Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC): Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 28, 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC): Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 28, 2020

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambayo ni Oktoba 28, 2020.

Aidha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa ratiba ya wateuzi wa Wagombea kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani utakuwa ni Agosti 25, na kampeni zitaanza rasmi Agosti 26 hadi Oktoba 27.

===
1595322437057.png

Screen Shot 2020-07-21 at 16.26.47.png

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza mabadiliko ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kuwa ni Jumatano Oktoba 28, mwaka huu.

Uteuzi wa wagombea kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani ni August 25 na Kampeni zitaanza Agosti 26, 2020 mpaka Oktoba 27, 2020.

Awali uchaguzi huo, ulipaswa kufanyika Oktoba 25. Mabadiliko haya yanafanywa kwa mujibu wa Mamlaka ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa chini ya Ibara ya 41 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Taarifa hii leo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambayo ni Oktoba 28, 2020.

Aidha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa ratiba ya wateuzi wa Wagombea kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani utakuwa ni Agosti 25, na kampeni zitaanza rasmi Agosti 26 hadi Oktoba 27.
 
Ok. Kampeni inaanza Jumatano na uchaguzi Jumatano
 
Sawa zimebaki siku 99 kuanzia leo. Tutaendelea ku countdown mpaka ifike siku ya tukio. #Super Wednesday
 
Safari hii wameuweka katikati ya week .... Nafirkiri turn out itakuwa kubwa sana. Watwambie tu kama watahesabu kura zetu kama walivyofanya CCM....!!

Kumekuwa na malalamiko muda mrefu kwamba Jumapili ni siku ya ibada kwa wapiga kura baadhi, hivyo kuathiri kimoja kati ya hivyo (kura au ibada).

It is addressed now.
 
Back
Top Bottom