Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Kama wafuasi wa kwenye mtandao watakufikisha mbinguni basi sawa ila kama ni wa hapa hapa Duniani hawana maana kwa hili nadhani watanzania tuache roho mbaya tumrudie Mungu watu wa Mungu siku zote huombeana mema hata kama umekosewa hutakiwi kumlaani mtu maana na wewe utalaaniwa na katika maisha tujifunze hakuna aijuwaye kesho yake zaidi ya Muumba wa Mbingu na nchi ukijiuliza ni mangapi tunatenda ya kumchukiza Mola na bado anatupatia tuombayo ila sisi tunaishi maisha ya chuki fitna husda na kuombena mabaya hakika Ni chukizo kwa Mungu zaidi ya yote ukimwona mtu anamwombea mabaya jirani yake ujue anafanya kazi ya shetani wengi tunasema tunampenda Mungu ilhali wamchukia nduguyo au jirani yako unayemuona kwa macho huku ukijitakabali wampenda Mungu usiyemuona huo ni unafiki na lifungwalo duniani na Mbinguni limefungwa watu wote tumrudie Mungu tutakiane Amani
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia kwenye kuvuja kwa siri za Ikulu.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 2.4 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia ya kitendo iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini na kuushadadia wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni kuwa viongozi wetu wa vyama vikuu vya upinzani nchini hawajui kinachoendelea Ikulu. Hii imekuja baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji, Godbless Lema na Lazaro Nyalandu wakiamini na kuushadadia uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu! Lazaro Nyalandu na Dkt Mashinji wanatoa mpaka ujumbe wa kuliombea Taifa huku wakiambatanisha mishumaa!

Haya ni maendeleo makubwa kwa taasisi/watu waliopewa dhamana ya kumlinda Rais na siri za Ikulu.

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
 
Mimi nimejifunza kuwa wananchi wanataka kujua afya ya kiongozi wao.
 
FATMA ni whistleblower, hahitaji wafuasi.
Ni k

ama kusema mtu ni mfuasi wa MANGE KIMAMBI AU SARUNGI, kama hujui uliza, si dhambi?

Kwani lazma hawa wawe mbadala wetu sisi CCM?
CHEYO , LIPUMBA wanatosha, si lamza CHADEMA
Sasa huku ona mange alivyokuwa amewashika akili hadi Mbowe?
 
Kutungwa uongo kunasaidia taifa au kunalipumbaza taifa.
Mkuu mimi sizungumzii kama huo uongo unalisaidia au unalipumbaza Taifa,hayo nakuachia wewe uamuwe.Shida yangu ni kuona kwamba watanzania wanawezaje kuombeana au kuomba mtu AFE.HII SI KAWAIDA.Tuliona kwa Lissu jinsi watu walivyofurahi kushambuliwa kwake.Na sasa kwa Mh.HII SI TANZANIA TULIYOACHIWA na Baba wa Taifa,,Tanzania iliyojaa upendo.SIYO.Bahati mbaya sana wajinga wachache mambo muhimu kama haya yanapotokea wanaingiza siasa zao za kijinga za UChadema na UCCM.Kama tumeshindwa kurudi kwenye misingi ya Baba wa Taifa basi angalao tubaki hapo kwenye msing wa rais mstaafu Kikwete(UPENDO).Tunapenda kuona vile ilivyokuwa spika mstaafu mama Anna Makinda akisakata rumba na Lissu mtu ambaye muda mchache ametoka kumsumbuwa Bungeni.
 
Nimekusoma...

Kiukweli sina nililojifunza maana wabongo ni wabongo tu, tegemea lolote. liwe lina ukweli ama la, mimi nakanyaga tu.

Ila nipo kwenye thread yako kwa ajili yakumtakia Rais wangu afya njema.
 
Na Elius Ndabila
0768239284

Niseme kuwa weekend hii ilikuwa mbaya sana kwangu, ilikuwa ni weekend ambayo kila nikitazama Tanzania sikupata matumaini tena. Ni weekend ambayo ninaamini wapo wengi ambao afya zao zimeharibiwa na huenda hata wengine tumewapoteza uhai wao. Ni weekend hii ambayo watu walizua mambo ya hovyo juu ya Taifa letu. Nilisikitika kuona Watanzania wanaweza kuanzisha jambo tena la kifo bila hata haya. Nilisikitishwa kwa watu wanaoaminiwa kwenye vyama vyao kushangilia jambo hilo kana kwamba wao wana miliki ya maisha yaw engine. Sikutegemea kuona upuuzi huo ukisambazwa na Zito kiongozi mkubwa bila ya kuwa na ushahidi wa jambo lenyewe. Hapa ndipo nilipoona utofauti wa MH Mbowe matured na Zitto(utoto).

Kuonyesha kuwa walitengeneza kwa kusudi maalumu, aliposikia kuwa mchana Mh Rais ataapisha viongozi mchana, Zito akaja na andiko lake la kuomba samahani na kutaka kujua mambo matatu. Uetengeneza taharuki then unaomba radhi, for what? Nilijiuliza maswali, Kama siku zote twetter zake zilijaa upuuzi juu ya Rais na leo anasema anaomba radhi je siku zote alipokuwa anatuma habari hizo kwenye mitandao alikuwa hana utu? Nilijiuliza, kuna uhusiano gani wa mtu anayejiita Kigogo@2014 na ZITO? Kamahakuna uhusiano kwa nini walilibebea bango hili jambo?

Jana bada ya kumuona kipenzi cha Watanzania Wanyonge, ambao kwa miaka mingi walinyonywa na kuporwa mali zao moyo wangu ulitulia. Baada ya moyo kutulia ndipo niliposhika biblia na kuanza kumsoma Yosefu ambaye Biblia inamtaja kama mtu shujaa na aliyeshinda majaribu mengi. Kwa kazi anayoifanya JPM inahitaji uzalendo, utashi, ujasiri na weredi wa hali ya juu. Inahitaji mtu aliyejitoa rohona mwili kama sadaka kwa Watanzania. Kwa kazi anazofanya JPM ni jambo la kawaida kupitia mapito kama ya Yosefu na akashinda. Watanzaniawengi wanamhitaji JPM ndio maana dua za hao wachache waliokesha mitandaoni sikutatu wameshindwa.

Hebu njoo nikupe kisa cha Yosefu huenda kikakuongeza kitu kichwani mwako, Yosefu alikuwa kijana tu mwenye umri wa miaka 17 au 18—lakini alikabili magumu ambayo yangeweza kuwavunja moyo watu wazima. Ndugu zake, walimwonea wivu kwa sababu Yosefu alipendwa sana na baba yake, hata walikuwa karibu kumuua. Badala ya kumuua walimuuza kwa wafanyabiashara hao. (Mwanzo 37:2, 5, 18-28) Sasa, baada ya kusafiri kwa majuma kadhaa, wafanyabiashara hao wanafurahi wanapozidi kukaribia jiji kubwa mahali wanakokusudia kupata faida kubwa kwa kumuuza Yosefu pamoja na bidhaa zao za thamani. Ni nini kilichomsaidia Yosefu kutovunjika moyo na kukata tamaa? Na tunawezaje kukabiliana na hali ngumu na mambo yenye kuvunja moyo maishani bila kudhoofisha imani yetu? Tuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa Yosefu. Ukweli ni kuwa JPM ataendelea kushinda kila jaribu kwa kuwa Watanzania waliodhurumiwa kwa miaka mingi ni wengi kulikowaliokuwa wakitudhurumu. Hivyo dua za waliozoea kuwanyonya walalao hoi ni dhaifu kuliko dua za waliokuwa walala hoi kwa kipindi hicho. Wezi sasa hawana uwezo wa kulitikisa taifa kwani JPM ameamuakufa ni masilahi ya wengi. Ndivyo hata Yosefu alivyofanya.

Ukisoma historiaya Yosefu inaeleza mambo mengi sana aliyoyashinda. Hata hivyo wachimbuaji wa vitu vya kale wanasema kwamba Wamisri wa kale walipenda anasa, kulikuwa na bustani zilizozungushwa ukuta pamoja na miti ya kivuli na visima vilivyotumiwa kukuza mafunjo, mayungiyungi na mimea mingine ya majini. Nyumba nyingine zilijengwa ndani ya bustani, pamoja na varanda kwa ajili ya kupunga upepo, madirisha makubwa ya kupitishia hewa, na vyumba vingi kutia ndani chumba kikubwa cha kulia chakula na nyumba za watumishi. Ukifananisha na maisha halisi ya Watanzania, basi haya maisha ndiyo walizoea kuishi wezi, wabadhilifu wa mali zau umma na waliotutengenezea mikataba mibovu. JPM amekuja kuharibu bustani zao zote na kuondoa miti ya kivuri liyotengenezwa kwa fedha za walala hoi.

Je, Yosefu alivutiwa sana na starehe hizo? Inaonekana sivyo. Zaidi ya yote, inaelekea alijihisi upweke sana. Kulikuwa na tofauti kati yake na Wamisri katika lugha, mavazi na mapambo, na hasa dini. Waliabudu miungu mbalimbali ya uwongo, walizoea kufanya mazingaombwe na ufundi wa uchawi, na walivutiwa na kifo na maisha baada ya kifo. Hata hivyo kuna jambo lililomfanya Yosefu asilemewe na upweke. Simulizi la Biblia linatuambia hivi: “Yehova alikuwa pamoja na Yosefu.” (Mwanzo 39:2) Kwa hakika Yosefu alimweleza Mungu hisia zake. Biblia inasema kwamba “Yehova yuko karibu na wote wanaomwitia.” (Zaburi 145:18) Ni jambo gani lingine lililomfanya Yosefu awe karibu na Mungu wake?

Biblia inatukumbusha kuwa Yosefu alishinda majaribu mengikwa kuwa alimtanguliza Mungu kwenyekila jambo. Alitambua kuwa ana maadui lakini ili kuwashinda alijua silaha pekee ni kumtanguliza Mungu. Siasa zisituondolee utu, kuumwa ni kwa binadamu yeyote. Hata kama Raisaliuwa kwani tatizo liko wapi? Kuna mtu haugui? Anzisheni vita nyingine hii kama mlitaka kumtega, basi mumejitega.Huenda tukapatwa na hali zenye kuhangaisha na hata kutendewa isivyo haki, lakini tunaweza kujifunza kutokana na imani ya Yosefu. Ikiwa tunaendelea kuwa karibu na Yehova kupitia sala, kubaki washikamanifu kwa amri zake, kujitahidi kufanya yaliyo sawa machoni pake, tutampa nafasi ya kutubariki. Katika kisa cha Yosefu, Yehova aliendelea kumbariki.
 
Chuki ilikuwepo na itaendelea kuwepo hata aje nani as long as chadema wapo! Chadema hawajawahi kuishiwa chuki
Angalia hapa comments zao baada ya kikwete kuanguka 2010, soma mstari kwa mstari

Hao cdm wanatendewa haki? Kama hawatendewi haki nitashangaa sana kama hawataonyesha hisia zao kwa mkandamizaji yoyote. Tena hata huyu Zitto kachemsha sana kuomba msamaha, alipaswa akae kimya maana hizo ndio siasa zetu. Wapinzani wanapigwa na kuumizwa hata kuuwawa, acha kufanyiwa hujuma za wazi kwenye chaguzi kwa maagizo ya viongozi, kisha wajifanye eti kuna upendo. Kama wapinzani hawana uwezo wa kujitetea pindi wanapofanya ukatili kwa uratibu wa vyombo vya dola, basi hata hisia zao washindwe kuonyesha? Unapofanyiwa ukatili ukajifanya una busara ni wendawazimu.
 
Nimpongeze Tundu Lisu, amekaa kimya na hata alipotaka kusema alitamka maneno ya kuomba heri ya Mhe.Rais. Kwamba ameandika kutoka moyoni au la ni Siri yake na Mwenyenzi Mungu.
Lisu ameishagundua waliompiga risasi ni kundi la wahuni wasiotaka kuachia U/Kiti wakiongozwa na Mbowe Mugabe!
 
Katika mambo ambayo upinzani wanajivua heshima ni pamoja na kushadadia upuuzi ambao unageuka kua aibu na fedheha kwao.

1. MPUUZI mmoja alisema Tanzania itafulisiwa kwa kuzuia makinikia. Karibuni tumeshuhudia kampuni mpya ambayo Tanzania itapata share 16%

2. Bombadia ikakamatwa wakachonga sana kwamba na bado. Tukapeleka wanasheria makini tukashinda kesi ndege ikaachiwa.

3. Wametuzulia taharuki takribani siku tatu kua Rais Ni mgonjwa na kapelekwa Ujerumani, Jana Mubashara tumemuona akiwaapisha wateule.

SASA
Nyie mnaochonga unapomuona Kobe kainama jua anatunga sheria. Na dawa yenu ikishachemka mtainywa tena kwenye mustin (vikombe vya bati) tena ikiwa ya moto.

KUNA WAKATI NAJIULIZA
Hivi mlikua mnafurahia yale yaliyokua yakitendeka serikalini kabla ya awamu ya Tano (angalizo najua bado hajaisha lakini afueni ni kubwa sana)

Labda nitaje machache
1. Familia kufanya sherehe mtoto akipata kazi TRA

2. Magogo/nguzo za TANESCO kukatwa Tanga kupelekwa Mombasa Kisha kuonekana ni imported.

3. Kufungulia maji kwenye mabwawa ya kuzaliasha umeme ili kina kipungue watu wauze majenereta.

4. Magari ya mafuta kupewa vibali vya transit yakaenda hadi tunduma na kurudi kimara kupakua mafuta yasiyolipiwa kodi hata sh 1.

5. Viongozi wa uma kulipana posho kwenye vikao vya brainstorm ndani ya ofisi.

Hivi Rais Magufuli kawakosea nini hasa? Ni kwa kua kaamua kusimamia raslimali za Taifa hili?

Tuambieni kosa lake? Mnasema kaminya democrasia, Ni kweli lakini tujiulize wakati Kikwete alivyoiruhusu hiyo mikutano ya siasa mlifanya nini? Mlipita nchi nzima kumnadi Lowassa kuwa fisadi kisha mkamkaribisha na kumpa nafasi ya kugombea uraisi.

Aliwapa Uhuru wa mnayoiita democrasia mkamtukana, mkamwita majina mkawazomea wanaccm waliopita na nguo za kijani mitaani, je lile ndilo lilikua jibu la yaliyokua yakiendelea serikalini?

Nawaza kwa sauti naishia kusema Kiongozi bora hawaulizi wananchi awafanyie nini? Bali hufanya lile ambalo Ni sahihi kwa jamii yake kwakua naye ni sehemu ya jamii hiyo.
 
chadema waige kutoka kwa Mbowe..
its ok awe kiongozi wa chadema milele
Hao cdm wanatendewa haki? Kama hawatendewi haki nitashangaa sana kama hawataonyesha hisia zao kwa mkandamizaji yoyote. Tena hata huyu Zitto kachemsha sana kuomba msamaha, alipaswa akae kimya maana hizo ndio siasa zetu. Wapinzani wanapigwa na kuumizwa hata kuuwawa, acha kufanyiwa hujuma za wazi kwenye chaguzi kwa maagizo ya viongozi, kisha wajifanye eti kuna upendo. Kama wapinzani hawana uwezo wa kujitetea pindi wanapofanya ukatili kwa uratibu wa vyombo vya dola, basi hata hisia zao washindwe kuonyesha? Unapofanyiwa ukatili ukajifanya una busara ni wendawazimu.
 
chadema waige kutoka kwa Mbowe..
its ok awe kiongozi wa chadema milele

Mimi sio muumini wa kiongozi yoyote wa kuchaguliwa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Mbowe ameshakaa zaidi ya miaka 10, huu ni wakati wake sasa kumpisha mwanacdm mwingine. Ni kweli nafahamu mchangu wa Mbowe kwa cdm, lakini wakati ukuta. Kama wewe umefaidika na Mbowe kwenye hili, mimi siangalii maslahi binafsi, bali naiangalia cdm kama taasisi, na uongozi wa taasisi ni kupokezana. Msimamo wangu huu uko wazi wala haubadilishwi na tukio lolote.
 
Back
Top Bottom