Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Aise dah.kama hayo yanayofanyika kwako ndo unaita weledi basi hii nchi ina safari ndefu sana yakujikwamua toka kwenye lindi la ujinga.Weledi unaozungumzia ni upi,kwasababu ili kuwe na weledi ni lazima haki itendeke kwa usawa.Je nikweli kuna haki sawa kwa wote?.
Inawezekana hujui maana ya weledi katika kutekeleza usimamizi wa sheria; kwako wewe weledi ni kukubaliwa matakwa yako tu.
 
Wapuuzi sana ninyi, mnajifanya ni Tume huru wakati kila mtu anaona namna mnavyotekeleza majukumu yenu kwa kumfurahisha Magufuli. Nchi hii ikiingia kwenye machafuko lawama na laana zote zitakua juu yenu MILELE.
Nchi ipo kwenye mikono salama ya Jemedari Magufuli nikutoe wasiwasi machafuko hayawezi kutokea.
 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutoa matokeo ya rufaa za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020.

Leo tume imetoa matokeo ya rufaa 55 kama ifuatavyo:

1. Imekubali rufaa 15 na kuwarejesha wagombea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.

2. Imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa.

3. Imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.

Mleta uzi ungetufanyia update ya ordodha mpya au bado tume iko na majina.Tuwekee kadiri yanavyotoka.Tunataka tuangalia other legal options kwa wale ambao wamezuiliwa so tunahitaji full list
 
Hata nami nime fanya kazi na huyu Mahela, kwanza ni kada mwaminifu wa Ccm, pili ni mwoga hana maamuzi akikoromewa na mamlaka iliyoko juu yake. Refer Jerry Muro alivyo mfokea mbele ya media.
Kumbe huyu ndo yule Dr aliyefokewa na Muro? Ohoo hakuna kitu hapo.
 
Amani yetu ipo mikononi mwetu wenyewe. Sie ndo tunaamua kuliamsha au la. Tutakao umia au kutokuumia na maamuzi yetu pia ni sisi wenyewe. Tusitake kukwepa majukumu kwa kubebesha mzigo NEC.
Kabisa mkuu....
 
Naona orodha ya Terehe nyingine haiwekwi ili tujue nani kapita na nani kakwama
 
Back
Top Bottom