BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akizungumza leo Jumanne Januari 31, 2023 Ikulu Chamwino, Dodoma wakati akizindua tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini, Rais Samia ameitaka tume hiyo kuichunguza ofisi hiyo juu ya utendaji kazi na uendeshaji ili kubaini kasoro zilizopo na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuiboresha iweze kutoa haki kwa wananchi.
Amesema mbali na ofisi hiyo ya mashtaka tume hiyo itakayoanza kazi Jumatano Februari 1, hadi Mei 30, 2023 itazifanyia tathmini taasisi za utoaji haki jinai nchini ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kuibua manung’uniko kwa wananchi, ikiwamo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Jeshi la Polisi, Magereza na Mahakama.
“Kutokana na ukubwa wa kazi tunawapa miezi minne kuanzia kesho hadi Mei 30 nendeni mkaangalie Ofisi ya Mashtaka kwenyewe kukoje na kuna kasoro zipi.
“Zamani ofisi hii kulikuwa na ngoma nzito inachezwa mpaka kukusanya fedha za plea bargaining nyingine zimeonekana na nyingine hazijaonekana ukifuatilia utaambiwa mara kuna akaunti China.
“Tutazame kuna nini haswa kilichoharibu hii taasisi, pia tuiangalie Takukuru kwa sababu kubadilisha tu mkuu wa taasisi haisaidii watamdanganya tu wafanye wanavyotaka.
“Jeshi la Magereza na kwenyewe tukalitazame, magereza zetu zikoje na zinatakiwa ziweje, mwendelezo wake na kama linafanya kazi ya msingi? Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya nako kuna changamoto nyingi za kutegea watu dawa,” amesema Rais Samia.
Naye, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amempongeza Rais kwa kuanzisha tume hiyo ili Watanzania waweze kupata haki kwani kumekuwa na manung’uniko mengi ya wananchi juu ya mfumo wa utoaji haki jinai nchini.
MWANANCHI