Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona January amejitangazia ushindi na ametangaza matokeo. Again sheria ni msumeno lazima ukate kote.kujitangazia ushindi kunaathiri vipi matokeo ?
hii kali !
maagizo ya DODOMA hayo !
Mwenyekiti wa uchaguzi zanzibar amefuta uchaguzi wote kisiwani huko... tutaendelea kujuzana
Naamini hapa hatukosi majibu. Tume ya uchaguzi zanzibar imefuta uchaguzi wa visiwa hivyo. Naomba kujua,km zec imefuta uchaguzi huo kwa sababu walizozitaja,vp kuhusu kura za urais wa jamhuri ya muungano wa Tz??
Km uchaguzi wa zanzibar umefutwa na utaathiri matokeo ya urais wa jamhuri,uchaguzi wa Tz bara utabaki kuwa halali!!?? Naomba kuelimishwa.
Azam tv pia wamesema, maalim kaliwa masikini
Kwanini wanachosema wao kinafuatwa? Sheria iwe ni Kwa vyama vyote?Uchaguzi ukirudiwa CCM wanajua matokeo ya bara yata wa influence wapiga kura Zanzibar. Wapinzani kuweni makini?
Hapo yakirudiwa lazima washinde
Wanajiandaa kupeleka nyomi a.k.a mtiti wa askari na wapiga kura. Kama hali ndio hii haina ahaja ya kufanya uchaguzi kuwasimamisha watu juani
Hatimaye ZEC wamefitilia mbali uchaguzi wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa tangazo la ZEC wameainisha mambo mawili ambayo yamepelekea kufutwa kwa uchaguzi huo ambayo ni mgombea mmoja kujitangaza mshindi kinyume cha taratibu na jambo lingine wamedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.
Huyo Jecha ajue kua kuna the Hague, na akumbuke yaliyotokea Kenya enzi za Sam KivuituDuh CCM wamekimbilia kwa refa, na refa katia mpira kwapani,
Nilitamani kuona ccm inapotea znz, lakini bara nilitamani kuona fisadi lowassa anapotezwa kabisa kwenye siasa za nchi hii, Alhamdulillahi dua yangu upande mmoja imepokelewa
Wazenji tulieni msikate tamaa, pigeni tena kura kwa wingi kuikataa ccm waibe mpaka washindwe kuiba