Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
NEC leo inatarajiwa kutangaza waombaji walioteuliwa kugombea urais wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Wagombea hao walitakiwa kupata wadhamini 200 kila mkoa kutoka mikoa 10 na kati ya hiyo miwili ya Zanzibar
Tanzania ina vyama 19 vya siasa vyenye usajili, viwili TLP na UDP havikufanya mchakato wa kupata wagombea urais kwa kuwa vimeamua kumuunga mkono mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli
Wagombea kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), UPDP, DP na NCCR-Mageuzi jana walifika katika ofisi za makao makuu ya NEC kuhakiki taarifa na ujazaji wa fomu kama ziko sahihi.
Kwa mujibu wa ratiba ya NEC baada ya wagombea kurejesha fomu, itachambua, itapitisha majina na kutangaza wale walioteuliwa ifikapo leo saa 10 jioni.
Majina hayo yatakaa kwenye ubao wa matangazo hadi kesho saa 10 jioni ikiwa ni fursa iliyotolewa na NEC kwa wale wanaotaka kuwawekea pingamizi wateule. wagombea kuanza kampeni.
Uteuzi huo utafanyika katika ofisi za makao makuu ya NEC, Njedengwa jijini Dodoma. Mwanzoni mwa mwezi huu, NEC ilikutana na vyama vya siasa na pamoja na mambo mengine, ilitangaza kuwa fomu za uteuzi wagombea urais zingeanza kutolewa Agosti 5 hadi 25 mwaka huu, Dodoma.
Wagombea 17 wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea urais akiwemo Seif Maalim Seif (AAFP), Philip Fimbo ( DP), Leopard Mahona (NRA), John Magufuli (CCM), Qeen Sendiga (ADC) , Mutamwega Mgaiwa (SAU) naYeremia Maganja (NCCR Mageuzi).
Wengine waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa ni Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Bernard Membe (ACT Wazalendo), Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini), na Tundu Lissu (Chadema).
Wagombea wengine ni Hashim Rungwe (Chauma), Khalfan Mohamed Mazurui (UMD), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), David Mwaijojele (CCK), John Shibuda (ADA-TADEA, na Maisha Muchunguzi (NLD).
Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 waombaji 11 walichukua fomu NEC, wawili hawakuzirudisha, na mmoja alirejesha nje ya muda uliokuwa umepangwa hivyo kulikuwa na wagombea wanane.
Katika uchaguzi wa mwaka huu, kati ya wagombea 17 waliochukua fomu za uteuzi NEC, wanawake ni wawili Cecilia Augustino Mwanga, Qeen Sendiga na kuna wagombea wenza watano wanawake.
Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amesema fomu kwa ajili ya ubunge na udiwani zingetolewa makao makuu ya halmashauri za wilaya yalipo majimbo na za udiwani zingetolewa kwenye kata husika kuanzia Agosti 12 hadi leo.
Kukamilika kwa kazi hiyo kutatoa fursa kwa vyama kuanza kampeni kwa wagombea urais, ubunge na udiwani. Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu zinatarajiwa kuanza kesho Agosti 26 hadi Oktoba 27 mwaka huu.
Oktoba 28 Watanzania waliojiandikisha kupiga kura watatumia haki yao hiyo kuchagua viongozi wao. Kwa mujibu wa NEC daftari la wapigakura kwa sasa lina jumla ya wapiga kura milioni 29,188,347, vituo vyakupigia kura 80,155 na kila kituo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.
NEC pia imetangaza kuwa kama ilivyokuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 mwaka huu kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 264 yakiwemo 214 ya Tanzania Bara na 50 ya Zanzibar.
UPDATES
NEC YAANZA KUBANDIKA MAJINA YA WAGOMBEA KUTOA NAFASI YA PINGAMIZI
Zoezi la kubandika majina ya walioteuliwa kugombea kiti cha Rais na Makamu wa Rais linaendelea nje ya Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
Hatua hii inatoa fursa kwa watu walioruhusiwa kisheria kuweka pingamizi dhidi ya wagombea hao kuweka pingamizi zao. Mwisho wa kuweka pingamizi ni kesho tarehe 26 Agosti 2020, saa 10 jioni.
Wanaoruhusiwa kuweka pingamizi ni Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.