Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Ami yake ndo nani?
 
Inasemekana wafuasi wa Mtume (saw) hawajawahi kuazimisha siku ya kuzaliwa kwake, Pia Maimam wakubwa kama Imam Malik, Imam Shafii nk hawajawi kusema na kuazimisha suala hilo, zaidi katika Quran hakuna ilipoandikwa hata wake zake hawajawahi kufanya. Je sisi jambo hili tumelitowa wapi?
 
Ahsante sana kwa majibu yako mazuri. Hakika umeiva kwenye majadiliano na midahalo.Huna hasira hata kama unapata kejeli na dharau.Pia unaonekana una elimu na maarifa makubwa.Ubarikiwe sana!!!
 
Haya ni mastory ya uongo uongo tu. Hamnaga kiumbe kama hicho. Ni sawa na kudanganywa kuwa ukienda mbinguni utapewa wanawake wa kufanya nao mapenzi 70. Kamba tu hizo za kusaidia kuweka watu kwenye line
 
makatuni gani?
Haya ndiyo matatizo ya kukimbia maswali,uwe una jibu maswali unayoulizwa,hii itakufanya uwe makini zaidi. Nilipokuuliza kwamba habari hizo umezipata wapi na sifa zile uzitaje ulidhani nacheza au naleta mzaha au napoteza muda kama unavyo poteza muda wewe ?
 
Swali..je ni kweli kuwa Muhammad na ukoo(uzao) wake wa Qusay, wa kabila la Quraysh- Hashimu ndo walikuwa wanawajibika ( responsible) katika kuitunza kabbah ( The cube), wakijipatia fedha kutoka kwa wanaoenda kutambika, kabbah ambayo kipindi hicho kabla ya Muhammad kuleta uislamu mwaka 610, kabbah ilikuwa inatumika kwaajili ya matambiko ya miungu wa kiarabu wa Al- Lat na Al- uzzah? Na Muhammad alishiriki kikamilifu kwenye mambo ya matambiko akishirikiana na baba yake mkubwa Abu Taibu?
 
Nashukuru sana, na MUNGU azidi kukupa nguvu ya kujitahidi katika utafiti wako, Tafuta kitabu cha Sulaym ibn Qays (694-714). Kazi hiyo ni mkusanyiko wa hadithi za mapema za uislamu, Karne ya 7, na mara nyingi hutambuliwa kama mkusanyiko wa mapema zaidi zilizoandikwa kwa mikono yake.
 
Ahsante,
Kaaba ilikuwa patakatifu katika nyakati za kabla ya Uisilamu. Kaaba ya kabla ya Uisilamu iliwekewa Jiwe Nyeusi na sanamu za miungu ya kipagani. Muhammad aliamrishwa na MUNGU kusafisha Kaaba kwa kuondoa masanamu wakati wa ushindi wake kurudi Makka, akirudisha hadhi ya alkaaba kwa imani ya mungu mmoja wa Ibrahim.

Juu ya Ushindi wa Makka mnamo Januari 630, Muhammad aligundua kuwa Kaaba ilikuwa imefungwa. Akasema, Ni nani aliye na ufunguo? "na aliambiwa kwamba Uthman Ibn Talha alikuwa nayo. Muhammad alimwambia Ali achukue ufunguo kutoka kwa Uthman. Lakini hawakuwa na wajibu wa kuitunza kwa kujipatia fedha, si kweli
 
Una uhakika gani kusema" hakika wanawake wa peponi wapo" wakati hujawahi kufika peponi zaidi ya kusoma tu kwenye mavitabu yaliyoandikwa na watu wa hapahapa duniani, ambao hata wao wenyewe hawajawahi kufika huko peponi
 
Ok, sijawahi kisikia hiki, ngoja nimtafute
 
Ami yake ndo nani?
Baba yake na mtume anaitwa Abdallah ibn Abd al-Muttalib., Huyu Abdallah mkubwa wake anaitwa Abu Talib ibn Abd al-Muttalib. Kwa hivyo Abdallah alimzaa Muhammad, na Abu Talib alimzaa Ally. Kwa hivyo Abu Talib ni ami yake na Muhammad, yaani ni Baba yake mkubwa.
 
Soma vizuri kabbah ilikuwa ipo chini ya nani miaka yote tangu Muhammad alikuwa mdogo anaishi na babu yake Abu Mutalib, na hata Kabbah ilivyovunjika kuta zake kwaajili ya mafuriko mwaka 605 ikajengwa tena, chunguza kama Muhammad hakushiriki kujenga hizo kuta nne. Halaf mi nimeuliza kabla hajawa mtume, wewe unaniletea story za baada. Tangu enzi za mababu,wa mababu zake, kuanzia Qusay mwenyewe..kazi yao kubwa ilikuwa kutunza kabbah na kuuzia watu wanaokuja kutambika kwenye hilo Jiwe chakula na mahitaji mengine, kazi ambayo hata Muhammad ameifanya sana. Maana hiyo ndo ilikuwa chanzo cha mapato enzi na enzi za familia yote ya Qusay
 
Sio kweli kwamba Abu Talib alikuwa baba yake mdogo na Muhammad..bali alikuwa ni baba yake mkubwa. Maana baba yake na Muhammad ( Abdullah) ndo alikuwa mtoto mdogo wa Mzee Abd- Al Muttalib. Kuwa makini master
 
Nimejaribu kupitia kumjua huyu ndugu kwa haraka haraka nimeona ni very interesting. However, nikajaribu kuangalia taarifa zake tunazijuaje? Nikakutana na hii statement Wikipedia.

"Much of the information about Sulaym comes from Shia Muslim tradition.[8] According to modern historian Mokhtar Djebeli, "the very existence of this man, and his work, should be regarded with caution, since apart from Ibn al-Nadim ... only a few Shi'is mention him, and then only in a very terse and laconic fashion".[8] "

Nimeangalia Ibn al Nadim qliishi karne ya 10. Miaka 300 na baada ya Uislam na Muhammad. Kaa hiyo vado sio chanzo cha kuaminika kihistoria. Ni kama tu ambavyo Ibn Ishaq anasemekana kuandika Sira ila hatuna taarifa zake ispokuwa kile alichosema Ibn Hisham. Na Ibn Hisham ni mwandishi aliyekuja baadaye sana.

Kama una kitabu kingine au una hoja kinyume na hiyo hapo, kwamba maandiko ya huyu ndugu ni sahih na yaliandikwa karne ya saba, nakusikiliza

Link ya WP hii hapa: Sulaym ibn Qays - Wikipedia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…