Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

This is a joke and this guy is a total joke. Huko kupigana kwa makamishna wa tume kuna uhusiano gani na matokeo?Yeye kushindwa kufanya kufanya kazi yake kucommand nidhamu ndani ya tume kunahusika vipi na suala la uchaguzi kuwa au kutokuwa huru na wa haki? Kwa nini wasiyashughulikie hayo matatizo yaliyojitokeza specifically? Na kwa nini nani ameshinda? This is insane. Maalim usikubali katu katu uchaguzi kurudiwa ikibidi usifanyike kabisa au wafanye na ADC na dunia itambue hivyo.
 
ni ngumu sana kuproove kwamba kura za urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania hazijaathirika na hizo sababu za zec. Ikiwa mpiga kura ni yule yule, kituo ni kile kile, msimamizi wa kituo ni yule yule na mazingira ni yale yale.

rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania anatokana na kura za urais za bara na visiwani, hivyo kama kura za kura za kule zanzibar ni batili-ndio maana uchaguzi umefutwa, means hata kura za urais za jamuhuri ya muungano wa tanzania ni batili pia.

Kura zote ni batili, other wise tume-nec ihesabu tu kura za huku bara, na isubiri mpaka zanzibar watakapo fanya uchaguzi wao tena, ndipo matokeo ya urasi wa jmt yajumlishwe upya. Hivyo kikwete by that time ataendelea kubaki madarakani

wale waliosema tareh 29 oktoba watamuapisha rais basi wasitukane mamba na huku hawaja vuka mto. Haki ya mtu huwa haipotei.

Asante mungu
 
Maalim Seif uvumilivu nasubira ilikushinda sasa mkono wa she ria unakufuata.
 
...hata kama wakiurudia seif linda kura zako,pigeni kura,hesabu,kama umeshinda tangazia dunia..hakuna kurudi nyuma.
Haki yako inacheleweshwa tu,ila iko pale pale.
 
Maelezo yako yamejikita kisheria au umeongea kwa mihemko tu? Naomba maelezo ya kisheria au kikatiba..pls!!

kikatiba ni kuwa , rais wa muungano atapigiwa kura na wananchi wa zenji na bara,
sasa leo kura zote zilizopigwa zenji zimetangazwa ni batili,
hii inamaanisha kura walizopata wagombea wa bara kutoka zenji ni batili inabidi either uchaguzi wote tz bara urudiwe au rais wa muunagano asitangazwe mpaka uchaguzi wa zenji ukamilike.
 
Kama huelewi taratibu nyamaza! ZEC zanzibar ndio inayogawa majimbo yote ya uchaguzi. Hata majina hayo ya wapikupiga kura yaliratibiwa na hao hao ZEC kwa maneno ya Lubuva. Simply ni kwamba CCM kashindwa vibaya Zanzibar. Hao ZEC walipotangaza hawakujipanga na sasa impact yake ni nchi nzima. UCHAGUZI WA TANZANIA NAO UFUTWE!

Mbona kuna mikoa mingi uchaguzi umehairishwa, kwanini USIRUDIWE ZANZIBAR ??? ..Hii ni internal matter ya wana Zanzibar sio swala la kila mtu. Leo hii Ubungo wakitaka kurudia uchaguzi utafutwa na waanze upya, HAUWEZI kusema TANZANIA nzima WARUDIE UCHAGUZI.

Kwani Bara mliona picha ya MAALIM SEIF kwenye karatasi YOYOTE ?? ?? ?? Hili tatizo ni LOCAL jimboni Zanzibar sio TANZANIA nzima.... Wao wanapiga kote, kama Jimbo lolote, kura zinapigwa hierarchical ...(sijui kiswahili wanaitaje).
 
nadhani ni wakati wa dunia kuangalia ni jinsi gani uchaguzi wa tanzania ulivyo na vitimbwi sasa ni wakati wa cuf kutumia umoja wa ukawa naimani vyama vyote vnavyounda ukawa ni wakati wa kumsaidia seif
 
Tuna wagombea walioshika nafasi mbalimbali katika kinyang'anyiro cha urais. Sikujua athari ya hii sheria ya kujitangaza mshindi inaweza kupelekea uchaguzi kufutwa. Kumbe hata hao wanaoambulia kura mbili au tatu kwenye majimbo wakitaka uchaguzi urudiwe wala hawahitaji kutumia nguvu nyingi, ni kiasi tu cha kujitangaza mshindi. Kwa mantiki hiyo uchaguzi unaweza usiishe iwapo miongoni mwa wagombea atatokea kichaa ambaye kila inapofikia hatua ya kujumlisha matokeo basi anajitangaza mshindi na uchaguzi unafutwa na kurudiwa, na tena, na tena, na tena ...., labda aache kujitangaza mshindi!
 
Huku tunajitambua bana. Hatutaki mchezo katika haki yetu....!!!!! Huko bara kaeni na kukubalikubali kwenu...!!! Asa sijui Sheria inafatwa hapa au ndo ubabe tu basi....!!!!
 
Zilizofutwa ni Matokeo Ya Urais na Sio Ya Wabunge, madiwani wala Wawakilishi. Kwa hiyo Kura za Ubunge ziko pale pale

Wakuu someni bandiko hapo chuni, umefutwa uchaguzi wote.....

Katika hali ya kushtua Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) imetangaza kuyafuta Matokeo ya urais wa Zanzibar.

Yadaiwa Uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.

Imeahidi kutangaza tarehe rasmi ya kurudiwa uchaguzi.

====
Statement:

vU05dG9.jpg

EdIidYV.jpg

BLhdlD9.jpg


VIDEO:

Chanzo: ZBC TV
 
Last edited by a moderator:
Mkuuu unawezaje kuthibitisha kuwa hizo kura za muungano hazikuathiriwa na hizo dosari zec wasemazo.

Ikiwa mpiga kura ni yuleyule, alikuwa kituo hicho hicho, msimamizi ni yule yule, etc, kila kitu kilifanyika hapo kituoni wakati mmoja, sasa how come hizo dosari ziathiri tu kura za urais za maalimu seif na dr. Shein???

mkuu matokeo ysliyofutwa ni ya serikali ya mapinduzi na sii ya muungano.
Tambua kwamba wazanzibar wamechagua rais wa zanzibar na rais wa muungano.
na kasoro zipo kwenye uchaguzi wa rais wa zanzibar na sii rais wa muungano.
 
Zilizofutwa ni Matokeo Ya Urais na Sio Ya Wabunge, madiwani wala Wawakilishi. Kwa hiyo Kura za Ubunge ziko pale pale


Sikiliza vizur hiyo video. Wamefuta kutokana na KASORO nyingi sana.

 
Last edited by a moderator:
kuna sababu tisa zimetajwa hapo juu....Ina maana hizo haziifanyi Uchaguzi wa Rais wa Muungano upande wa Zanzibar kutokuwa batili??Kuwa mkweli usiegemee upande...

Mbona kuna mikoa mingi uchaguzi umehairishwa, kwanini USIRUDIWE ZANZIBAR ??? ..Hii ni internal matter ya wana Zanzibar sio swala la kila mtu. Leo hii Ubungo wakitaka kurudia uchaguzi utafutwa na waanze upya, HAUWEZI kusema TANZANIA nzima WARUDIE UCHAGUZI.

Kwani Bara mliona picha ya MAALIM SEIF kwenye karatasi YOYOTE ?? ?? ?? Hili tatizo ni LOCAL jimboni Zanzibar sio TANZANIA nzima.... Wao wanapiga kote, sisi tunapiga ya kwetu tu kama Jimbo lolote, kura zinapigwa hierarchical ..kijimbo na kitaifa, ARUSHA WAMEPIGA KURA ZA RAISI BARA LAKINI UBUNGE BAADAE. Kwahiyo Zanzibar za PAMOJA URAISI BARA ni sawa ila majimbo yaani RAISI wao ndio zinarudiwa.
 
Ukawa jitokezeni kutangaza Matokeo yenu ili na Bars uchaguzi ufutwe haraka sana.

Kura za Urais wa Muungano kule Zanzibar zitakua so halali tena.
 
Ni wakati sasa wa NEC nao kusitisha matokeo yao feki maana hata waliyoyapokea kutoka zanzibar ni batili
 
...ingekua ni magamba yameshinda halafu Seif alalamike haukuwa huru na haki wangerudia uchaguzi?
Kama tume ni yao,polisi wa kwao, na vyote vyao,inakuaje ccm mnalia lia uchaguzi haukua huru na haki?
Au mlikuja na huu ujanja wa uchaguzi haukua huru ili mpate sababu ya kurudia uchaguzi?
Amini nawaambia; as long as kura zitapigwa tena,nawaambia Seif ushindi uko palepale...mnauchelewesha tu.!! kwani waliompa kura jumapili,ndio hao hao watakaompa kura hiyo siku mtakayoipanga...
#vivaseif!!
 
Mkuu matokeo ysliyofutwa ni ya serikali ya mapinduzi na sii ya muungano.
Tambua kwamba wazanzibar wamechagua rais wa Zanzibar na rais wa muungano.
Na kasoro zipo kwenye uchaguzi wa rais wa Zanzibar na sii rais wa muungano.
....




Ndo nikakuuliza huyu rasi atakuwawa Tanganyika peke yake kama matokeao yake ya Zanzibar yamefutwa?
 
CUF msikubali hilo ndio bao la mkono lenyewe lizuieni lisitoke.
 
Back
Top Bottom