Tumeacha kutetea bandari zetu sasa tunatetea mwekezaji muislam, waziri muislam na rais muislam!

Tumeacha kutetea bandari zetu sasa tunatetea mwekezaji muislam, waziri muislam na rais muislam!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Ni rahisi sana kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao na CCM wanalifahamu vizuri jambo hili.

Hata kama kuna jambo baya sana kwa maslahi ya nchi yetu ukitaka likubalike basi wewe lipake rangi ya dini flani utaona mara moja watazuka watu na kulitetea kwa nguvu zao zote kwasababu tu jambo hilo lina rangi ya dini yao!

Suala la mkataba wa bandari limeonesha kuwa watanzania hawana misingi ya kusimamia isipokuwa mafungamano na dini zao.

Ni ajabu kubwa kwamba watu wapo tayari kuuza nchi yao kwa kuaminishwa kwamba hili ni jambo la kidini! CCM wanajua fika jambo hilo na wanalitumia sasa kama walivyolitumia kwenye chaguzi zilizopita dhidi ya CHADEMA na CUF.

Suala la bandari lilianza kujadiliwa vizuri kwa uzalendo lakini watu flani walipogungua linagusa dini yao sasa wamebadili hoja zao na bandari imekuwa suala la kidini.

Sakata la bandari sasa limekuwa suala la Uislamu; mwekezaji muislam, waziri mwislam na rais mwislam!
 
Miaka yote haya mambo ya udini hujitokeza pale anapotokea mtawala dhaifu, asiyeweza kuenenda vyema na majukumu yake ya kiofisi, hasa anapoanza kuharibu kwa ujinga wake mwenyewe, na nchi kuanza kumshinda.

Ndipo wanajitokeza wajinga wenzie wa imani yake na kuanza kumtetea, huwa wanafanya hivyo kwasababu wamezoea kuchanganya hisia na facts, kwangu ni vitu viwili ambavyo haviendani kabisa, kwani suala la imani na ubovu wa mkataba, ni mambo mawili tofauti.

CCM nao, kwa kutambua huo ujinga wao, huanza kuitumia karata ya udini pale wanapoona utetezi wao mwingine wote tumegoma kuusikiliza, hapo ndipo hugeukia kwenye dini kama karata yao ya mwisho, ila bahati mbaya kwao this time, kwenye hili suala la bandari zetu watanganyika, udini wao nao umegoma.

Hapa niwaase wale jamaa ambao hujidai kuogopa kujadili jambo lenye muelekeo wa kidini, wakijiona wastaarabu sana, kwa kuhofia kuwakwaza wa imani tofauti.

Watambue kwa kufanya kwao hivyo, ndipo wanawapa CCM na uhuni wao ushindi, jambo lolote lenye muelekeo wa kidini lazima lijadiliwe kwa umakini, penye ukweli usemwe with facts, pasiwepo unafiki, tusifichane. Muhimu heshima iwepo mwiongoni mwetu, ili siku nyingine CCM washindwe kuitumia hii karata yao pendwa ya turufu kutupoteza.

Sasa hapa ni kuamua, ama kusema kweli ituweke huru, tujikomboe kifikra, na tulikomboe taifa, au tufichane kwa hofu ya kuogopa dini zetu hivyo tusiambizane ukweli, ili CCM iendelee kutuchezea milele kwa kujua na kuutumia udhaifu wetu, kwa maslahi yao, chaguo ni letu..
 
Ni rahisi sana kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao na CCM wanalifahamu vizuri jambo hili.

Hata kama kuna jambo mbaya sana kwa maslahi ya nchi yetu ukitaka likubalike basi wewe lipake rangi ya dini flani utaona mara moja watazuka watu na kulitetea kwa nguvu zao zote kwasababu tu jambo hilo lina rangi ya dini yao!

Suala la mkataba wa bandari limeonesha kuwa watanzania hawana misingi ya kusimamia isipokuwa mafungamano na dini zao.

Ni ajabu kubwa kwamba watu wapo tayari kuuza nchi yao kwa kuaminishwa kwamba hili ni jambo la kidini! CCM wanajua fika jambo hilo na wanalitumia sasa kama walivyolitumia kwenye chaguzi zilizopita dhidi ya CHADEMA na CUF.

Suala la bandari lilianza kujadiliwa vizuri kwa uzalendo lakini watu flani walipogungua linagusa dini yao sasa wamebadili hoja zao na bandari imekuwa suala la kidini.

Sakata la bandari sasa limekuwa suala la Uislamu; mwekezaji muislam, waziri mwislam na rais mwislam!
Uzalendo ni kuchukua maaskofu na kwenda nao press conferences?
Uzalendo ni maaskofu kuacha makanisa na kwenda viwanjani kumtukana Rais?

Yaani uzalendo Tanzania wanao maaskofu tu?...
Wengineo wote hawana uzalendo??

Hao maaskofu wakati watu wanapigwa risasi uzalendo wao ulikuwa wapi??
 
Another thread ingine ya uwongo na uzushi . ..from you ..
Wewe Jana umeanzisha thread unasema askofu Mwamakula kasema Dpworld watajenga msikiti...

Dpw world wamejenga msikiti UK walipopewa bandari?
German walijenga msikiti walipopewa bandari?..
China walijenga msikiti walipopewa bandari
South Africa walijenga msikiti walipopewa bandari?
Belgium walijenga msikiti walipopewa bandari?

Yaani Dpworld waendeshe bandari nchi 92 Duniani kote huko wasijjenge msikiti ila waje wajenge msikiti Mbeya??

Na kuna wajinga wanakuona unaongea vya maana?
 
Tatizo nchi hii akiongoza mvaa kobasi kuna watu roho zinawawasha ata awe mwema kiasi gani,Mwalimu Nyerere alilia kuhusu ubinafshaji wa mashirika ya Umma lakini tulibinafsisha. Miaka kadhaa nyuma tumesaini mikataba ya reli SGR na bwawa la Mwalimu Nyerere rufiji,Tuna mkataba wa mradi wa umeme pia maporomoko ya Rusumo(Tanzania,Burundi na Rwanda) walalamikaji wa sasa hawajawai kulalamika popote na wala awahoji.
Tupendane
 
Uzalendo ni kuchukua maaskofu na kwenda nao press conferences?
Uzalendo ni maaskofu kuacha makanisa na kwenda viwanjani kumtukana Rais?

Yaani uzalendo Tanzania wanao maaskofu tu?...
Wengineo wote hawana uzalendo??

Hao maaskofu wakati watu wanapigwa risasi uzalendo wao ulikuwa wapi??
Shehe Ponda alivyotunguliwa Risasi Maaskofu walipiga kelele za kukemea Bakwata walikaa Kimya

Msamaria Mwema😂😂😂🔥
 
Kwani ni ubaya upi Kwa askofu ama shekhe kukubaliana na kuunga mkono hoja za Chama Fulani?

Tunapotaka demokrasia tujifunnze kuvumiliana pia. Hoja zijibiwe kwa hoja.

Nchi ni yetu sote, Dini sio za wote. Wacha Kila Mtu aongee mawazo yake na ajibiwe kwa hoja.
 
Back
Top Bottom