Unaweza kuweka chanzo cha kihistoria kuwa Quran ilikuwa compiled Karne ya 7? Data zote nilizoziona ni kuwa ilikuwa compiled angalau miaka 200 baadaye. Kitu kinachomaanisha hakukuwa na shuhuda hata mmoja.
Huyu swahaba aliandika vitabu vyake karne ya ngapi?
Kwanza kwa ushahid wa Quran wenyewe
Mwenyezi Mungu (s.w) ameikusudia Qur-an iwe kitabu hata kabla ya kuumbwa chochote katika maumbile yake aliyo yaumba.Kama inavyoashiriwa katika aya mbali mbali kwamba Qur-an ilikuwako kwenye Lawhil Mahfudh hata kabla ya kuteremshwa kwa Mtume (s.a.w) kulingana na matukio mbali mbali yalivyotokea:
“Bila shaka hiki (mnacho somewa) ni kitabu kilichokusanya kila yanayohitajiwa na chenye heshima. Kimetolewa katika hicho kitabu kilicho hifadhiwa kweli kweli."
(Qur-an 56:77-78).
"Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu."
(Qur'an 2:2).
vile rejea Qur-an 3:3, 7; 7:2; 10:1; 13:1; 14:1, n.k
Kutokana na marejeo hayo haiwezekani kuwa pawe hapana kitu cha aina hiyo lakini bado Mwenyezi Mungu arudie namna hiyo neno "kitab" linatumika kwa vitu mbali mbali vilivyoandikwa kama mikataba au hata barua lakini bado katika Qur-an neno hili limetumika kurudia kitabu katika maana halisi hasa ya kitabu.
Hivyo Allah(s.w) alipotaja neno Al-Kitab kwa kuirudia Qur-an alikuwa na maana hiyo .
Ushahidi wa kihistoria
Katika hadithi maarufu sana iliyo pokelewa na Imam Muslim toka kwa Ibnu Mas-'ud, Mtume amesema katika Hijja yake ya kuaga kuwa:
"Na nimewaachieni vitu wili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu - Kitabu cha Allah na Sunnah yangu." (Musilim)
Hadith hii kiakili haiashirii kitu ambacho hakijulikani kilipo na chenye ugumu kupatikana kama alivyoeleza Zaid (r.a) bali ni kitu ambacho kila mmoja anatarajiwa kukifikia pasipo na ugumu wowote. Wala Hadith hii haishirii kitu ambacho kimetawanyika katika mawe na mifupa ambayo pa kupatikana hapafahamiki bali ni kitu kilichokusanywa na kuhifadhiwa mahala
maalumu.Mtume(s.a.w) asingelisema hivyo kama kitabu hicho hakikuwepo
Ukiacha hadithi hiyo, kuna hadithi nyingine ambayo ameipokea mwenyewe Imamu Bukhari ambayo inasema wazi kabisa kuwa Mtume ameacha Msahafu:
'Abdul'-Aziz bin Rufai(ra) ameeleza kuwa: "Mimi na Shaddad bin Ma'aqil tuliingia kwa Ibnu "Abbas. Shaddad akamuuliza:
Je Mtume (s.a.w) ameacha chochote?" akajibu (Ibn 'Abbas) "Hakuacha chochote isipokuwa (hiki) kilichopo baina ya magamba mawili (ya Qur-an)." Baadaye tulimtembelea Muhammad bin Al-Hanafiyya na akamuuliza suala (lile lile). Akajibu (Al-Hanafiyya), Mtume hakuacha kitu isipokuwa (hiki) kilichopo baina ya magamba mawili (ya Qur-an)."
Hadithi hii, kwanza, inaisadikisha Qur-an kuwa ni kitabu (mas-hafu) ambacho kimeandikwa katika kurasa na kuwekewa magamba (bindings or covers) ili kihifad hike.
Pili, Hadithi hii inaisadikisha Hadith tuliyoirejea juu miongoni mwa vitu ambavyo Mtume ameviacha. Hapa tunaambiwa alichoacha ni kile kilicho baina ya magamba mawili - la mwanzo na mwisho - yaliyokuwa yamehifadhi Qur-an ambayo hapana shaka ilikuwa ndani ya karatasi za aina yake