Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Kuna sheghe mmoja mpenda ubwabwa mwenye elim ya uhakika ya kidini Tena anawakilisha Jimbo Fulani nchini kwa masuala ya dini. Sheghe huyu aliwahi kuzema mtu Fulani aliye kuzimu kwa Sasa ni mkubwa au zaidi ya mtume Mohammad.
Swali langu ni. Je mwanazuoni huyo Yuko sahihi? (Sikuona mtu yoyote aliyemkemea kwa maneno Yale)
 
Hiyo tarehe uliyo itaja ni tarehe aliyo fariki sio tarehe aliyo zaliwa.

Prophet Muhammad ,Peace Be Upon Him was born on 29 August 570
 
Ad-uuka ahmad ya Muhammad,
Yaa Sayyidarrussuli al muqadam

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Ish-faa ilaallahi ya Muhammad,
Yawmal qiyamat kay una-aam

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Arjuu sh-shafaat min Muhammad,
Law kuntu artakibu al muharram

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Man jaa wamal jaana Muhammad,
Yawmal hawaani bihi tahash-sham

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Wannuru jaa-abihi Muhammad,
Wal haqqu buyyina in takallam

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Aala ssamaai samaa Muhammad,
Jibriilu qaala lahu taqaddam

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Wal jun-du hiina ghazaa Muhammad,
Minhum Mmalaaikatun tasawwam

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)

Waddinu adh-harahuu Muhammad,
Walkufru abtwalahu fahaddam

(Allahumma swallii aala Muhammad Yaa rabbi swalli alayhi wasallim)
 
Ila waafrika hapa tulikamatwa Sana akili.
 
Kwanini alimbaka Aisha wakati yeye akiwa na miaka 54 na mtoto Aisha akiwa na miaka 9 tu? Mungu anaruhusu ubakaji kwa watoto kweli?
 
siku ya kuzaliwa yesu sio realistic maana haijaandikwa popote ni kundi flani liliamua kuitenga tar 25/12 ,wangeweza kuitenga siku yoyote ile ila ya muhamad ni real
Yale yale tu, hivi vitabu vimetungwa na watu na si Mungu. Constantin The 1st akishirikiana na wafalme 12 wa nchi za Ulaya ndiyo waliotunga Ukristu na sheria zake. Hawakuwa na siku maalum ya sherehe ya dini yao, wakakopi siku kuu nyingi za kipagani na za Misri (Kiafrika). Waafrika tumechezewa sana akili na hizi dini za kuletewa na ndiyo maana siku za nyuma tukiwa wadogo sie tuliyetaka kujuwa ukweli tulikatazwa kuuliza maswali na kuambiwa kila kilichoandikwa kwenye Quran na Biblia ni neno sahihi la Mungu, kuuliza maswali ni dhambi. What kind of crap is this, Mohammad na mitume wengi walikuwa wauwaji...Mungu anaruhusu haya kweli?
 
Yale yale tu, hivi vitabu vimetungwa na watu na si Mungu. Constantin The 1st akishirikiana na wafalme 12 wa nchi za Ulaya ndiyo waliotunga Ukristu na sheria zake.
Doh! Kwamba Wakristo waliokuwa wanateswa na Neeo, Domitian et al mamia ya miaka kabla ya Constantine walikuwa wanatumia sheria zipi? Au Constantine alitunga akafa na kuja kufufuka mamia ya miaka baadaye?

Hawakuwa na siku maalum ya sherehe ya dini yao, wakakopi siku kuu nyingi za kipagani na za Misri (Kiafrika).
Biblically hizo siku hazipo. Kikristo siku zote ni za Bwana na unaruhusiwa kusheherekea. Yesu hakuzaliwa tar 25/12. Hilo liko wazi. Lakini Mkristo hafingwi kusheherekea kuzaliwa, maisha. Kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu muda wowote. Ndio maana kuwa wengine wana tarehe tofauti na 25/12 na pasaka vivyo hivyo.

Waafrika tumechezewa sana akili
Ukiwa mjinga hata wa vitu vidogo hivi lazima uchezewe sana. Sasa kama unaandika kwa confidence kabisa Ukristo ulianza na Constantine karne ya tatu wakati historia iko wazi ulianza karne ya kwanza, kwa nini usichezewe?

na hizi dini za kuletewa
Kama vtu vya kuletewa ni vibaya tupa basi na hiyo simu, tupa nguo kavae magome ya miti. Ujinga wa kuacha kupima kitu on merit na kuanza kulialia vya kuletewa na unaandika kwa kutumia simu ya kuletewa kwenye software ya forum ya kuletewa, ni ujinga mkubwa!

na ndiyo maana siku za nyuma tukiwa wadogo sie tuliyetaka kujuwa ukweli tulikatazwa kuuliza maswali na kuambiwa kila kilichoandikwa kwenye Quran na Biblia ni neno sahihi la Mungu, kuuliza maswali ni dhambi.
Sasa unaulaumu Ukristo kwa ujinga wa uliowauliza? Kwa akili hizi lazima uchezewe sana. Biblia inakualika kuhoji


“Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.” Isa‬ ‭41:21‬ ‭

“Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.”
‭‭1 Pet‬ ‭3:15‬ ‭

Kwa hiyo kama Biblia inakualika kuhoji na inafundisha tuwe tayari kuwajibu watu wenye maswali wewe unacholaumu ni kipi? Naamini ni ule ule ukinga wa kukosoa usichokijua. Yaani unakosoa kwa kutumia ufahamu wa kusikia ma sio wa kujifunza wewe mwenyewe.

What kind of crap is this, Mohammad na mitume wengi walikuwa wauwaji...Mungu anaruhusu haya kweli?
Hilo la Muhammad nitawaachia Waislam wakujibu. Ila hakuna mtume wa Kikristo hata mmoja aliua kwa sababu ya dini. In fact mitume wote 11 ukiacha Yohana pekee waliuawa wakihubiri injili. Kwa hiyo kama ulikuwa unahisianisha hii comment na Ukristo, hakuna kitu kama hicho huku!

Nikushauri tu ujifunze Ukristo na kuuelewa nadala ya ule wa kukaririshwa na kukariri. Ili hata ukiamua kuukosoa angalau makosoo yawe ni yenye mantiki
 
Waweza kuwa uko sahihi lakini ukweli kuwa huo ukristo umeletewa kama ulivyoletewa simu. Sasa kujifanya unaujua kuliko waliokuletea si sawa na jua siyo asili yako
 
Ila waafrika hapa tulikamatwa Sana akili.
Bado huelewi?

Kwa Mungu hakuna mtu mweusi wala mzungu au mwarabu wala mtu wa manjano. Mungu anatutambua sote kama waja wake kama viumbe vyake. Kwa sababu huo uweusi kauumba yeye, uweupe kauumba yeye. Kwake ni viumbe vyake alivyoviumba kwa muonekano wa rangi tofauti kama alivyoumba samaki kwa rangi tofauti. Haya matabaka tunajiwekea sisi.

Mungu akimteua mtu miongoni mwa waja wake binadamu kuwa huyu ndiye atakayekuwa mjumbe wangu kwenu ninyi tafsiri yake ina maanisha ni kwa waja wake. Tafsiri yake haimaanishi ni kwa mtu mweupe au mweusi.

Kutokana na changamoto alizozipitia na anazozipitia mwafrika chochote kitokacho nje ya jamii yake hususani likiwa suala la imani ya Mungu, moyo wake bado unajihisi ni mtumwa na akili yake inakataa kutojifungamana na macho yanabakia kwa anachokiangalia akili inakifafanua kwa misingi ya rangi ya ngozi, na haya ni makosa Kama makosa mengineyo.

Laiti kama mwafrika angelikuwa ni mtawala wa dunia kama walivyo wazungu hii fikra ya kusema hii hapa tulikamatwa akili asingelikuwa nayo. Kwani angejitukuza kwa kusema nimestaarabika na namjua Mungu.

Toka kwenye hiyo taswira ya ubaguzi wa rangi na uufurahie upendo ama mapenzi ya Mungu.
 
Duuh aisee
 
Eti ni kweli alipaa angani na mnyama aitwaye "buraq" ambaye anamuonekano wa farasi jamii ya punda ila yeye ana kichwa cha mwanamke?

Tukio hilo liliwahi kutokea kweli au ni masimulizi tu kunogesha stori?
Hakuna anaejuw buraq anafananaje hixo nyingine ni story
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…