Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Hiyo ya ibrahiimvkutumia mnyama buraq itakuwa ni hadith za kiisrailiyat
 
Je Baba wa Mtume Mohammed Alikua dini Gani?
Baba wa mtume alikuwa akiitwa Abdullah ibn Abd al-Muttalib Alikuwa mtoto wa Abdul-Muttalib ibn Hashim na Fatimah binti Amr wa ukoo wa Makhzum. Hawa walikuwa wakifuata mila za Nabii Ibrahim, bila shaka walikuwa waisilamu
 
Baba wa mtume alikuwa akiitwa Abdullah ibn Abd al-Muttalib Alikuwa mtoto wa Abdul-Muttalib ibn Hashim na Fatimah binti Amr wa ukoo wa Makhzum. Hawa walikuwa wakifuata mila za Nabii Ibrahim, bila shaka walikuwa waisilamu
Tumepigwaaaaaa
Nasemaje tumepigwaaaaaaaa!
Sheikh wangu hapa umenipiga kamba kubali ukatae!
 
Je ni halali kuisherekea hio siku ya kuzaliwa kwa mtume? Na je Quran inaonesha kuwa ata enzi za mtume watu waliihadhimisha siku yake ya kuzaliwa?
Ahsante ndugu, Uhalali wa Mawlid "umekuwa mada ya mjadala mkali" na imeelezewa kama "labda moja ya majadiliano mabaya zaidi katika sheria ya Kiislamu". Wasunni wengi na karibu wasomi wote wa Shia wameidhinisha maadhimisho ya Mawlid, wakati wasomi wa Salafi, Mawahabi na Ahmadiyya wanapinga sherehe hiyo. Hapo zamani, Saudi Arabia kwa sasa inakataza maadhimisho ya Mawlid. Lakini ni ajenda maalum iliyotengenezwa na wamagharibi ili kuupunguza nguvu uwislamu, kwani mawlid hutumika kuutangaza uwislamu.

Kusoma Mawlid halali- maadamu ina mkutano na watu, kisomo cha Qu'an, kusimuliwa kwa ( wasifu wa) Nabii MUHAMMAD) - Mungu ambariki na ampe amani - na maajabu yaliyotokea wakati wa kuzaliwa kwake, ambayo yote hufuatiwa na karamu ambayo huhudumiwa kwao na wanayokula-ni ubunifu mzuri ( bid'a hasana), ambayo mtu hupewa thawabu kwa sababu ya heshima iliyoonyeshwa kwa nafasi ya Mtume - Mungu ambariki na ampe amani.
-----
Mtume alifanyiwa mawlid mbele yake kwa kusifiwa.
 
[emoji1756][emoji1756] hili la mwisho mbona kama mnabumbabumba?
 
Mgawanyiko wa mwezi ni muujiza wa kweli katika mila ya Waislamu inayohusishwa na nabii wa wetu Muhammad. Kisa hicho kimeelezwa kwenye Qur'an 54: 1-2, Maswahaba pia walisema ''Tulikuwa pamoja na Mjumbe wa Mungu huko mlima wa Mina, mwezi huo uligawanyika mara mbili. Sehemu moja yake ilikuwa nyuma ya mlima na ile nyingine ilikuwa upande huu wa mlima.''
 
Dhul qarnaine alijenga ukuta kuzuia viombe viasi juuj wa maajuj, huo ukuta upo wapi kwa sasa. Quran 18.83-104
Bwana Dhulqarnain alikuwa akiitwa Ayash, alikuwa ndiye Mfalme wa kwanza baada ya Mtume Nuh a.s., wengi wa watu wanadhani kuwa yeye ndiye Alexandria wa Kirumi lakini haya si kweli, vile vile Bwana Dhulqarnain yeye hakuwa mtume bali alikuwa mja mwema wa Allah swt .

Ni kweli Zu al-Qarnayn, anaonekana katika Quran, Surah Al-Kahf (18), Ayahs 83-101 kama mtu anayesafiri kuelekea mashariki na magharibi na kuweka ukuta kati ya watu fulani kuwazuwia '' Ya'juj na Ma'juj''. Mwisho wa ulimwengu utaonyeshwa na kuachiliwa kwa '' Ya'juj na Ma'juj' kutoka nyuma ya ukuta hu, kisha wataangamizwa na Mungu kwa usiku mmoja. Ukuta huo hakika mimi sifahamu ulipo Wengine wanasema unapatikana huko miji ya Siberia. Wengine wanasema milima ya Himalaya inaweza kuwa eneo sahihi la ukuta wa Yajuj na Majuj. Wengine wanasema kwamba wanaishi katika maeneo ya kaskazini mwa Azabajani, Armenia, na Georgia.
 
Unataka kumaanisha nini ndugu? kuna hoja yoyote unataka kuiweka ? Qur'an Iliandaliwa chini ya swahaba aitwae Uthman miaka ishirini baada ya kifo cha Mtume Muhammad s.a.w.
 
Kijografia na kiteolojia kwann kunautofauti?
Namaanisha mitume yoote (mayahudi) iliyotangulia mafundisho yao hawakutofautiana, kwann yeye amekuja tofauti pamoja na kukubali au kuyabeba baadhi ya mafundisho ya kiyahudi?
Unaweza kutoa mfano hata kwa jambo moja ndugu
 
Kwanza kwa ushahid wa Quran wenyewe

Mwenyezi Mungu (s.w) ameikusudia Qur-an iwe kitabu hata kabla ya kuumbwa chochote katika maumbile yake aliyo yaumba.Kama inavyoashiriwa katika aya mbali mbali kwamba Qur-an ilikuwako kwenye Lawhil Mahfudh hata kabla ya kuteremshwa kwa Mtume (s.a.w) kulingana na matukio mbali mbali yalivyotokea:

“Bila shaka hiki (mnacho somewa) ni kitabu kilichokusanya kila yanayohitajiwa na chenye heshima. Kimetolewa katika hicho kitabu kilicho hifadhiwa kweli kweli."
(Qur-an 56:77-78).


"Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu."
(Qur'an 2:2).

vile rejea Qur-an 3:3, 7; 7:2; 10:1; 13:1; 14:1, n.k

Kutokana na marejeo hayo haiwezekani kuwa pawe hapana kitu cha aina hiyo lakini bado Mwenyezi Mungu arudie namna hiyo neno "kitab" linatumika kwa vitu mbali mbali vilivyoandikwa kama mikataba au hata barua lakini bado katika Qur-an neno hili limetumika kurudia kitabu katika maana halisi hasa ya kitabu.

Hivyo Allah(s.w) alipotaja neno Al-Kitab kwa kuirudia Qur-an alikuwa na maana hiyo .

Ushahidi wa kihistoria

Katika hadithi maarufu sana iliyo pokelewa na Imam Muslim toka kwa Ibnu Mas-'ud, Mtume amesema katika Hijja yake ya kuaga kuwa:

"Na nimewaachieni vitu wili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu - Kitabu cha Allah na Sunnah yangu." (Musilim)

Hadith hii kiakili haiashirii kitu ambacho hakijulikani kilipo na chenye ugumu kupatikana kama alivyoeleza Zaid (r.a) bali ni kitu ambacho kila mmoja anatarajiwa kukifikia pasipo na ugumu wowote. Wala Hadith hii haishirii kitu ambacho kimetawanyika katika mawe na mifupa ambayo pa kupatikana hapafahamiki bali ni kitu kilichokusanywa na kuhifadhiwa mahala
maalumu.Mtume(s.a.w) asingelisema hivyo kama kitabu hicho hakikuwepo

Ukiacha hadithi hiyo, kuna hadithi nyingine ambayo ameipokea mwenyewe Imamu Bukhari ambayo inasema wazi kabisa kuwa Mtume ameacha Msahafu:

'Abdul'-Aziz bin Rufai(ra) ameeleza kuwa: "Mimi na Shaddad bin Ma'aqil tuliingia kwa Ibnu "Abbas. Shaddad akamuuliza:
Je Mtume (s.a.w) ameacha chochote?" akajibu (Ibn 'Abbas) "Hakuacha chochote isipokuwa (hiki) kilichopo baina ya magamba mawili (ya Qur-an)." Baadaye tulimtembelea Muhammad bin Al-Hanafiyya na akamuuliza suala (lile lile). Akajibu (Al-Hanafiyya), Mtume hakuacha kitu isipokuwa (hiki) kilichopo baina ya magamba mawili (ya Qur-an)."

Hadithi hii, kwanza, inaisadikisha Qur-an kuwa ni kitabu (mas-hafu) ambacho kimeandikwa katika kurasa na kuwekewa magamba (bindings or covers) ili kihifad hike.

Pili, Hadithi hii inaisadikisha Hadith tuliyoirejea juu miongoni mwa vitu ambavyo Mtume ameviacha. Hapa tunaambiwa alichoacha ni kile kilicho baina ya magamba mawili - la mwanzo na mwisho - yaliyokuwa yamehifadhi Qur-an ambayo hapana shaka ilikuwa ndani ya karatasi za aina yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…