Pre GE2025 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yamkuta na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka Paul Makonda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa kuwaweka ndani watu bila kuwapeleka mahakamani masaa 96? Angewekwa dada yako au mama yako ndani ungesema hivyo?
Kwani makonda ana kituo cha polisi kipi hicho cha magomeni au kibirizi😂😂
 
Na kukaidi kuitikia wito wa Time, kuna toa taswira gani kwa wake anaowangoza.
Makonda Kenya nchi zinazo heshimu haki za binadamu, hawezi kuwa hata mwenyekiti wa kitongoji
Hivi kupeleka Mahakamani anahusika Makonda au? Yeye aliweka ndani taratibu zingine zinabaki juu ya polisi!
Vilaza hao bila shaka wanatumika lakini watafail big time!

Nasimama na MAKONDA
Kwa vile ndugu zako au wewe hujawai kuwa muhanga wa kadhia za kunyimwa haki ya kuishi.
Subiri yakukute utajuta kuzaliwa.
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imemkuta na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka, Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Paul Makonda aliyeagiza mwananchi mmoja kukamatwa na kuwenda rumande saa 96 bila kufunguliwa mashtaka...
Way forward ya hiyo tume ni nini

Maana binafsi nilitegemea tume wangetoa na mwelekeo kwamba baada ya kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka huyo aliye shitakiwa nini kinafata
 
Hivi hizo tume za Nini?naona kama tunapoteza fedha za umma Bure
 
Hivi hizo tume za Nini?naona kama tunapoteza fedha za umma Bure
 
Hayo mambo mbona tunayaona kwa viongozi karibu wote ktk serikali ya Samia kwann iwe Makonda tu? Nahisi Kuna watu wanamuwinda Makonda kwa udi na ubani.
 
Hii rume haianaga meno bali ina recommendations tu ..ni moja ya taasisi zinazo kula pesa zetu tu bure
 
Wawe wanapima mabaya na mazuri then wanafanya uamuzi, yawezekana issue ilikuwa framed kumchafua Makonda lakini kwanini akatae wito...?
Kuna umuhimu wa Viongozi vijana kuwa na unyenyekevu,lakini pia wenye kufanya tathmini wasijudge kabla ya kusikiliza upande wa pili hata kama upande huo umekataa kutoa ushirikiano,mbinu zipo nyingi kabla ya kutoa report.
 
Ndugu zake wasukuma wakikusikia watakuja mbio mbio kama kumtetea ndugu yao.
Hakuna habari ya usukuma au ukabila hapa. Andika habari ya Makonda kama mtanzania.
Watanzania tulivuka mipaka ya ukabila miongo mingi iliyopita, tusirudi nyuma. Ukienda usukumani wanakuona kama ndugu yao (walioishi mikoa mingi ya Tanzania wanalijua hili).
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imemkuta na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka, Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Paul Makonda aliyeagiza mwananchi mmoja kukamatwa na kuwenda rumande saa 96 bila kufunguliwa mashtaka...
Hii tume ingebadili jina tu maana haisadifu.

Kujiita Tume ya Haki za binadamu na utawala bora sio sahihi.
 
Siasa haiamini kama binadamu hatujakamilika...
 
Nauliza tu ndugu zangu kwa mfano Makonda katoa Amri fulani akamatwe je wakamataji hawaangalii sheria inasemaje?!

Niliwahi kuuliza swali hili mahali fulani wakati DC wa Kinondoni by then Salum Happi alipoagiza Polisi wamuweke rumande mbunge wa Kawe mh Halima Mdee kwa saa 48

Mlale Unono 😀
 
Tume ndiyo inafanya uchunguzi, inasikiliza kesi na ndiyo inayotoa hukumu? Mbona hapa ni kama hapajakaa sawa au wanasheria mnasemaje? Yaani mtu huyo huyo afanye uchunguzi, aendeshe mashitaka na awe hakimu wa kutoa hukumu? Mbona hii tume ni kama imekaa kisiasa zaidi badala ya ki profession.
 
Kwanza nimpongeze tume kwa kutekekeleza majukumu yake bila woga, ila niipe pole kwa kukanganyikiwa na kesi za viongozi.

Kwa uelewa wangu mdogo ninaoweza kusema kwa upande mmoja wa Sheria makonda hayupo sawa maana ameikandamiza hakika ya mshtakiwa, lakini kwa upande mwingine ni sahihi kwa alichokifanya.

Kuna muda inabidi kuchukua maamuzi makali kwa wakosaji ili kuwakumbusha wajibu wa haki kwa wote, mathalani na hapo maamuzi ya makonda yalilenga kutetea haki na sio kuipoteza.

Tukumbuke na yeye ni mwanadamu mwenye moyo wa damu na nyama
 
Chadema mmepata ajenda 🐼
Simpaka iwe😮🐼🔥

CHADEMA toka imeshikiliwa na Dikteta Mbowe, ajenda yao ni moja tu-kutengeneza mazingira ya kudhoofisha Jeshi la Polisi-na hivyo kuonekana hakuna usalama wa raia. Yaani kwa kifupi,wanataka kuidhoofisha serikali na hatimaye nchi.

Hatahivyo
==========
Kuh: Makonda
Swali la msingi: Amevunja sheria gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…