Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Kwa kweli dunia ina mambo ya ajabu sana. Exboyfriend wangu ni Mchaga wa milimani. Tumedumu naye katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitano. Lakini katika muda huo kumekuwa na ups and down nyingi sana ambapo tukikaa tunarekebisha maisha yanaendelea.

Kwao natambulika ingawa si rasmi. Na swali la kwanza waliloniuliza kwao mimi ni kabila gani.

Wakaonyesha kunipokea na kunijali ingawa haikuwa utambulisho rasmi.
Baada ya miaka yote, nimegundua mwenzangu ameanzisha mahusiano na binti wa kichaga, yupo chuo mkoani.

Nikajaribu kuongea na mwenzangu ambaye aliniambia hayupo serious naye na ndio maana muda wote yupo na mimi na hawezi kuniacha hata itokee nini.

Baada ya siku chache tena mwenzangu akawa anaendeleza mahusiano hadi kupigiana simu zao mbele yangu.

Nilichokifanya ni kumlazimisha jamaa kuchagua jambo moja, mimi au Mchaga mwenzake wa huko chuo.
Mwenzangu alionyesha ugumu sana sana sana kuniacha ila pia kule kwa Mchaga mwenzake pia hataki kuacha.

Anachonieleza ni kuwa amenizoea, namjali, mimi ni part ya maisha yake, hivyo hataki niondoke ila wazazi wake wanataka apeleke mtu Mchaga na si kabila lingine.

Nimeamua kuondoka katika maisha yake ingawa mpaka sasa mwenzangu analeta ugumu sana katika kuchukua vitu vyangu nilivyoacha kwake. Ananidanganya na kunizungusha sana lakini kiukweli maisha anayotaka niyaishi, si maisha ninayoyataka.

Nimehuzunika tu kwa kuwa tumefika mwisho kwa sababu mimi si MCHAGA. Ubaguzi ambao Wachaga wengi wanao.

Nashukuru Mungu kwa kunipa pumzi hii hata nimeweza kulitoa dukuduku hili kwa ndugu zangu wana JF.
Pamoja na comment za kibabe ila kiukweli huwa ninafarijika sana ninaposhare na kukosolewa au kuonyeshwa njia sahihi.
Pole dear, hajakupenda tu
Wadada wa kichaga wanabaguliwa Sana jaman waache waolewe na kaka zao
 
Yaani ukitaka usalama wa roho yako kama wewe si mchaga basi usioe /kuolewa na mchaga....yale matambiko wanayofanyaga Kila mwisho wa mwaka hawatakuruhusu ushiriki maana wewe ni CHASAKA
Mmhhh acheni uongo, hamna matambiko yoyote. Watu wasiende kwao kufurahi??
 
Kuna dada yangu wa ukoo aliolewa uchagani (yeye ni kabila tofauti), Mume wake akafariki, aisee katika vitu niliona wachaga ni wanyama ni baada ya kumfukuza yule sister kwenye nyumba na kumnyang'anya kila kitu, ikiwa na pamoja na miradi ambayo ingewasaidia kusukuma maisha. Sister akarudi mkoa mwingine kuanza na maisha upya akiwa na watoto wanne, watatu wakiwa shule mmoja ndio alikuwa mdogo. Huwezi amini wale watoto nusura waache shule kwa kukosa ada bahati nzur kama familia tuligawana mtoto mmoja mmoja ndo wakaendelea na shule. Wale watoto ukiwaita wachaga wanakuonesha kuchukia Live... hawapendi kbs hilo kbl ingawa ndo hvy wachaga by birth!!
Wachaga utu kwao ni pesa na mali tu.
Dada yako aliolewa kwenye familia yenye njaa,hakuna familia yenye maisha yake hubagua damu yao...istoshe hilo tatizo la kupora marehemu mali liko kila mkoa labda uwe umeandika wosia
 
Ungejtajidi kidogo uwe mchaga but umekata tamaa mapema . Tafuta mwingine ila kabila rahisi sana ni kuwa Mang'ati 😂😂😂
 
Kaka yangu m1 hivi anamiliki kiwanda flani hapa TZ, mkewe ni meneja mkuu ktk hicho kiwanda, basi huweziamini kajaza Wachaga tupu kwenye hicho kiwanda hadi wasio na CV na wakienda ndugu wa kaka yangu hata wakiwa na CV zote kuajiriwa ni kukataliwa mbele kwa mbele tu mpaka wakati mwingine ndugu hutamani hicho kiwanda kife.
Kaka yako dhaifu
 
mpaka wewe unatukandia mkuu....tupunzisheni kidogo basi......

mapenzi kutokujua ni sisi
wizi sisi
umalaya sisi
wazulamti sisi
wabinafsi sisi
wahongaji sisi
wachawi sisi


sifa mbaya kwanini zote ziende kwa wachaga tu....
Sisi ni wana wa israel tulishafika kanani mda wakati wao bado wanaoga maji ya tope
 
Haya mapalestina ni bora muyaachage yaoane yenyewe kwa yenyewe tu...tena afadhali yako maana mwanaume ndo alikua mchaga ndo maana ukapata hata hiko kinafasi cha kutambulishwa ukweni
Mahusiano ambayo mwanamke ndo mchaga na mwanaume ni kabila jingine ndo yanakuwaga magumu balaa!!
Ni nadra sana mwanaume asiye mchaga (CHASAKA) kukubaliwa kuoa uchagani maana wanahofiaga kumpoteza member wa ukoo wao.
Kiufupi wachaga ni wabaguzi sana na wana ukabila kiwango cha SGR
Oa kwenu aisee...hii ndio taabu ya kushobokea jamii considered ni advanced kumbe sio kama unavyodhani..

Jamii yako ina mabinti wazuri,wape umuhimu,waoe...

I really dont respect a man who despise women of his own people who gave him life....

Kukimbilia wasichana anao consider wametoka jamii aliyotamani kua humo...

Weak societies make it a mission to marry women of superior societies,infact they hate their own societies and people,which to me I cant forgive this kind of lunacy!

Oa kwenu,u will be more respected by your own people!Stop this self hate!
 
”Nimehuzunika tu kwa kuwa tumefika mwisho kwa sababu mimi si MCHAGA. Ubaguzi ambao Wachaga wengi wanao."

Kwanza nikutakie pole sana!

Pili, nikupe hongera kwa kudumu penzini na Chagaboy kwa miaka mitano.

Tatu, ninashangaa sana uliwezaje kudumu penzini miaka mitano na mtu ambaye unadai kuwa kwao ni wabaguzi.

Hivi, ulikuwa kipofu kiasi gani?

Mimi maoni yangu ni kwamba, wewe ndiye mwenye makosa kwa sababu ulikubali kutambulishwa kienyeji na huko Uchaggani wakakusoma kienyeji, wakakuchoka kienyeji kwa tabia zako za kienyeji maana ulijirahisisha kienyeji, tena inawezekana hata ulienda kujifulisha na kujipikisha kienyeji wakati hutambuliki rasmi huko.

Halafu, kwa kuwa ulikaa nao miaka mitano+ ni kwanini ulichukua muda kuvumilia Kama kweli ulibaguliwa?

Then, Kama ulisikia na au ulipata taarifa kwamba Wachaga hawapendi makabila mengine ni kwanini ung'ang'anie penzi la Kichagga?

Mimi niwape tu ujumbe humu na wewe mleta mada. Siyo kweli kwamba Wachaga hawaoi makabila mengine, ila ndugu zangu Watanzania, Wachaga tuna tamaduni tofauti kidogo na jamii nyingine, kwa hiyo, kuoana sisi kwa sisi huwa inashauriwa kwa sababu ndoa nyingi na makabila mengine hazidumu kwa sababu za kitamaduni!

Poleni nyote mnaosumbuka na mahusiano typical ya aina hii; kinachowasumbua siyo ukabila wa Wachaga ila ni tamaduni zenu ambazo haziivi na Wachaga na siyo vinginevyo.

Sijasema Kama una mahusiano na Mchagga muacheni, isipokuwa kama haupo tayari kufuata mila na desturi za Kichagga, kaa pembeni na upishe kwa amani maana hamtafika popote.

Pongezi kwenu mlionielewa!

Wachaga tuna asili ya Kiyahudi. Msamo wa Kichagga hauyumbi kienyeji!
Meku umemalizaa yote,kunywa kitoshi bili nakuja kulipa
 
Hata huyo atamwacha kisa ni mchaga wa machame.

Baadae atamwacha mchaga wa Rombo kwa sababu ni Ukoo wa Shirima.

Guys hatima ya maisha yako ya baadae kwa maana ya mahusiano unayo wewe, sio ndugu, rafiki wala wazazi. Kuta nne ndizo zitakuwa shahidi wa maisha yenu. Wake up guys!!
Na kweli;baadhi ya wachaga ni vihiyo.,ubaguzi wao kwa wao.,
Mkibosho atamuacha mwenzie kisa tu ni Mmarangu
MRombo hataki kusikia Mmachame/mpalestina!
 
Tangu nimezaliwa na kukulia uchagan sijawahi kuona tambiko la Aina yeyote kwa upande wangu. Kwa wengine sijui ila Mimi sijawahi
Nmeishi, Uru, machame, Marangu, rombo, tarakea, mashati, mwika, na kibosho muda mrefu sana ,,so I am speaking from experience and I sincerely have no any reason to throw a shade on wachaga for nothing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmeishi, Uru, machame, Marangu, rombo, tarakea, mashati, mwika, na kibosho muda mrefu sana ,,so I am speaking from experience and I sincerely have no any reason to throw a shade on wachaga for nothing

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikatai but Mimi na uchaga wangu sijawahi kuona hiyo kitu, may be cause niliishi modern family ya baba Dr
 
Sikatai but Mimi na uchaga wangu sijawahi kuona hiyo kitu, may be cause niliishi modern family ya baba Dr
Yap,,Kuna wachache waliostaarabika kutokana na Elimu na ushika Dini hasa waishio mijini kwenye modern family as you said. Lakini hayo maeneo ya vijijini niliyokutajia Bado wanahusudu matambiko mpaka leo. Na huko ndio uchagani kwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom