Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Je, Mtume alisema siku ya kiyama tutapewa mabikira 70?
Je, kama ndivyo tutatumia mkongo au alkasusu?
1.Mkongo Na alkasusu Ni Mambo Ya Maisha haya ya kidunia.

Na Baada ya maisha haya hakutakua na Mambo hayo.

2.Mwenyezi MUNGU mtukufu atawaumba waumini kwa umbo jipya ambalo litaendena na hali hiyo hivyo kuondoa haja ya kutumia Mkongo na alkasusu!
 
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ

Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. [Al-Baqarah (2: 120)]

Cha ajabu, kwa upande wa waisilamu wa jamiiforum n.k mada muhimu kama hizi huwezi waona ila wachache sana, hata kuchangia tuu hamna. Mleta mada anajikuta kaambulia wachangiaji wachache sana kama 2onavyo manaswara wameingia kuuliza maswali, na wengine wanapitisha kejeli,,,,. Lakinii nenda jukwaa la siasa, mapenzi, sports, jokes, international furum n.k utawakuta waislamu kama co wengi bac ni wachache wao wakichangia.

Kweli kabisa mkuu
Mada nzuri ila wanapita kama hawauoni
 
Mohammed alikua SHIA au SUNNI?
Madhehebu ni mafundisho, maadili na matendo ya ibada yaliyo ya msingi katika dini fulani. Hutumiwa pia kutaja makundi ndani ya dini fulani ambayo yanatofautiana bila ya kuvunja umoja wa msingi. Historia inashuhudia hata leo kwamba madhehebu mbalimbali ya dini ileile yanaweza kushindana hata kupigana vita.

Mfano, Wafuasi wa dini ya Ukristo, kutokana na wingi wao katika urefu wa historia na upana wa jiografia, wamegawanyika katika madhehebu mengi, kuanzia Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki hadi makundi elfu kadhaa ya Uprotestanti ambayo yalitokea hasa karne za nyuma na yanazidi kuongezeka siku kwa siku.

Uislamu hugawiwa katika mikondo miwili mikubwa ambayo ni Wasunni na Washia. Washia ndani yao wamegawanyika katika makundi mengi zaidi. Kati ya Wasunni kuna madhehebu au madhhab manne yanayokubaliwa rasmi, madhehebu yote haya asili yake ni baada ya mtume kufariki. Hivyo mtume hakuwa na dhehebu
 
Cha ajabu wachangiaji watakuwa wa upande mwingine na kukejeli kwa kashfa na matusi

Ni ajabu moja nimeiona JF uzi ukiletwa wa wakristo wachangiaji wengi wanakuwa ni wakristo kwa mfano jana uzi kuhusu RC na ndoa...
Waafrika tuna roho mbaya sana. Asante umejibu vizuri sana. Mi ni mkristu ila siwezi kumsema vibaya mtu wa dini nyingine hayatuhusu hayo mambo. Yetu tu yanatushinda tukomae na yetu na kuheshimiana ndo jambo la msingi.
 
Swahili Muslims kuna chanzo chochote cha kihistoria kuhusu kuwepo kwa Muhammad rasul Allah, na kwamba aliishi na kufanya kama inavyoelezwa kwenye Quran, Sunnah na Sira? Angalau kilichoandikwa ndani ya miaka hata 50 baada ya uwepo wake, au kilichoandikwa na watu walioishi zama zake?

Nimejaribu kutafuta naona vingi vimeandikwa miaka mingi sana baadaye, angalau miaka 200 baadaye.
Ukinisaidia hii nitashukuru!
 
Kwa dini yetu ni sawa. Mwanamke wa miak 9 amepevuka! Sijui utofaut w hao wa miaka ile na sasa... Kislam mwanamke ni chombo tu kibachosevia uzazi na kumtumikia mume
baada ya jibu hili nimesitisha nilichotaka kuuliza, nimepata ukakasi na ujuzi na uadilifu wa mtoa mada.....kuna kitu kinaniambia tofauti, the guy is here just to make fun of islam!!!
 
Waafrika tuna roho mbaya sana. Asante umejibu vizuri sana. Mi ni mkristu ila siwezi kumsema vibaya mtu wa dini nyingine hayatuhusu hayo mambo. Yetu tu yanatushinda tukomae na yetu na kuheshimiana ndo jambo la msingi.

Najua sio wote wabaya la hasha
Naelewa mpo wenye roho nzuri na kuishi maisha yenu bila kuudhi mtu wala kashfa

Kuna threads nyingi nasoma zikiwa na maneno mabaya na yanakera haswa ila huwezi jua huyo mtu ana matatizo gani au nini kimempelekea mpaka awe na roho mbaya kiasi hicho

Asante
 
Kwa dini yetu ni sawa. Mwanamke wa miak 9 amepevuka! Sijui utofaut w hao wa miaka ile na sasa... Kislam mwanamke ni chombo tu kibachosevia uzazi na kumtumikia mume

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Je ni kweli mtume alizaliwa akiwa ametahiriwa?

Je ni kweli mtume hakuwa na kimvuli hata alipotembea juwani?

Je Uislami unaamini Masia ndio atahukumu wazima na wafu siku ya mwisho.?
 
Ahsante. Buraq maana yake ni "mwendo mkali mfano wa umeme" au kwa ujumla "ni kama mwanga wa radi") ni kiumbe katika mila ya Kiisilamu ambaye alitumika kama usafiri kwa manabii fulani. Buraq alimbeba nabii wa Kiislam Muhammad kutoka Makka kwenda Yerusalemu na kwenda juu mbinguni na kurudi usiku huo huo. Kwasababu alikuwa akikimbia sana, anatua pale macho yake yanapoishia kutazama, alikuwa kikimbia mfano wa speed ya mwanga.
Pia Ibrahimu alipomtembelea Hajiri na Ishmaeli. Ibrahimu aliishi na Sara huko Kanaani lakini usafiri wake ilikuwa ni Buraq walimsafirisha asubuhi kwenda Makka kuiona familia yake huko na kumrudisha jioni.

Ingawa Hadithi haionyeshi Buraq wazi kuwa na sura ya kibinadamu, bali hiyo ni sanaa ya Kiislamu ya Uhindi na Uajemi. Hii inaweza kuwa ilitokana na tafsiri ya kiumbe kuelezewa kuwa na "uso mzuri" kama uso wa kibinadamu badala ya mnyama.
Jitahidi kupitia marejeo yako(vitabu).
Buraq alitumika kutoka Macca hadi Jerusalem (Israa). Kutoka Jerusalem hadi mbinguni ilitumika ngazi(mi-iraaj).
Ndio sababu ya kuitwa safari hiyo "israa na mi'iraaj)
 
Yeye (Muhammad Ibn Abdullah) alizaliwa katika nyumba ya ami yake, Abu Talib, katika “mtaa wa Bani Hashim” huko Makka, tarehe 12 Rabil-awal ya ule Mwaka wa Tembo, tarehe ambayo inaoana na tarehe 8 Juni 570.

Mama yake na mtume Muhammad (s.a.w), Bi Amina, alituma habari za uzazi huu wa kheri kwa babu yake na Muhammad, Mzee Abdul Muttalib, ambaye alikuja, akamchukuwa mikononi mwake, na akampa jina hili la Muhammad.” Lenye maana ya MSIFIWA.

Nawakaribisha kuuliza maswali kuhusu mtume wetu huyu MUHAMMAD "amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake".

View attachment 1975182
wanasema sababu ya waislam kutokula kitimoto (nguruwe) japo wengine wanakula kwa kuvizia. Wanasema kwamba walimzika Muhhamad wakamuacha mkono unanin'ginia nje ili afufuke, nguruwe akapita nao.

i.) Je ni kweli?

ii.) Nipe sababu za waislam kula nguruwe (kitimoto) kwa kuvizia au kutokula kabisa.
 
HAYA NI MAMBO YA KIIMANI ZAIDI. KWANI NI VIGEZO GANI VILIVYOTUMIKA KUTHIBITISHA MIMBA YA YESU, KWAMBA ILIPATIKANA BILA BABA? MIMI NA WW TUNAAMINI ILIPATIKANA KWA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU, LKN WAYAHUDI MPK LEO WANAAMINI KWMB YESU NI MTOTO WA ZINAA
Mimi nimehoji kwa lengo la kujua uhalisia wa hiyo habari kama zipo njia zilizowahi kuthibitisha hiyo habari.

Nitakupa mfano mmoja kwenye kuran ukiongelea jambo la imani kuhusu bahari mbili yaliyoungana bila maji yao kuchanganyana, na ni ukweli maji hayo yapo na yanathibitishika japokua yameongelewa kwenye mambo ya kiimani

Sasa leo hii nikiuliza kua habari hiyo ya maji kutochanganyikana inauhalisia wowote sitategemea kuambiwa "hayo ni mambo ya kiimani"

Hizo habari za yesu naona umezi-propose kua kwa namna moja nitakua nazikubali au kuziamini kwakuni perceive kama mkristo, kitu ambacho sio. Hayo ni madai , ila ikitokea nimepewa fursa ya kuuliza maswali basi nitaomba kuuliza kama madai hayo yana uthibitisho wowote au ni stori za watu tu.
 
Back
Top Bottom