Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wanabodi,
Baada ya pilikapilika za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeendelea na zoezi imeendelea na mchakato wake wa kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk tarehe 29 Novemba, 2024 alifungua mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani humo.
Uboreshaji huo utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume, Bw. Selemani Mtibora amesema kwa mkoa wa Kilimanjaro Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 180,540 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 ya wapiga kura 1,009,726 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Soma pia: Kuelekea 2025 Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutekeleza uboreshaji wa daftari la wapiga kura kisiwani Zanzibar kuanza Oktoba 7 hadi 13, 2024
“Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Kilimanjaro utakuwa na wapiga kura 1,190,266,” amesema.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una vituo 1,316 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 30 katika vituo 1,286 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
============================================================