Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Mwanamke ambaye anaweza ishinda mitihani ya Dar ni wa kumuheshimu sana. Yani mwanamke hata awe na misimamo kiasi gani akija Dar lazima atafunwe na wajuba 😂😂😂
Nilikua staki kuchangia zaidi ya kusoma ila kusema ukweli

mwanamke alie dar akashinda mitihani ya hili JIJI mimi nampa Vyeo vyotee....
 
Mimi mchaga na babangu ananikazia lazima nioe mchaga nikitaka kuoa.japo babangu ni muislamu pure alieshika dini



Ila mimi ni mchaga rebel sina kabisa mambo yao ya kichaga na nitaoa yoyote sitaki limit kwenye maisha yangu.
Uyo mzee wako kweli kashika dini Ila haifuati dini...
 
Tatizo mnapenda wachaga lakini wao hawawapendi
Pumbavu sana kaoe /kaolewe kwenu hakuna watu huko? ?
Mimi nimeshuhudia kabsaaaa muhaya kanyimwa kuoa mrangi tena ameshamzalisha
Wazee wake wakampiga pin hawamtaki kabsaaaa huyo binti

Wamemtafutia muhaya mwenzake na ndoa ilishafungwa

Halafu sio lazima kuoa /kuolewa na kabila lingine tafuta wa kwenu kuondoa hizi lawama

Mnapenda kabila fulani kwa vile ni mafighter wa maisha ili unufaike nenda kwenu pumbavu kabsaa
Mbona mimi nimeoa kwetu Singida?
Tunakula maisha Hapa Denmark tuu

Kila kabila lina taratibu zake Hata wanangu nitataka waoe nyumbani

Period. !!!!!!

Mmesikia au niongoze sauti. ????

Mkuu acha hizo,mimi nina mchumba msichana wa Rombo tabia swaaafi wazazi pia wamenielewa sana.
 
Aiseee..mm Baba angu ni mchaga mama Kabila kingne,
Kiukweli cjawah kuishi uchagan hata lugha yao cjui kuiongea nahc mshua alibobea Sana mjini na alikua anafanya Mambo yake mengi Kwa kificho.huwezi amini Baba alikuja kufunga ndoa kimyakimya na mchaga mwenzake wakaanzisha familia,Mzee cjui alirogwa maana hata matunzo kwetu akawa hatoi mama ndo alitusomesha mungu saidia sasa hv kila mtu ana kazi yake ya maana.
Babu mzaa Baba alipofariki ndio tulienda huko na kukutana na familia nyingine ya Mzee lakini ubaguz ulijionyesha dhahiri..kwakua Nina mpunga wangu wa kutosha na Mzee analijua hilo akawa anajaribu Kama kubalance Mambo Ila mashangazi wakatukazia kimtindo.
Mambo yalipoisha mshua akatutambulisha pale pamoja na kazi tunazofanya nikaona mashangazi mishipa ya uso inawalegea mara ooh hawa pia ni wadogo zenu muwasaidie nikamjibu sawa.baadae mm na familia yangu tukajitia ndani ya ndinga tunaamsha japo walijidai ooh kuna Mambo ya Mila mm ckujali.
Kuna wakati ctaman kusema mm ni mchaga yaan nataman badili hata ukoo maana hata mwanamke ukimpenda ukimtajia jina la ukoo ana kukwepa.
WACHAGA NI WANA ROHO MBAYA KULIKO SHETANI.
NI WABINAFSI HATARI.


Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Pole sana
 
Kwa kweli dunia ina mambo ya ajabu sana. Exboyfriend wangu ni Mchaga wa milimani. Tumedumu naye katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitano. Lakini katika muda huo kumekuwa na ups and down nyingi sana ambapo tukikaa tunarekebisha maisha yanaendelea.

Kwao natambulika ingawa si rasmi. Na swali la kwanza waliloniuliza kwao mimi ni kabila gani.

Wakaonyesha kunipokea na kunijali ingawa haikuwa utambulisho rasmi.
Baada ya miaka yote, nimegundua mwenzangu ameanzisha mahusiano na binti wa kichaga, yupo chuo mkoani.

Nikajaribu kuongea na mwenzangu ambaye aliniambia hayupo serious naye na ndio maana muda wote yupo na mimi na hawezi kuniacha hata itokee nini.

Baada ya siku chache tena mwenzangu akawa anaendeleza mahusiano hadi kupigiana simu zao mbele yangu.

Nilichokifanya ni kumlazimisha jamaa kuchagua jambo moja, mimi au Mchaga mwenzake wa huko chuo.
Mwenzangu alionyesha ugumu sana sana sana kuniacha ila pia kule kwa Mchaga mwenzake pia hataki kuacha.

Anachonieleza ni kuwa amenizoea, namjali, mimi ni part ya maisha yake, hivyo hataki niondoke ila wazazi wake wanataka apeleke mtu Mchaga na si kabila lingine.

Nimeamua kuondoka katika maisha yake ingawa mpaka sasa mwenzangu analeta ugumu sana katika kuchukua vitu vyangu nilivyoacha kwake. Ananidanganya na kunizungusha sana lakini kiukweli maisha anayotaka niyaishi, si maisha ninayoyataka.

Nimehuzunika tu kwa kuwa tumefika mwisho kwa sababu mimi si MCHAGA. Ubaguzi ambao Wachaga wengi wanao.

Nashukuru Mungu kwa kunipa pumzi hii hata nimeweza kulitoa dukuduku hili kwa ndugu zangu wana JF.
Pamoja na comment za kibabe ila kiukweli huwa ninafarijika sana ninaposhare na kukosolewa au kuonyeshwa njia sahihi.
Ukiona hujakiwa mahali sio fungu lako huyu,yani tunaita vyasaka
 
Back
Top Bottom