Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Zitto alipaswa kuwa mwanasiasa wa kwanza kujua kuwa ile ilikuwa fake news sababu ya direct connection ya Ujerumani kupitia wife!
 
Mnakosea kusema kunakuombewa kifo, unaombewa kwa nani?!

Kifo kinaombwaje?!

Mungu huyohuyo mnamuomba mema, huyohuyo mnamuomba mabaya, au Luna side mbaya ya Mungu?!
 
mimi sio chadema wala sio mfuasi wa Mbowe... ila ni mwanasiasa makini sana.

Inaniuma hata Mbowe kuwa na kesi ambapo ni ama ameonewa ama mambo ya mob.

nilichomaanisha ni kwamba kuna kiwango cha viongozi wa upinzani kuto act ama kuongea kitoto....

Mbowe ni mfano hai wa aina hiyo ya kiongozi. Akiongea Mbowe unashtuka. Akiongea Zitto una ignore
 
Kwa mambo yanaoendelea sasa, hakika inasikitisha sana...

Ila mkuki kwa... ...kwa binadamu mchungu...


Cc: mahondaw
 
Ben Saanane, Azory Gwanda na wengio ni Serikali ya Chama gani nani imewapoteza wewe ndezi?
Umekosa hoja unaishia kuonyesha uduanzi wako hapa. Baada ya kuzusha kifo hao uliowataja wamerudi? Kwa kauli yako inaonekana una ushahidi jinsi walivyopotezwa na serikali weka hadharani basi
 
Wabongo wengi wanapenda sana drama.

Kuanzia upinzani mpaka CCM.

Na drama zikipungua, wanaleta za kuzusha.

Za kuzusha zikionekana wazi za uzushi, wanafanya review.

Kabla review haijaisha, zinazuka drama nyingine.

Yani wanaona bila mdundiko wa drama inakuwa nchi hainogi.

Halafu drama zao nyingi maneno matupu, hazina "facts and figures" watu wabishane objectively.

Mara chache sana utaona ripoti ya BOT inajadiliwa katika hizi drama.
 
Magufuli ni binamu mwenye maona, kila jambo linawakati wake, watu wanamsema vibaya ni binadamu wa ajabu Sana, nadhani wameshuhudia, Magufuli alivyo kwenye mioyo ya Watanzania, ni mtu wa vitendo hataki siasa za kulemba ni kiongozi aliyetayari kuwakemea wataule wake bila waoga,Mungu akulinde rais wetu.
 
Huwezi ukapendwa na wote na wala huwezi kuchukiwa na wote jee pigeni tasmi ni watanzania wangapi wamechukizwa na huu utawala wa awamu ya tano
 
Mitandao ya Jamii hasa Twitter na JF zilitawaliwa na habari mbaya juu ya Rais JPM. Watu wengi wamewalaumu sana watoa maoni ambao walikuwa wanamtakia mabaya Mkuu wa Nchi. Hata hivyo kuna matano ya kujifunza na ushauri;

1. Afya ya Rais siyo nzuri, pengine ana mapenzi makubwa ya kuwatumikia Watanzania kwa juhudi na Uzalendo, lakini hajapata mapumziko. Afya yake tumeiona kwenye runinga.

2. Madaktari wanaogopa kumshauri juu ya working hours and over working kutokana na attitude yake ya kutoshaurika.

3. Kuna watu wengi wanampenda na walikuwa wamefadhaika sana wakati mitandao ya jamii ilikuwa inaongea habari mbaya kuhusu yeye.

4. Kuna watu wengi pia wasiompenda kutokana na stahili yake ya uongozi na uamuzi.

5. Mfumo wa mawasiliano wa Ikulu haujui wajibu wake. Labda ulikuwa unataka upate ruksa yake ili utoe taarifa. Je mgonjwa ambaye amepata dharura kubwa anakupaje ruhusa

6. Vyombo vya habari vile vya main-stream vinaogopa kuandika chochote mpaka kwa ruhusa ya Ikulu. Matokeo yake mitandao ya jamii ikabakia ndiyo njia kuu ya habari.

NINI KIFANYIKE:
1. Rais afanye full checkup ya afya yake na apate muda wa kupumzika.

2. Rais ajitathmini style yake uongozi, asifurahie kuogopwa bali ajenge mazingira ya kuheshimiwa

3. Ni vizuri kuna watu wanampenda ila asipuuze sababu za wale wasiompenda. Azifanye kazi na kuchukua hatua.

4. Vyombo vya habari viachwe vifanye kazi zake kitaalamu
 
Ufupi wa akili yako ni pale unapofikiri kila anaye muombea mabaya Rais Maghufuli ni mpinzani na siyo CCM . hebu nikuulize swali , zile clips zilizo wahusisha makambas , kinana , nape nk hao nao ni chadema ? Tumieni kidogo basi hizo akili zenu . anaweza hata akawa ni m CCM mwenzenu alozusha huo uzushi
 
Nilicho jifunza wasiomtakia mema Raisi ni wachache lakini wenye njia mbadala za kuwadanganya wengi ili ionekane kama Tausi anachukiwa na wengi.
Pili ni kwamba ",mafisadi kwa kweli wamebanwa kweli kweli hivyo wanatafuta njia yeyote ile ili wapate kupumua kidogo
 
Tundu Lissu je?!, hata kuvaa fulana tu iliyoandikwa "Pray for Lissu" ilikuwa jinai kubwa ya kupigwa virungu na mabomu ya machozi,. was that right?!
 
hapo umepotoka, binadamu hapaswi kushangilia mabaya ya binadamu mwenzao, sio kiongozi tu.., ila kwa kiongozi anapoona kuna baadhi ya watu wanashangilia inabidi kujiuliza, je wanafanya hivyo kwa chuki binafsi au kuna kitu anachofanya kinawa-marginalize.., kumbuka kiongozi inabidi kuongoza wote wanaokupenda na wasiokupenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…