Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Huo umoja wa kitaifa kuyumba sababu ya tweets za akina Zitto mzee? Yaani kakikundi ambacho tunajua hadi fake IDs zao ndio unasema taifa? Unajua mliheshimika sana kiasi kwamba sasa significant number imeanza kujua motives zenu!
Kwenda zako. kuna watu wapuuzi nchi
hii kama vibaraka wa jiwe? au mmesahau?
 

Somo ni moja tu: IKULU ipo imara!
 
Kwanza nimeungana na Pascal Mayalla kwamba Magufuli anabadilika positively
Lakin tuna somo la kujifunza kwamba pamoja na kwamba hakuwa na ugonjwa wa kutisha na over exagration kwenye reporting imefanyika
Lakin Wanaona kwamba Umoja wa Kitaifa ni Muhimu sana

Cc
Pascal Mayalla

Britannica
 
Chumvi inaweza kuwepo. lakini ukweli ni kwamba afya ya magufuli haiko timamu. Alionekana ni dhaifu.
 
Mkuu;
Una maana gani unaposema walijibebesha gunia la misumali?
Hakuna sehemu ikulu walitangaza kama Rais ana homa au mafua, sasa watu kuanza kushabikia habari ambazo ni za uzushi ambazo zinaweza kukuletea madhara si kujibebesha gunia la misumali. Kesho mtu akitiwa nguvuni utasikia kaonewa, matatizo mengine tunajiftia wenyewe
 
Kuna mengi ya kujifunza
1. Viongozi wa vyama vya upinzani hawana mifumo dhabiti ya intelijensia ambayo ingetoa ukweli kabla kutoa kauli zao.
2. Uzushi kama huu unaadhiri hali ya usalama na mwenendo wa biashara hasa soko la hisa.
3. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ni wepesi kusambaza uzushi bila kutafuta ukweli wa jambo husika. Wengine hupata fursa kueneza mawazo hasi ya kisiasa au kiuchumi.
4. Vyombo vya habari vya ndani na nje havikushadidia uvumi huu.
5. Sheria ya habari na uandishi wa habari imezingatiwa isipokuwa mitandao ya kijamii.
 
Nimejifunza kwamba utamaduni wa Watanzania kumstahi rais na kumuheshimu sana, siyo tu unaisha, bali unaelekea kwenye utamaduni wa ajabu wa kumtakia mtu, tena rais, kifo.

Hii ni tabia mbaya kwa upande wa wananchi wenye mawazo hayo.

Lakini tabia mbaya hii imepaliliwa na kutiliwa mbolea na ubabe wa rais Magufuli.

Watu waliwakejeli Kikwete na Mwinyi kwa udhaifu wao, lakini haikufikia watu wengi hivi kusheherekea uvumi wa kifo cha rais.
 
daah sijaamini yani kuna wananchi walifurah sana raisi wa nchi kuumwa yani kuna wengi sana wasiompenda Jamaa aisee
Mim sitaki kuamini watanzania hawampendi kwa kuangalia watu wanaofurahia taarifa zisizo nzuri kwa afya ya mheshimiwa.Watanzania wako zaidi ya million 55 kuchukulia mihemko ya watanzania wasiozidi hata laki tano wanaofurahia ilo suala si jambo la kusema ndo mwelekeo wa watanzania.
 
We kwa akili zako meco ulomuona akiongea leo ni yule wa kawaida? Hujaona alivyo mpole.
Ukweli ni kuwa anaumwa ila hajafariki. Ila kwa jinsi ilivyoonekana mtandaoni ni kuwa hapendwi kabisaaaaa, hata ajifariji namna gani nguvu ilokuwa mtandaoni inaonyesha waz kuwa hapendwi,
OVER
 
Nafikiria kwamba mimi ndo rais wa nchi ambaye nina majeshi na taasisi mbali mbali ambaye katiba Mbovu inanipa UMungu mtu ndani ya ardh ya watanganyika, nikasikia habari nimezushiwa si za Kufa au habari mbaya tu bali hata kujikwaa kidole kikavuja, alafu niwajue waliosambaza hizo KUNGECHIMBIKA

kumbe saa nyingine rais anapaswa kuwa baba kuwaona wanaomsema kama wanaosema wasilojua,

Urais ni mgumu kwa kakipengele haka

Britannica
 
Kwa tuliokuwa tukijadili afya ya Rais basi mimi ni mmoja wao ninaamini na itakuwa hivyo kuwa Rais hakuwa katika afya yake iliyozoeleka. Na hata ukimuona leo ni bado hakuwa vizuri.

Nimeona video akisalimiana na katibu mkuu kiongozi ndugu Kijazi kwakweli inaonekana kabisa ndugu Kijazi kama ananena mambo fulani hivi. Kwanza inaonekana hawakuwa pamoja kwa muda fulani.

Any way tushukuriwe sisi ambao tuliweza kujiongeza na kuulizia kuhusu afya ya Rais. Tulikuwa na wajibu huo na tutaendelea hivyo kwa kila litakapotokea jambo lisilo la kawaida.
 
Syo muongo kwa 100% ndyo. Au wewe % unaitafsiri vipi.
Huyu jamaa anaumwa.hutaki nenda kalale nae
Mkuu mbona una conclude kwamba Rais ni mgonjwa, umejuaje? Kigogo kadanganya watu hadi kufikia kutaja chumba ambacho ati Mh Rais alilazwa huko Ujeremani! Bado unasema Kigogo siyo muongo kwa 100%!! Ajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…