Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC): Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 28, 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC): Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 28, 2020

Tume, igeni mfano kwa CCM. TBC ya Ayubu Rioba, tunaomba matangazo LIVE ya uhesabuji kura majimboni. Hapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
 
Tume, igeni mfano kwa CCM. TBC ya Ayubu Rioba, tunaomba matangazo LIVE ya uhesabuji kura majimboni. Hapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
Huu ushauri wako hauna akili .MAJIMBO YA UCHAGUZI YAKO 393 unawekaje live yote kura zikihesabiwa?

Hutumii hata akili ndogo tu?
 
Nilifikiri "TUME HURU" kumbe ni hii ya "walamba nyayo" ? yaani Jaji nanii? my foot!
 
Huu ushauri wako hauna akili .MAJIMBO YA UCHAGUZI YAKO 393 unawekaje live yote kura zikihesabiwa?

Hutumii hata akili ndogo tu?
Kura hazihesabiwi kwa wakati mmoja, hata hivyo hujui fani ya utangazazi, kuna wawakilishi kila wilaya wanaoweza kuripoti kwa wakati wao muafaka, na sio kila tukio lazima liripotiwe kuna matukio muhimu yanayohitaji kuripotiwa.
 
Habari za mida hii wanajamvi.

Kama kuna kitu kimekuwa kikinikera kipindi cha uchaguzi mkuu, ni kupanga tarehe inayoangukia siku za ibada hasa Jumapili.

Uchaguzi ni Jambo kubwa la kitaifa, sikuwa naona sababu kwanini tusifanye siku za kazi na siku hiyo kuwa siku ya mapumziko. Binafsi nimekuwa nikipata wakati mgumu kuchagua kwenda ibadani au kwenda kupiga kura na mara nyingi nimekuwa nakosa upigaji kura.

Hongera sana mwenyekiti wa Tume na makamishna wako Kwa uamuzi huo. Hii ni dalili nzuri na mwanzo mzuri wa zoezi Hilo la uchaguzi
 
Sawa. Tutashiriki

Sisi wengine tumeshakata shauri la kutoshiriki kupiga kura chini ya tume hii isiyo huru ya uchaguzi. Wangalau Tundu Lissu akiwa mgombea wa upinzani tutajitokeza kwa shingo upande, lakini tukiwa hatuna imani yoyote ya tume hiyo.
 
Waungwana Uchaguzi Mkuu wa Nchi yetu miaka yote hufanyika Jumapili ili kuwapa nafasi Watanzania wengi kushiriki kwa sababu siyo siku ya kufanya kazi. Mwaka huu uchaguzi utafanyika Jumatano. Je, siku hiyo itakuwa ni public holiday ili kuhakikisha wengi wanashiriki kwenye uchaguzi huo au itakuwa siku ya kazi kama kawaida hivyo kuwaathiri baadhi ya Wafanyakazi kushindwa kushiriki katika kupiga kura kwa kuwa watakuwa kwenye ajira zao?

🙏🏽
 
Back
Top Bottom