Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

kama alizaliwa tarehe 8/6 mbona siku ya kuzaliwa inaadhimishwa mwezi wa 10
Ahsante ndugu yangu, Kalenda ya Hijri (kalenda ya kiisilamu) inachukuliwa kuwa moja ya kalenda nne kuu zinazotumika sasa ulimwenguni. Mwaka wa Hijri unamaanisha uhamiaji wa Nabii wetu Muhammad (amani iwe juu yake) (Hijira) kutoka mji wa Makka kwenda mji wa Madina El Monawara mnamo 622AD. Hapo ndipo tulianza kutumia kalenda ya Kiisilamu, na ndio maana mazazi ya mtume yanafuata kalenda ya kiisilamu nasio kalenda hii iliyo zoeleka.
 
Cha ajabu wachangiaji watakuwa wa upande mwingine na kukejeli kwa kashfa na matusi

Ni ajabu moja nimeiona JF uzi ukiletwa wa wakristo wachangiaji wengi wanakuwa ni wakristo kwa mfano jana uzi kuhusu RC na ndoa
Waislamu walipita kushoto kwani hauwahusu

Ila sasa uzi wa kiislam ndio utajua wakristo wana chuki mbaya tena ya wazi
Kuuliza maswali ni sawa ila kama hayakuhusu unapita kimya sio mpaka uonyeshe chuki kwa wengine
 
Ni kweli mtume alilaniwa na Babaye?
Ahsante ndugu yangu, si kweli, Mtume Muhammad hakunalaaniwa na Baba yake kwasababu, baba yake na mtume anaitwa Abdullah alikuwa ndiye mtoto kipenzi cha Mzee Abdul Muttalib. (Babu yake Mtume). Abdallah Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba, alimuoa Bi Amina, bibi wa uzao bora wa Yathrib, mji ulioko Kaskazini ya Makka. Huyu ABDALLA (Baba yake Mtume) Hakuwa hata hivyo, amekadiriwa kuishi muda mrefu, na akafa miezi saba tu baada ya ndoa yake. Muhammad, Mtume wa Mungu wakati huo alikuwa bado mimbani. Kwa hivyo Baba yake mtume amefariki mtume akiwa bado tumboni.
 
Ahsante. Buraq maana yake ni "mwendo mkali mfano wa umeme" au kwa ujumla "ni kama mwanga wa radi") ni kiumbe katika mila ya Kiisilamu ambaye alitumika kama usafiri kwa manabii fulani. Buraq alimbeba nabii wa Kiislam Muhammad kutoka Makka kwenda Yerusalemu na kwenda juu mbinguni na kurudi usiku huo huo. Kwasababu alikuwa akikimbia sana, anatua pale macho yake yanapoishia kutazama, alikuwa kikimbia mfano wa speed ya mwanga.
Pia Ibrahimu alipomtembelea Hajiri na Ishmaeli. Ibrahimu aliishi na Sara huko Kanaani lakini usafiri wake ilikuwa ni Buraq walimsafirisha asubuhi kwenda Makka kuiona familia yake huko na kumrudisha jioni.

Ingawa Hadithi haionyeshi Buraq wazi kuwa na sura ya kibinadamu, bali hiyo ni sanaa ya Kiislamu ya Uhindi na Uajemi. Hii inaweza kuwa ilitokana na tafsiri ya kiumbe kuelezewa kuwa na "uso mzuri" kama uso wa kibinadamu badala ya mnyama.
Kwenye translation ya mwanazuoni wa kiislamu maarufu kama Ibn Ishaq, alimuelezea buraq kama mnyama ambaye ni mnyama nusu farasi nusu mtu akiwa na mabawa pembeni

image ambayo unaweza ukaijenga kwa sifa hizo alizoelezea huyo mwanazuoni unaweza ukapata picha hii

817896-29673797262_7baa39fbf7_z.jpg

Mimi nilikuwa nataka kuuliza tu, habari hiyo ni ya kweli au yakufikirika? Vigezo gani vilivyotumika kuthibitisha uhalisia wa hilo tukio?
 
Cha ajabu wachangiaji watakuwa wa upande mwingine na kukejeli kwa kashfa na matusi

Ni ajabu moja nimeiona JF uzi ukiletwa wa wakristo wachangiaji wengi wanakuwa ni wakristo kwa mfano jana uzi kuhusu RC na ndoa
Waislamu walipita kushoto kwani hauwahusu

Ila sasa uzi wa kiislam ndio utajua wakristo wana chuki mbaya tena ya wazi
Kuuliza maswali ni sawa ila kama hayakuhusu unapita kimya sio mpaka uonyeshe chuki kwa wengine
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ

Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. [Al-Baqarah (2: 120)]

Cha ajabu, kwa upande wa waisilamu wa jamiiforum n.k mada muhimu kama hizi huwezi waona ila wachache sana, hata kuchangia tuu hamna. Mleta mada anajikuta kaambulia wachangiaji wachache sana kama 2onavyo manaswara wameingia kuuliza maswali, na wengine wanapitisha kejeli,,,,. Lakinii nenda jukwaa la siasa, mapenzi, sports, jokes, international furum n.k utawakuta waislamu kama co wengi bac ni wachache wao wakichangia.
 
Ni kweli kitabu tukufu alikuwa anapewa haya zake mapangoni na majini?
Na ni kwanini mjomba wake alimkataa kuwa yeye sio mtume wa MUNGU?
Ufunuo wa kwanza wa Muhammad lilikuwa tukio lililoelezewa katika mila ya Kiisilamu kama ilifanyika mnamo AD 610, wakati ambapo nabii wa Kiislam, Muhammad alitembelewa na malaika Jibrīl, anayejulikana kama Gabrieli kwa Kiingereza, ambaye alimfunulia mwanzo wa kkitabu cha Qur.'an. Hafla hiyo ilifanyika katika pango liitwalo Hijra, lililoko kwenye mlima Jabal an-Nour, karibu na Makka. Ilikuwa Jumatatu, tarehe 21 ya Ramadhani kabla tu ya jua kuchomoza, yaani Agosti 10, 610 - wakati Muhammad alikuwa na miaka 40. Baada ya hapo aya za kitabu kitukufu zilikuwa zikishuka kulingana na matukio husika nasio mapangano.

.............
Abu Lahab alikuwa mjomba wa mtume Muhammad, ndiye mtu pekee kutoka kwa maadui wa Uislamu ambaye amelaaniwa kwa jina lake katika Qur'an Tukufu. Baada ya mtume kutangaza kuwa yeye ni mjumbe wa MUNGU Watu walitawanyika wakinung'unika kimya kimya, lakini Abu Lahab, ambaye kila wakati alimpenda mpwa wake Mohammed (S.A.W.), alimpinga vikali kwa sababu aliona ujumbe huo kuwa changamoto kwa uongozi wake.

Wakati Mtume Muhammad (SAW) alikuwa akitoa hotuba yake ya kwanza hadharani wakati akiwaalika watu wa kabila la Quraishi kwenye Uislam kwa mara ya kwanza hadharani, hakuna mtu aliyemtukana Nabii Mohammed (s.a.w) ispokuwa mjomba wake Abu Lahab mwenyewe, Nabii Mohammed (s.a.w) alitumia kimya kujibu tusi la Mjomba wake lakini Mwenyezi Mungu (SWT) hakufanya hivyo na akafunua ufunuo wa kumlani Abu lahab. Hivyo basi alimpinga mtume kwa kuhofia uwongozi wake.
 
Kwenye translation ya mwanazuoni wa kiislamu maarufu kama Ibn Ishaq, alimuelezea buraq kama mnyama ambaye ni mnyama nusu farasi nusu mtu akiwa na mabawa pembeni

image ambayo unaweza ukaijenga kwa sifa hizo alizoelezea huyo mwanazuoni unaweza ukapata picha hii

817896-29673797262_7baa39fbf7_z.jpg

Mimi nilikuwa nataka kuuliza tu, habari hiyo ni ya kweli au yakufikirika? Vigezo gani vilivyotumika kuthibitisha uhalisia wa hilo tukio?
Hii picha ilishawahi niathiri kisaikolojia nilipokuwa mtt kwa kupanda bus lenye picha hii nilishtuka sana
 
Back
Top Bottom