johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
NEC imesema muda wa kutangaza wateule bado kwani kuna mapingamizi yanayoshughulikiwa na kwa mujibu wa ratiba mwisho wa kupokea mapingamizi ni leo 26 Agosti, saa 10.00 jioni. NEC imesema taarifa hizo zinaweza kupeleka uvunjifu wa amani
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson Mahera amesema, hadi kufikia 6:32 mchana, tume hiyo ilikuwa haijapokea pingamizi lolote la nafasi ya urais. Mwisho wa kuweka pingamizi ni saa 10 jioni.
Agosti 25,2020 tume ilikamilisha uteuzi wagombea urais na makamu, ubunge na udiwani, hatujatoa taarifa yoyote juu ya zoezi hili, tayari vyombo vya habari kadhaa vinaaza kutoa matokeo ya uteuzi huu, hii ni kinyume na sheria” Dk.Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC.
Mkurugenzi wa uchaguzi amesema haya... namnukuu
''Unapotangaza mtu amepita bila kupingwa hiyo inaweza pelekea uvunjifu wa amani pale mtu anapowekewa mapingamizi, isionekane ameshinda. Mimi mwenyewe mkurugenzi wa uchaguzi sijapata majina hayo rasmi''
''Kumekuwepo na dhana ambayo wanadhani watu wanakatwa, suala la uteuzi huwezi kukata mtu kwa matakwa yako, sababu tume inafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, tumeweka masharti ya uteuzi kwa urais wa Tanzania, ubunge na udiwani''
Unapowekea mtu pingamizi au ukiona hakuteuliwa maana yake hajatekeleza masharti, mtu akitoa maneno nje ya masharti hatafanikiwa sababau huyu akitaka rufaa atashinda. Tume inafanya kazi kwa uwazi na uhuru .