Kiwarhoapandenga
JF-Expert Member
- Aug 10, 2019
- 2,078
- 1,805
Kama wafuasi wa kwenye mtandao watakufikisha mbinguni basi sawa ila kama ni wa hapa hapa Duniani hawana maana kwa hili nadhani watanzania tuache roho mbaya tumrudie Mungu watu wa Mungu siku zote huombeana mema hata kama umekosewa hutakiwi kumlaani mtu maana na wewe utalaaniwa na katika maisha tujifunze hakuna aijuwaye kesho yake zaidi ya Muumba wa Mbingu na nchi ukijiuliza ni mangapi tunatenda ya kumchukiza Mola na bado anatupatia tuombayo ila sisi tunaishi maisha ya chuki fitna husda na kuombena mabaya hakika Ni chukizo kwa Mungu zaidi ya yote ukimwona mtu anamwombea mabaya jirani yake ujue anafanya kazi ya shetani wengi tunasema tunampenda Mungu ilhali wamchukia nduguyo au jirani yako unayemuona kwa macho huku ukijitakabali wampenda Mungu usiyemuona huo ni unafiki na lifungwalo duniani na Mbinguni limefungwa watu wote tumrudie Mungu tutakiane Amani
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia kwenye kuvuja kwa siri za Ikulu.
Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!
Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.
Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 2.4 kutoka laki 300000.
Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).
Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia ya kitendo iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini na kuushadadia wameonekana ni wajinga au wapumbavu.
Kitu kingine nilichojifunza ni kuwa viongozi wetu wa vyama vikuu vya upinzani nchini hawajui kinachoendelea Ikulu. Hii imekuja baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji, Godbless Lema na Lazaro Nyalandu wakiamini na kuushadadia uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu! Lazaro Nyalandu na Dkt Mashinji wanatoa mpaka ujumbe wa kuliombea Taifa huku wakiambatanisha mishumaa!
Haya ni maendeleo makubwa kwa taasisi/watu waliopewa dhamana ya kumlinda Rais na siri za Ikulu.
Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.
Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.
Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!