Mkuu rombo
JF-Expert Member
- Oct 18, 2012
- 1,556
- 422
Hatimaye ZEC wamefitilia mbali uchaguzi wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa tangazo la ZEC wameainisha mambo mawili ambayo yamepelekea kufutwa kwa uchaguzi huo ambayo ni mgombea mmoja kujitangaza mshindi kinyume cha taratibu na jambo lingine wamedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.
Wakuu.
Hapa kilichofanyika ni kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na sii wa muungano.
Hii ni kwa majibu wa mmoja wa wanasheria niliyempigia simu na kumuuliza.
So uchaguzi wa Zanzibar (serikali) ya mapinduzi hauhathiri matokeo ya kura za muungano.
Mfano: Tanzania bara Jimbo la ubungo, unapewa karatasi TATU (Raisi muungano, Mbunge na Diwani) . kwa ZANZIBAR unapewa 4 (Raisi wa Muungano, Raisi wa Zanzibar, Mwakilishi na Diwani) tatizo liko kwenye hizi tatu za mwisho sio ile ya TANZANIA yote!!! TANZANIA BARA Hawana karatasi ya nne ya URAISI ZANZIBAR kwahiyo HAWARUDII.
Hapa ndipo huwa namkumbuka Mh. Ally Keissy (Nkasi Kaskazini).
basi na tanzania bara wafute uchaguzi maana january alishatangaza kabla ya nec na nec ilisema ni tume peke yake ndio ina mamlaka ya kutangaza.
yani ccm ni majanga kwa kweli
Yes mkuu ndivyo ilivyokua.
Kulikua na meza mbili, ulikua unaanza kupiga kura za Zanzibar kwanza na ukishatumbukiza unaenda upande wa pili kuchukua karatasi mbili za wabunge wa jamuhuri na karatasi ya rais kisha unaenda kutumbukiza kwenye masanduku mengine.
Ndo maana tutaka serekali tatu
Mkuu ilitakiwa na Lowassa alalamike kwamba kura zake za Zanzibar zimechakachuliwa then time ndio ingefuta matokeo ya muungano Zanzibar.Mkuu ebu muulize huyo mwanasheria wako, kama kura zote zilipigwa kwenye chumba kimoja kwa wakati mmoja haoni kuwa sababu zilizobatilisha matokeo ya ZEC zinabatilisha pia matokeo ya NEC. Mazingira ni hayo hayo, chumba cha kura ni hicho hicho muda ni huo huo!
Nadhani hili halina ubishi kwani wasimamizi wa uchaguzi wa muungano ni kwa upande wa Zanzibar ni ZEC, hivyo kama kulikuwa na maroroso, basi yataathiri pande zote.
Ila sijui kama busara inamashiko kwamba kama mgombea wa chama X kamshinda mgombea wa chama Y kwa kura ziadi ya idadi ya wapiga kura wa Zanzibar, basi aweze kutangazwa mshindi bila kujali kura za Zenj. HILI LINAWEZA KUZUA MGOGORO WA KIKATIBA
Sasa umeniekewa, kwahiyo sasa ili na ya muungano yafutwe ni Lowassa anayetakiwa kulalamika na awe na ushahidi mkuu.hizo meza mbili zilikuwa ndani ya chumba kimoja au vyumba viwili tofauti. kama chumba kimoja ni batili hayo matokeo ya muungano
kura za urais wa jamhuri ya muungano zinasimamiwa na NEC si ZEC
Katika hali ya kushtua Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) imetangaza kuyafuta Matokeo ya urais wa Zanzibar.
Yadaiwa Uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.
Imeahidi kutangaza tarehe rasmi ya kurudiwa uchaguzi.
====
Statement:
VIDEO:
Chanzo: ZBC TV
Mkuu ilitakiwa na Lowassa alalamike kwamba kura zake za Zanzibar zimechakachuliwa then time ndio ingefuta matokeo ya muungano Zanzibar.
ZEC haina mamlaka kwa NEC na NEC hawana mamlaka kwa ZEC, hivyo uchaguzi uliyoahirishwa/ kufutwa ni wa Zanzibar tu , ila matokeo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapo salama