Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Tume inatuminisha kuwa Tanzania nzima hakuna mgombea wa CCM anayekosea kujaza fomu ila wagombea wa upinzani tu.

Huwa kuna wakati natamani Malaika washuke waje wasimamie uchaguzi nchi hii.
 
Wanatuona sisi Watanzania ni wajinga, wanalazimisha kupendwa na kukubalika kwa CCM ambao wanawatisha viongozi wa Tume kuwa wao ndio waajiri wa wajumbe wa Tume.

Hii sheria/utaratibu wa kupita bila kupingwa ni mbaya mno,ni kama vile kubaka demokrasia.Hapo mwnzo hata kama mgombea ni moja alikuwa akipigiwa kura ya Ndio ama Hapana.

Huu utaratibu wa CCM Mpya kupita bila kupingwa na kusimamiwa na sheria mbovu haukubaliki hata kidogo.Mbaya zaidi upungufu huu unafanyika kimkakati kuwapunguza wagombea wa upinzani.
 
Kwa hiyo mnafanya makusudi ili watu wawasusie? Mwaka huu mpaka kieleweke! Kura zikijaa mkataka kuziiba tunaingiza raia barabarani pumbavu nyie!
Hata 2015 mlibweka 🗣️ hivihivi, tushawazoea😂😂, hizo guts za kuingia road kukabiliana na special forces huna🚶🚶
 
Leo asubuhi Magufuli wakati yuko Misungwi amesikika akisema hapa kuanzia Mbunge hadi Madiwani wamepita bila kupingwa. Na akaenda mbali zaidi na kudai najua kuna mapingamizi yako Tume ila kwa dharau akasema najua wa hapa washapita labda kwingine huko ndio watarudishwa...
Maana yake Utulie dawa iingie
 
Mahesabu yao yamekaa kimashaka-mashaka.

Hichi alichofanya mgombea wa ccm kina tofauti gani na lile kosa walilofanya Clouds hadi kufungiwa kurusha matangazo?
 
Wapuuzi sana ninyi, mnajifanya ni Tume huru wakati kila mtu anaona namna mnavyotekeleza majukumu yenu kwa kumfurahisha Magufuli. Nchi hii ikiingia kwenye machafuko lawama na laana zote zitakua juu yenu MILELE.
Ulikuwepo kwenye maamuzi ya rufaa au umeandika tu kwa hisia
 
1 September 2020
Wagombea 557 ubunge, udiwani wakata rufaa

thumb_1939_800x420_0_0_auto.jpg


Imewekwa Tarehe: September 1st, 2020


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepokea rufaa 557 kutoka kwa wagombea ubunge na udiwani kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu wa 2020.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Rufaa Mst. Semistocles Kaijage wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Amesema rufaa hizo zinatokana na baadhi ya wagombea ubunge na udiwani kutoridhika na maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi na kwamba baada ya kupokea rufaa hizo itaanza kuzifanyika kazi leo na itajitahidi kuzitolea uamuzi mapema kwa kadri itakavyowezekana.

Jaji Kaijage amesema baada ya kukamilika kwa uteuzi wa wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa sasa Tume ipo katika hatua ya kupokea rufaa kutoka majimboni kwa ajili ya wagombea ubunge na kutoka katika kata mbalimbali kwa ajili ya wagombea udiwani.

“Hadi hivi sasa Tume imepokea jumla ya Rufaa zipatazo 557 ambazo itaanza kuzifanyika kazi leo na itajitahidi kuzitolea uamuzi mapema kwa kadri itakavyowezekana.” amesema Jaji Kaijage.

Amefafanua kuwa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 imeweka masharti ya wajibu wa kila mtu kufuata na kutii Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano na imeainisha haki ya kila mtu, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria, kuchukua hatua za kisheria kwa madhumuni ya kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi.

Jaji Kaijage amefafanua kuwa malalamiko ya ukiukwaji wa masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na Kanuni zilizotungwa chini ya Sheria hizo, yanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu na kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza wagombea wa Vyama vya Siasa mbalimbali ambao wamedai haki zao kwa kufuata taratibu za kisheria na za kikanuni katika kuweka pingamizi mbalimbali na hatimaye kukata rufaa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Tume itazishughulikia rufaa hizo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.”, amesema na kuongeza kuwa:

Kwa ujumla Sheria za uchaguzi na kanuni zake zimeweka masharti, taratibu na hatua za kuchukua panapokuwa na malalamiko ama ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi. Aidha, Sheria hizo zimeainisha mamlaka za kushughulikia malalamiko husika. Taratibu hizo zimebainishwa katika hatua mbalimbali za uchaguzi kuanzia uteuzi wa wagombea hadi kutangaza matokeo. Hivyo ni wajibu wa wagombea na Vyama vyao vya Siasa kujua haki zao, mamlaka husika na hatua za kuchukua pale ambapo hawajaridhika na jambo, katika kipindi chote cha uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.”

Jaji Kaijage amevipongeza Vyama vya Siasa na wagombea ambao tayari wameanza kampeni za uchaguzi na wanaendelea nazo, katika maeneo mbalimbali na kwamba Tume inaendelea kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wagombea kufanya kampeni za kistaarabu na zinazozingatia maadili ya uchaguzi ambayo wahusika wake wakuu ni Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na wagombea.

Mwenyekiti huyo wa NEC amesisitiza kuwa Tume ilipokutana na Vyama vya Siasa katika vikao mbalimbali ilivikumbusha vyama hivyo na serikali kuzingatia makubaliano ya pande zote, kuyafuata na kuyatekeleza maadili ya uchaguzi katika kipindi chote cha kampeni.

Hivyo amesema katika uchaguzi wa mwaka huu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020, Tume haitarajii kuona Vyama vya Siasa vikilalamika kuhusu ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi, badala ya kuchukua hatua stakihi za kisheria kwenye mamlaka husika.

Amebainisha hatua hizo kuwa ni pamoja na kuzitumia kamati za maadili, ambazo zimepewa mamlaka ya kushughulikia malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi husasan katika kipindi cha kampeni.

Jaji Kaijage amekumbusha kuwa kamati za maadili tayari zimeundwa kuanzia ngazi ya Kata kwa uchaguzi wa Madiwani, ngazi ya Jimbo kwa uchaguzi wa Wabunge na ngazi ya Taifa kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Makamu wa Rais na Kamati ya Rufaa kwa wale ambao hawataridhika na maamuzi ya kamati nyingine.

“Kamati hizo zimepewa uwezo wa kuyashughulikia malalamiko ya ukikwaji wa maadili ya uchaguzi. Aidha, mlalamikaji asiporidhika na maamuzi ya kamati katika ngazi husika anaweza kukata rufaa. Ikumbukwe kuwa wajumbe wa kamati hizo walio wengi ni wawakilishi kutoka kila Chama cha Siasa kilichosimamisha mgombea katika ngazi husika.”, amesema Jaji Kaijage na kuongeza kuwa:

“Ni muhumu kwa wadau wa uchaguzi, vikiwemo Vyama vya Siasa, wagombea wa nafasi mbalimbali na wananchi kwa ujumla, kutambua kwamba wakati huu ambapo Tume inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, utekelezaji wa sheria nyingine za nchi haujasimama. Hivyo kila mwananchi anashauriwa kujihadhari na maneno ama vitendo ambavyo vinatishia amani na utulivu uliopo nchini kwa kisingizio cha uchaguzi.”

Jaji Kaijage amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kusoma kitabu cha Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea ya Mwaka 2020. Kitabu hicho kina ufafanuzi wa mchakato wote wa uchaguzi kuanzia uteuzi wa wagombea, pingamizi, rufaa, kampeni na maadili, mawakala wa Vyama vya Siasa, hatua za upigaji kura hadi kutangaza matokeo.

Chanzo: Tovuti ye NEC (www.nec.go.tz)
 
CCM mpya imevuruga sana nchi yetu,na ikiendelea kubaki madarakani nchi itateketea kabisa.
 
Shida kubwa Ni huyo anayekunywa kikombe cha Loliondo kwenye hiyo Avater yako.

Hapendi haki Aman wala Demokrasia. Amejawa chuki kiburi na majivuno.

Watanzania Tugutuke.
 
Kwanza NEC niwape hongera kwa kurudisha wagombea wa upinzani. Nawapa hongera kwa sababu sasa wapambe tutapata maji ya kunywa toka kwa wagombe.

Maisha yalishakuwa magumu tukadhani yale ya serikali za mitaa yamejirudia. Sasa tajeni majimbo nione kama waziri wangu yumo ili nipige pesa yangu. Mie ndiye mpambe wake mkuu.
 
NEC wahuni tu hao

Safar hii ndio watajua.

Wapuuzi wanataka hao 15 wataje yale majimbo ambayo kwao kushinda ni rahisi.

NEC ni CCM kama walivo Polisi.
 
Kwanza NEC niwape hongera kwa kurudisha wagombea wa upinzani. Nawapa hongera kwa sababu sasa wapambe tutapata maji ya kunywa toka kwa wagombe. Maisha yalishakuwa magumu tukadhani yale ya serikali za mitaa yamejirudia. Sasa tajeni majimbo nione kama waziri wangu yumo ili nipige pesa yangu. Mie ndiye mpambe wake mkuu.
Umeandika kwa uchungu sana.
 
Mpambe maana yake ni kibaraka wake? Au nimekosea?
 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutoa matokeo ya rufaa za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020.

Leo tume imetoa matokeo ya rufaa 55 kama ifuatavyo:

1. Imekubali rufaa 15 na kuwarejesha wagombea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.

2. Imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa.

3. Imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.

Ushenzi mkubwa huu na lazima haki ipatikane na wahusika wachukuliwe hatua.
 
Back
Top Bottom