Tume ya Haki Jinai kuanza kuzichunguza TAKUKURU, DCEA, Polisi, Magereza na Mahakama kesho

Tume ya Haki Jinai kuanza kuzichunguza TAKUKURU, DCEA, Polisi, Magereza na Mahakama kesho

tunaishauri hii Tume ianze kuvichunguza kwanza hivi vyombo vya haki jinai, kwani wakati mwengine ndani ya vyombo hivi vinafanyiania uonevu mkubwa sana wao kwao wao ndani na matokeo yake huathiri utendaji kwa ujumla.
 
tunaishauri hii Tume ianze kuvichunguza kwanza hivi vyombo vya haki jinai, kwani wakati mwengine ndani ya vyombo hivi vinafanyiania uonevu mkubwa sana wao kwao wao ndani na matokeo yake huathiri utendaji kwa ujumla.
Sahihi
 
Akizungumza leo Jumanne Januari 31, 2023 Ikulu Chamwino, Dodoma wakati akizindua tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini, Rais Samia ameitaka tume hiyo kuichunguza ofisi hiyo juu ya utendaji kazi na uendeshaji ili kubaini kasoro zilizopo na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuiboresha iweze kutoa haki kwa wananchi.

Amesema mbali na ofisi hiyo ya mashtaka tume hiyo itakayoanza kazi Jumatano Februari 1, hadi Mei 30, 2023 itazifanyia tathmini taasisi za utoaji haki jinai nchini ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kuibua manung’uniko kwa wananchi, ikiwamo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Jeshi la Polisi, Magereza na Mahakama.

“Kutokana na ukubwa wa kazi tunawapa miezi minne kuanzia kesho hadi Mei 30 nendeni mkaangalie Ofisi ya Mashtaka kwenyewe kukoje na kuna kasoro zipi.

“Zamani ofisi hii kulikuwa na ngoma nzito inachezwa mpaka kukusanya fedha za plea bargaining nyingine zimeonekana na nyingine hazijaonekana ukifuatilia utaambiwa mara kuna akaunti China.

“Tutazame kuna nini haswa kilichoharibu hii taasisi, pia tuiangalie Takukuru kwa sababu kubadilisha tu mkuu wa taasisi haisaidii watamdanganya tu wafanye wanavyotaka.

“Jeshi la Magereza na kwenyewe tukalitazame, magereza zetu zikoje na zinatakiwa ziweje, mwendelezo wake na kama linafanya kazi ya msingi? Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya nako kuna changamoto nyingi za kutegea watu dawa,” amesema Rais Samia.

Naye, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amempongeza Rais kwa kuanzisha tume hiyo ili Watanzania waweze kupata haki kwani kumekuwa na manung’uniko mengi ya wananchi juu ya mfumo wa utoaji haki jinai nchini.

MWANANCHI
Takukuru Tanzania inabidi ifutwe wafukuzwe wote na waanze upya kwani ndio wanaoendeleza rushwa nchi nzima wanitafute niwape mifano hai haswa temeke ile ofisi imejaa wala rushwa na sio wanaopambana na rushwa
 
Swali langu Ni moja tu.
Hiyo tume imeundwa na wazungu toka Denmark au Ni Hawa Hawa kina Mbonde ?
Naomba waanze na yule MTU wa takukuru aliyechukua rushwa ya dola 2500 sawa na madafu miloni sita halafu akapigwa faini ya milioni moja.
Hata kuku akiliangalia hili ataelewa tu kwamba Kuna ujinga ulifanyika.
Hakuna ujinga ni rushwa ilifanyika
 
Wengine hawakuwahi kukemea, tumpongeze
Kina nani wengine? JPM si aliweka watu ndani bila kuangalia sura? Hebu niambie wapi maneno matupu yamerekebisha kitu?
Mazee mkono mtupu haulambwi! Actions, ili tusonge mbele. Taifa letu lazima liwe na uwezo wa kujitibu, ili siku moja tuwe Taifa lililoendelea
 
Kuna Tume ngapia zilizoshawahi kutungwa na hakuna kitu. Siku moja atakuja Rais , ataunda Tume kuchunguza Tume zilizowahi kupita. Ndio siasa ilivyo.
Ukiona tume imeundwa ujuewanataka kuhalalisha maovu ili waseme hatatume imechunguza nahawajaona tatizo kila siku tatizo ni mabeberu je kwanini kama mabeberu ni waovu hamachani nao makaenda kwa warusi au wachina??
 
Back
Top Bottom