Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Uchaguzi, (NEC), Lawamani Kuwaengua Wagombea Kwa Hoja Nyepesi Nyepesi, Je ni Ukiukwaji wa Haki za Binaadamu? Jicho Letu

Acha kulalamika kama mtu asiyefahamu ukweli wa mambo. Mchakato wa kura za maoni ndani ya Ccm ilikuwa ni ushahidi tosha kuwa mwaka huu upinzani haikupata wagombea wenye elimu na sifa za kutosha.
Kama nafasi moja iligombewa na watu 50 au zaidi ni wazi kuwa Ccm walipata wagombea bora na hii ni sababu kila mtu mwenye elimu nzuri na sifa bora alitaka agombee kupitia Ccm.
Upinzani ulibaki kujichotea hovyohovyo hata wasiokuwa na umakini kujaza fomu na kusoma ili mradi waonekane wamesimamisha wagombea.
 
P , naona leo umeamua kuusema ukweli kiaina sio . Tume inatekeleza maagizo kutoka juu kwa mhutu ndio chanzo cha yote . Tume haina mamlaka ya kumtoa mgombea yoyote yule ,kazi Yao ni kusimamia zoezi la uchaguzi , wenye haki ya kumchagua mgombea au kumkata Ni wananchi sio tume .CCM please rudisheni nchi yetu toka mikononi mwa mhutu .
 
Tunaomba wanasheria atusaidie kushtaki hii tume ili hivyo vipengele virekebishwe
 
Kwa CCM neno haki haliko kwenye kamusi zao. Kwa tume isiyokuwa huru hakuna maajabu kwa hayo yanayo tokea. Ukisoma na michango humu utashangaa great thinkers wanavyo jigeuza "great sinkers" na kuhalalisha ushenzi unaofanyika na tume. Ni fahari yetu kuona mtu amepita bila kupingwa wakati tunajua ushenzi uliotendeka kuwa na matokeo hayo. Shenzi kabisa.
 
Kule zanzibar wakati wakutupilia mbali pingamizi dhidi ya maalim hoja ilikuwa wazi kuwa, makosa pekee yanayoweza kumuengua mgombea ni yale ambayo kama yataruhusiwa kubaki kama yalivyo yanaweza kumnufaisha mgombea dhidi ya mpinzani wake na kwa hivyo taarifa hizo ziwe zililenga kupotosha ili kujinufaisha, otherwise dosari za kimaandishi zisizokuwa na lengo la kunufaika dhidi ya mpinzani wako hazina msingi kisheria wa kumuengua mgombea.
 
Tume imeshapoteza uhalali wa kuitwa tume ya uchaguzi.

Ni heri wafungashe virago waondoke kwenye ofisi zetu badala ya kuzitia najisi ofisi za umma.

Yanayofanywa na tume ya uchaguzi ni kielelezo halisi cha matumizi mabaya ya kodi za watanzania.

Tume inatumia kodi za watanzania kuvunja haki za watanzania huu ushenzi haukubaliki.
 
Tume inapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria siyo matakwa binafsi ya mteuzi wao.

Kama wao wameamua kupindisha sheria ili kulipa fadhila unataka tumlaumu mpewa fadhila?

Walipaswa kutenda haki kama wakifutwa kazi tungejua wakumlaumu lakini kwa sasa wa kuwanyooshea mkono ni wao.
 
Leo umevaa uana habari mbobezi.

Kesho utakuwa kwaya ya praise team Ukiongoza mapambio na nguo za kijani.

Chagua moja kuwa baridi ama moto na si vuguvugu.

UTATAPIKWA.
 
 
Bila shaka kama ungeshiriki ungepinga nao wote na kutetea tume ya chama chenu na mfalme j
 
Ewe Mwenyezi Mungu mlaani muasisi wa uharamia huu wa kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…