Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Hatimaye ZEC wamefitilia mbali uchaguzi wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa tangazo la ZEC wameainisha mambo mawili ambayo yamepelekea kufutwa kwa uchaguzi huo ambayo ni mgombea mmoja kujitangaza mshindi kinyume cha taratibu na jambo lingine wamedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

kazi kweli kweli na huku mamvi nae akijitangazia ushindi itakuaje watafuta???
 
Wakuu.
Hapa kilichofanyika ni kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na sii wa muungano.
Hii ni kwa majibu wa mmoja wa wanasheria niliyempigia simu na kumuuliza.
So uchaguzi wa Zanzibar (serikali) ya mapinduzi hauhathiri matokeo ya kura za muungano.

Mkuu ebu muulize huyo mwanasheria wako, kama kura zote zilipigwa kwenye chumba kimoja kwa wakati mmoja haoni kuwa sababu zilizobatilisha matokeo ya ZEC zinabatilisha pia matokeo ya NEC. Mazingira ni hayo hayo, chumba cha kura ni hicho hicho muda ni huo huo!
 
Mfano: Tanzania bara Jimbo la ubungo, unapewa karatasi TATU (Raisi muungano, Mbunge na Diwani) . kwa ZANZIBAR unapewa 4 (Raisi wa Muungano, Raisi wa Zanzibar, Mwakilishi na Diwani) tatizo liko kwenye hizi tatu za mwisho sio ile ya TANZANIA yote!!! TANZANIA BARA Hawana karatasi ya nne ya URAISI ZANZIBAR kwahiyo HAWARUDII.


Nakuona wewe ni bush lawyer. Watu walewale, jimbo lilelile, wasimamizi wa chumba kile kile. Msimamizi harafu unasema yaha menigine ni safi ya jamhuri, ila ya zenji ni batili? Tafakali!
 
Ujinga tu nanuhafidhina. Maalim alikuwa sahihi kutajantakwimu. Mbona Makamba kafingua vituo vya kutangazia matokeo na anatumia tweeter kwa hash tag #tanzaniadecides. Ana kituo kingine Kenya.
 
basi na tanzania bara wafute uchaguzi maana january alishatangaza kabla ya nec na nec ilisema ni tume peke yake ndio ina mamlaka ya kutangaza.

yani ccm ni majanga kwa kweli

ni majanga kabisa sheria iwaguse wapinzani tu, wao wako juu ya sharia, ving'ang'anizi hawakubali kushindwa, nilikuwa ccm lakini uchagu ukirudiwa znz naichagua cuf, kumbe ccm ndio waroho wa madaraka
 
Mwenyeketi NEC jaji Lubuva hatambui kufutwa kwa matokeo ya Zanzibar na ZEC CCM imekula kwao.
 
Yes mkuu ndivyo ilivyokua.
Kulikua na meza mbili, ulikua unaanza kupiga kura za Zanzibar kwanza na ukishatumbukiza unaenda upande wa pili kuchukua karatasi mbili za wabunge wa jamuhuri na karatasi ya rais kisha unaenda kutumbukiza kwenye masanduku mengine.

hizo meza mbili zilikuwa ndani ya chumba kimoja au vyumba viwili tofauti. kama chumba kimoja ni batili hayo matokeo ya muungano
 
Ndo maana tutaka serekali tatu

SERIKALI TATU isaidie nini? unajua serikali inahitaji mambo makuu matatu, REVENUE, EXECUTIVE na DEFENCE. sasa hiyo serikali yako ya tatu unayotaka wewe itakuwa na EXECUTIVE asiye na nguvu yoyote (mana haitakuwa na wananchi), REVENUE ya kuomba omba (kutoka visiwani na bara) na DEFENCE itakuwa wanajeshi wa kukodi (maana haina wananchi)? ..hiyo itakuwa serikali au vioja ???
 
Mkuu ebu muulize huyo mwanasheria wako, kama kura zote zilipigwa kwenye chumba kimoja kwa wakati mmoja haoni kuwa sababu zilizobatilisha matokeo ya ZEC zinabatilisha pia matokeo ya NEC. Mazingira ni hayo hayo, chumba cha kura ni hicho hicho muda ni huo huo!
Mkuu ilitakiwa na Lowassa alalamike kwamba kura zake za Zanzibar zimechakachuliwa then time ndio ingefuta matokeo ya muungano Zanzibar.
 
Nadhani hili halina ubishi kwani wasimamizi wa uchaguzi wa muungano ni kwa upande wa Zanzibar ni ZEC, hivyo kama kulikuwa na maroroso, basi yataathiri pande zote.

Ila sijui kama busara inamashiko kwamba kama mgombea wa chama X kamshinda mgombea wa chama Y kwa kura ziadi ya idadi ya wapiga kura wa Zanzibar, basi aweze kutangazwa mshindi bila kujali kura za Zenj. HILI LINAWEZA KUZUA MGOGORO WA KIKATIBA

ZEC haina mamlaka kwa NEC na NEC hawana mamlaka kwa ZEC, hivyo uchaguzi uliyoahirishwa/ kufutwa ni wa Zanzibar tu , ila matokeo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapo salama
 
hizo meza mbili zilikuwa ndani ya chumba kimoja au vyumba viwili tofauti. kama chumba kimoja ni batili hayo matokeo ya muungano
Sasa umeniekewa, kwahiyo sasa ili na ya muungano yafutwe ni Lowassa anayetakiwa kulalamika na awe na ushahidi mkuu.
 
kura za urais wa jamhuri ya muungano zinasimamiwa na NEC si ZEC

Mkuu sijaelewa bado kwani hili bandiko hapa chini lina maana gani? Je kulikuwa na wasimamizi wa ZEC na NEC huko vituoni?

Katika hali ya kushtua Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) imetangaza kuyafuta Matokeo ya urais wa Zanzibar.

Yadaiwa Uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.

Imeahidi kutangaza tarehe rasmi ya kurudiwa uchaguzi.

====
Statement:

vU05dG9.jpg

EdIidYV.jpg

BLhdlD9.jpg


VIDEO:

Chanzo: ZBC TV
 
Last edited by a moderator:
BREAKING NEWZ

Mwenyekiti wa NEC hatambui kufutwa uchaguzi Zanzibar. Kwa kufutwa uchaguzi Zanzibar, Tanganyika nako hakuna uchaguzi kwa kuwa uchaguzi wa NEC Zanzibar unasimamiwa na ZEC
 
Mkuu ilitakiwa na Lowassa alalamike kwamba kura zake za Zanzibar zimechakachuliwa then time ndio ingefuta matokeo ya muungano Zanzibar.

Lowassa hajachelewa so far, hata hivyo kwani ccm wali lodge official complain kuwa wameibiwa pemba? au zec wamefuta kutokana na kuona kasoro walizoziainisha kwenye barua yao?
 
ZEC haina mamlaka kwa NEC na NEC hawana mamlaka kwa ZEC, hivyo uchaguzi uliyoahirishwa/ kufutwa ni wa Zanzibar tu , ila matokeo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapo salama

Soma tamko uchaguzi wote umefutwa ZEC ni mawakala wa NEC Zanzibar
 
Back
Top Bottom