Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Siasa hizi..aisee kwa hiyo leo ZEC ndo wameona kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki,amaa kweli mtenda akitendewa........
 
Duh CCM wamekimbilia kwa refa, na refa katia mpira kwapani,
Nilitamani kuona ccm inapotea znz, lakini bara nilitamani kuona fisadi lowassa anapotezwa kabisa kwenye siasa za nchi hii, Alhamdulillahi dua yangu upande mmoja imepokelewa
Wazenji tulieni msikate tamaa, pigeni tena kura kwa wingi kuikataa ccm waibe mpaka washindwe kuiba
 
Nashawishika kuamini kuwa matokeo aliyosema Maalim Seif kuwataka ZEC watangaze mshindi yalikuwa sahihi. Tangu lini refa amalize mechi halafu aseme hakuchezesha kwa haki?

Vv
 
Naamini hapa hatukosi majibu. Tume ya uchaguzi zanzibar imefuta uchaguzi wa visiwa hivyo. Naomba kujua,km zec imefuta uchaguzi huo kwa sababu walizozitaja,vp kuhusu kura za urais wa jamhuri ya muungano wa Tz??

Km uchaguzi wa zanzibar umefutwa na utaathiri matokeo ya urais wa jamhuri,uchaguzi wa Tz bara utabaki kuwa halali!!?? Naomba kuelimishwa.

Uchaguzi wa muungano hausimamiwi na ZEC, ni NEC mkuu...
 
Tunataka na hapa bara ufutwe january makamba alijitangazia matokeo ya majimbo
 
Watarudia CCM Maalim Seifu ameshatangaza hatarudia uchaguzi hata wakimfunga sawa
 
BREAKING NEWS.

Uchaguzi Zanzibar Umefutwa Rasmi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imefuta uchaguzi wa Zanzibar

Sababu kubwa inayofichwa ni tume kutofautiana baada ya kupishana katika kuibeba CCM

Baadhi ya Wajumbe wa tume wamekubali kutenda haki Na kutokubali kuyumbishwa Na Serikali ya CCM

Hivyo kupelekea wao wenyewekutofautiana na kupelekea kushikana mashati
 
Hapo yakirudiwa lazima washinde

Wanajua matokeo ya bara yatawa influence wapiga kura Zanzibar. Na vile vile inategemea uchaguzi utarudiwa lini, Kama ni baada ya Magufuli kuanza kazi anaweza kuanza kwa moto ika influence wapiga kura wa Zanzibar pia.
 
Kwa hiyo matokeo ya Bara yatasubiri au inakuwaje ?Maana kuna kura za Bara kule Zanzibar
 
Wanajiandaa kupeleka nyomi a.k.a mtiti wa askari na wapiga kura. Kama hali ndio hii haina ahaja ya kufanya uchaguzi kuwasimamisha watu juani

Wala siyo askari wanaopiga kura! Raia watiifu wa chama ndio huvuka kuokoa jahazi!
 
Hatimaye ZEC wamefitilia mbali uchaguzi wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa tangazo la ZEC wameainisha mambo mawili ambayo yamepelekea kufutwa kwa uchaguzi huo ambayo ni mgombea mmoja kujitangaza mshindi kinyume cha taratibu na jambo lingine wamedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

Bara kuna mtu alisema tuna muapisha magufuli tarehe 29/10 kabla hata rais hajajulikana, Je hiyo haikuwa kujitangazia ushindi?
 
jamani kufuatia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huko Zanzibar hakuathiri matokeo ya Uraisi wa JMT??? wanasheria tunaomb mwongozo hapa....
 
Duh CCM wamekimbilia kwa refa, na refa katia mpira kwapani,
Nilitamani kuona ccm inapotea znz, lakini bara nilitamani kuona fisadi lowassa anapotezwa kabisa kwenye siasa za nchi hii, Alhamdulillahi dua yangu upande mmoja imepokelewa
Wazenji tulieni msikate tamaa, pigeni tena kura kwa wingi kuikataa ccm waibe mpaka washindwe kuiba
Huyo Jecha ajue kua kuna the Hague, na akumbuke yaliyotokea Kenya enzi za Sam Kivuitu
 
Back
Top Bottom