Tumechoka na Kampeni za Hedhi Salama 'Maredioni'. Himizeni Mabinti kuacha Tamaa na Kumomonyoka Kimaadili

Tumechoka na Kampeni za Hedhi Salama 'Maredioni'. Himizeni Mabinti kuacha Tamaa na Kumomonyoka Kimaadili

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kila Siku tu ukifungulia Redio mbalimbali Mada nyingi ni Hedhi kwa Mabinti hadi wengine sasa mnatutia Kinyaa tu kutokana na wengine kuelezea jinsi Damu zinavyotoka.

Huu muda mnaoutumia kufanya Kampeni za Hedhi Salama kwa Mabinti utumieni katika Kuwajenga zaidi Kimaadili na kuwaasa waache Tamaa na wasiwe Mazuzu ( Majuha ) katika Jamii.

Mbona miaka ya zamani akina Bibi zetu, Mama zetu, Shangazi zetu na Dada zetu walikuwa hawapati Changamoto zozote na Shule walikuwa Wanaenda, Wanafaulu, walikuwa Werevu na mpaka Wametuzaa Sisi Watoto Wao tuliorithi Uwerevu wao?

Acheni Unafiki na jikiteni katika Mambo ya Msingi juu ya hawa Mabinti na siyo Kelele za Kutwa za Hedhi Salama.

Nimemaliza.
 
Kila Siku tu ukifungulia Redio mbalimbali Mada nyingi ni Hedhi kwa Mabinti hadi wengine sasa mnatutia Kinyaa tu kutokana na wengine kuelezea jinsi Damu zinavyotoka...
Huyu anadhani hedhi inatokana na ufuska! Kichaa huyu hajui siku hizi makundi makubwa ya wasichana wako mashuleni na hawana uwezo wa kununua sodo.
 
Usichokijuwa wewe hizo ni ajira za watu na NGO zao.

Zamani wakati jukumu la kumsomesha mtoto lilikuwa ni jukumu la Serikali watu walizaana kama panya mpaka ikaja kampeni ya nyota ya kijani.

Lakini ugumu wa maisha umewatia displini wabongo kiasi kwamba family plan wala haiitaji makelele popote, bill za shule tu tayari zinakutia akili na kufunga zipu yako.
 
Hivi karibuni kulikua na kampeni ya siku ya hedhi duniani kama sikosei, ndio maana matangazo na msisitizo ukawa wa kutosha na maeneo mengi ikawa ni ajenda kuu.

Sijaona hedhi inaingiliana vipi na mabinti kusisitizwa kuhusu maadili, hizo ni kampeni mbili tofauti na hazi ingiliani.

Ni kweli mambo mengi zamani yalifanyika tofauti haimaanishi yote yabaki vilevile, mambo yanabadilika.
 
Back
Top Bottom