jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Huyo maandiko yako wazi..na Mungu alimuahidi ibrahimu hivyo.Mama Sara mke wa Ibrahimu alizaa na Age ya 90+
#MaendeleoHayanaChama
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo maandiko yako wazi..na Mungu alimuahidi ibrahimu hivyo.Mama Sara mke wa Ibrahimu alizaa na Age ya 90+
Ami yake ndo nani?Yeye (Muhammad Ibn Abdullah) alizaliwa katika nyumba ya ami yake, Abu Talib, katika “mtaa wa Bani Hashim” huko Makka, tarehe 12 Rabil-awal ya ule Mwaka wa Tembo, tarehe ambayo inaoana na tarehe 8 Juni 570.
Mama yake na mtume Muhammad (s.a.w), Bi Amina, alituma habari za uzazi huu wa kheri kwa babu yake na Muhammad, Mzee Abdul Muttalib, ambaye alikuja, akamchukuwa mikononi mwake, na akampa jina hili la Muhammad.” Lenye maana ya MSIFIWA.
Nawakaribisha kuuliza maswali kuhusu mtume wetu huyu MUHAMMAD "amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake".
View attachment 1975182
Ahsante sana kwa majibu yako mazuri. Hakika umeiva kwenye majadiliano na midahalo.Huna hasira hata kama unapata kejeli na dharau.Pia unaonekana una elimu na maarifa makubwa.Ubarikiwe sana!!!Ahsante ndugu.
------1
Wasunni wanaamini kwamba Mtume hakuwa ameteua mrithi na badala yake alikuwa amekusudia jamii ya Waislamu kuchagua kiongozi kati yao. Wanakubali utawala wa Abu Bakr, ambaye alichaguliwa huko eneo la Bani Saqifah, na ule wa warithi wake, ambao wote wanajulikana kama Makhalifa wa Rashidun.
Swala la Mrithi wa Muhammad ni jambo kuu ambalo liligawanya jamii ya Waislamu katika mafungu kadhaa katika karne ya kwanza ya historia ya Kiisilamu, na kutokea madhehebu ya Shia na Sunni. Uislamu wa Shia unashikilia kwamba Ali ibn Abi Talib ndiye mrithi aliyeteuliwa wa nabii wa Kiislamu baada ya Muhammad kama mkuu wa jamii. Uislamu wa Kisuni unashikilia Abu Bakr kuwa kiongozi wa kwanza baada ya Muhammad kwa msingi wa uchaguzi.
Kwa upande mwingine, Shia wanaamini kwamba Ali alikuwa ameteuliwa na Mtume kuwa mrithi baada yake, haswa wakati wa hafla ya Ghadir Khumm. Kwa maoni ya Shia, warithi halali wa Muhammad ni Ali na Maimamu kumi na wawili wa ukoo wake, ambao wanaonekana kama walioteuliwa na Mungu. Na wa mwisho katika hao Maimamu 12, anaitwa Mahdi, ambaye ujio wake unangojewa na kukubalika na Shia na Sunni kwa pamoja.
Kwa hivyo, mtume alichagua uwongozi baada yake na alimchagua Ali ibn Abi Talib kwenye hadhara ya maelfu ya maswahaba kulingana na ushahidi mbalimbali, lakini baada ya kufa Mtume, waliokuwepo hawakufuata hayo maagizo. Nadhani ni mtihani ambao MUNGU aliwapima ili kutimiza kauli ya Mtume s.a.w aliyosema kwamba umati wangu utagawanyika makundi 73.
--------2
Mtume siyo chanzo cha madhehebu japokuwa mwenyewe aliacha ametabiri kwamba umati wake utagawanyika makundi 73
------3,4
Hakika baada ya kufa mtume watu walisambaratika sana, na waisilamu waliuwana wenyewe kwa wenyewe kwa kugombania maslahi ya uwongozi, na pia baadhi ya watu waliingiza mila zao katika dini. Huu wote ni mtihani bado ili kupima imani zao, nasisi kutupa juhudi ya kuupambania ukweli.
-----5
Misingi ilikuwa imara lakini watu walikengeuka, kumbuka mtume alipigana vita mbili, moja ni kupigana na wasio waisilamu lakini pili ni kupigana na wanafiqi ambao walijivika vazi la uwislamu. Wanafiqi ni maadui ambao unakuwa nao pamoja bila ya wewe kuwafahamu. Hii yote ni mitihani. Lau kama kila kitu kingelikuwa sawa kusingekuwa na juhudi za watu kupembua mambo, ndio maana MUNGU aliacha hili litokee.
Haya ni mastory ya uongo uongo tu. Hamnaga kiumbe kama hicho. Ni sawa na kudanganywa kuwa ukienda mbinguni utapewa wanawake wa kufanya nao mapenzi 70. Kamba tu hizo za kusaidia kuweka watu kwenye lineAhsante. Buraq maana yake ni "mwendo mkali mfano wa umeme" au kwa ujumla "ni kama mwanga wa radi") ni kiumbe katika mila ya Kiisilamu ambaye alitumika kama usafiri kwa manabii fulani. Buraq alimbeba nabii wa Kiislam Muhammad kutoka Makka kwenda Yerusalemu na kwenda juu mbinguni na kurudi usiku huo huo. Kwasababu alikuwa akikimbia sana, anatua pale macho yake yanapoishia kutazama, alikuwa kikimbia mfano wa speed ya mwanga.
Pia Ibrahimu alipomtembelea Hajiri na Ishmaeli. Ibrahimu aliishi na Sara huko Kanaani lakini usafiri wake ilikuwa ni Buraq walimsafirisha asubuhi kwenda Makka kuiona familia yake huko na kumrudisha jioni.
Ingawa Hadithi haionyeshi Buraq wazi kuwa na sura ya kibinadamu, bali hiyo ni sanaa ya Kiislamu ya Uhindi na Uajemi. Hii inaweza kuwa ilitokana na tafsiri ya kiumbe kuelezewa kuwa na "uso mzuri" kama uso wa kibinadamu badala ya mnyama.
Haya ndiyo matatizo ya kukimbia maswali,uwe una jibu maswali unayoulizwa,hii itakufanya uwe makini zaidi. Nilipokuuliza kwamba habari hizo umezipata wapi na sifa zile uzitaje ulidhani nacheza au naleta mzaha au napoteza muda kama unavyo poteza muda wewe ?makatuni gani?
Sijui kwanini unakimbia maswali ninayo kuuliza ?as log as unapinga haibadili maana kua kwa namna moja au nyingine unavikubali
Nashukuru sana, na MUNGU azidi kukupa nguvu ya kujitahidi katika utafiti wako, Tafuta kitabu cha Sulaym ibn Qays (694-714). Kazi hiyo ni mkusanyiko wa hadithi za mapema za uislamu, Karne ya 7, na mara nyingi hutambuliwa kama mkusanyiko wa mapema zaidi zilizoandikwa kwa mikono yake.Ninachomaanisha ni hiki nikichoandika ndugu yangu. Sina maana nyingine. Ninatafuta vyanzo vya kihistoria kuhusu uislam vinavyotoka karne ya 7. Ni kawaida tu mtu anapotaka kujua historia ya kitu huenda kuangalia ndani ya karne mambo yalitendeka.
Hii ya Quran kundaliwa na Khalif Uthman, ni inatoka kwenye hadith (sina hakika kama kwenye sira imeandikwa pia). Ila nimejaribu kuangalia waandishi wa hadith kama Muslim, al Bukhari, n.k. wanaandika miaka mingi sana baadaye.
Kwa hiyo kwa mtu anayetafiti, hii inakuwa haimfai, kwa sababu kihistoria hawa hawakuwahi kushuhudia walichokiandika na wala hawakuandika kipindi wale mashuhuda wakiwa hai, ili kama wamepunguza ama kuongeza wawakosoe.
Natumaini swali langu nimeliweka kwa uwazi zaidi, na naomba nilirudie: Unaweza nisaidia vyanzo vya historia na matukio ya Uislam, vya karne ya 7 au vilivyoqndikwa na shuhuda?
Ahsante
Huyu aliyeandika hicho ulichokisoma siye mtoa mada,huyu ni huyo ni kati ya wale wanaokejeri tu.baada ya jibu hili nimesitisha nilichotaka kuuliza, nimepata ukakasi na ujuzi na uadilifu wa mtoa mada.....kuna kitu kinaniambia tofauti, the guy is here just to make fun of islam!!!
Kwa uwelewa wako Muhammad (s.a.w) na Abraham walikuepo kwa wakati mmoja?waarabu weusi husema alianzisha Abraham
Na Mohamed aliendeleza
Kitu ambacho
What a joke!
Ahsante,Swali..je ni kweli kuwa Muhammad na ukoo(uzao) wake wa Qusay, wa kabila la Hashimu ndo walikuwa wanawajibika ( responsible) katika kuitunza kabbah ( The cube), wakijipatia fedha kutoka kwa wanaoenda kutambika, kabbah bambayo kipindi hicho kabla ya Muhammad kuleta uislamu mwaka 610, kabbah ilikuwa inatumika kwaajili ya matambiko ya miungu wa kiarabu wa Al- Lat na Al- uzzah?
Una uhakika gani kusema" hakika wanawake wa peponi wapo" wakati hujawahi kufika peponi zaidi ya kusoma tu kwenye mavitabu yaliyoandikwa na watu wa hapahapa duniani, ambao hata wao wenyewe hawajawahi kufika huko peponiKhur-lain
Katika imani ya dini ya Kiisilamu, hawa ni wanawake ambao watafuatana na waumini waaminifu wa Kiislam katika Pepo. Wasomi wa Kiislamu wanatofautiana kuhusu ikiwa wanarejelea wanawake waumini wa ulimwengu huu au uumbaji wao ni tofauti, lakini kwa hakika wanawake wa peponi wapo.
Ok, sijawahi kisikia hiki, ngoja nimtafuteNashukuru sana, na MUNGU azidi kukupa nguvu ya kujitahidi katika utafiti wako, Tafuta kitabu cha Sulaym ibn Qays (694-714). Kazi hiyo ni mkusanyiko wa hadithi za mapema za uislamu, Karne ya 7, na mara nyingi hutambuliwa kama mkusanyiko wa mapema zaidi zilizoandikwa kwa mikono yake.
Lete ushahidi aliua nani na wapi?huyu mwamba aliua watu wengi sana kwa interests zake.
damu ya hao watu allah ameiweka kundi gani?
Baba yake na mtume anaitwa Abdallah ibn Abd al-Muttalib., Huyu Abdallah mkubwa wake anaitwa Abu Talib ibn Abd al-Muttalib. Kwa hivyo Abdallah alimzaa Muhammad, na Abu Talib alimzaa Ally. Kwa hivyo Abu Talib ni ami yake na Muhammad, yaani ni Baba yake mkubwa.Ami yake ndo nani?
ndio swali Gani Hilo ArifKwa uwelewa wako Muhammad (s.a.w) na Abraham walikuepo kwa wakati mmoja?
Soma vizuri kabbah ilikuwa ipo chini ya nani miaka yote tangu Muhammad alikuwa mdogo anaishi na babu yake Abu Mutalib, na hata Kabbah ilivyovunjika kuta zake kwaajili ya mafuriko mwaka 605 ikajengwa tena, chunguza kama Muhammad hakushiriki kujenga hizo kuta nne. Halaf mi nimeuliza kabla hajawa mtume, wewe unaniletea story za baada. Tangu enzi za mababu,wa mababu zake, kuanzia Qusay mwenyewe..kazi yao kubwa ilikuwa kutunza kabbah na kuuzia watu wanaokuja kutambika kwenye hilo Jiwe chakula na mahitaji mengine, kazi ambayo hata Muhammad ameifanya sana. Maana hiyo ndo ilikuwa chanzo cha mapato enzi na enzi za familia yote ya QusayAhsante,
Kaaba ilikuwa patakatifu katika nyakati za kabla ya Uisilamu. Kaaba ya kabla ya Uisilamu iliwekewa Jiwe Nyeusi na sanamu za miungu ya kipagani. Muhammad aliamrishwa na MUNGU kusafisha Kaaba kwa kuondoa masanamu wakati wa ushindi wake kurudi Makka, akirudisha hadhi ya alkaaba kwa imani ya mungu mmoja wa Ibrahim.
Juu ya Ushindi wa Makka mnamo Januari 630, Muhammad aligundua kuwa Kaaba ilikuwa imefungwa. Akasema, Ni nani aliye na ufunguo? "na aliambiwa kwamba Uthman Ibn Talha alikuwa nayo. Muhammad alimwambia Ali achukue ufunguo kutoka kwa Uthman. Lakini hawakuwa na wajibu wa kuitunza kwa kujipatia fedha, si kweli
Sio kweli kwamba Abu Talib alikuwa baba yake mdogo na Muhammad..bali alikuwa ni baba yake mkubwa. Maana baba yake na Muhammad ( Abdullah) ndo alikuwa mtoto mdogo wa Mzee Abd- Al Muttalib. Kuwa makini masterBaba yake na mtume anaitwa Abdallah ibn Abd al-Muttalib., Huyu Abdallah mdogo wake anaitwa Abu Talib ibn Abd al-Muttalib. Kwa hivyo Abdallah alimzaa Muhammad, na Abu Talib alimzaa Ally. Kwa hivyo Abu Talib ni ami yake na Muhammad, yaani ni Baba yake mdogo.
Nimejaribu kupitia kumjua huyu ndugu kwa haraka haraka nimeona ni very interesting. However, nikajaribu kuangalia taarifa zake tunazijuaje? Nikakutana na hii statement Wikipedia.Nashukuru sana, na MUNGU azidi kukupa nguvu ya kujitahidi katika utafiti wako, Tafuta kitabu cha Sulaym ibn Qays (694-714). Kazi hiyo ni mkusanyiko wa hadithi za mapema za uislamu, Karne ya 7, na mara nyingi hutambuliwa kama mkusanyiko wa mapema zaidi zilizoandikwa kwa mikono yake.