Bora Ubwabwa wa Rungwe Kuliko Lissu; Mpinga Maendeleo
Nimewasikiliza kwa makini sana Wagombea wa Urais kwa vyama vya Upinzani na nimegundua Mgombea makini ni Hashimu Rungwe kutokana na kuwa na sera ambazo zinajali matatizo ya Watanzania kuliko wagombea wengine wa upinzani.
Rungwe ni mgombea imara asiyelalamika kama Mtoto wa Kambo Tundu Lissu anachokifanya yeye ni kunadi sera ya kuwapatia Watanzania Ubwabwa, hasa wanafunzi ili waweze kusoma na kufaulu.
Lissu ametembea Mikoa 16 hajawahi kuwaambia Watanzania atawafanyia nini zaidi ya kulalamika na kuwafokea kama Mbwa Koko anayekaribia Kufa , au Malaya aliyetapeliwa hela na Mwanaume.
Lissu akilalamika kuhusu igizo lake la kujipiga risasi, utadhani Tanzania kuna watu wanakufa kwa Corona, utadhani Tanzania hakuna Hospitali za Rufaa au Vituo vya afya, utadhani hakuna Flyover, au hakuna umeme.
Lissu aelewe Watanzania wasasa sio kama wale wa zamani, Watanzania hawamuhitaji mgombea anayelialia na kujifanya yatima Watanzania wanamtaka mgombea Jembe na imara atakayezungumzia matatizo yao.