kwenda kujenga nyumba kuendana na mila na desturi zao.

Fuatilia hapa > Rais Samia akipokea taarifa ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari, Ngorongoro
 
Hao wamasai hawataki kujenga nyumba ili waendelee kutembeza mifugo waki saka chakula na maji kuharibu mazingira huko Tanga na kugombana na wakulima.

Kujenga nyumba kuindena na Mila na desturi, ndio nyumba Gani hizo ? Nyumba za matope.

Taifa halitaendelea kwa kuendekeza watu wa hovyo
 
Back
Top Bottom