Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Uongozi mbovu hupelekea taifa kuwa na watu wenye maadili ya ajabu.

Kufurahia kifo cha mtu yeyote, sembuse rais, ni maadili ya ajabu. Maadili duni.

Waliofurahia uvumi wa kifo wamepungukiwa na maadili.

Lakini, wamefikaje huku kwenye kupungukiwa na maadili? Mbona viongozi wetu tuliwaheshimu sana mpaka heshima ikapitiliza?

Ukweli ni kwamba, jamii yetu imepungukiwa na maadili kuanzia chini kwa wananchi mpaka juu kwa viongozi.

Ndiyo maana mtu kama rais Magufuli anakuwa na kauli za ajabu zisizo na maadili.

Na kwa mfumo wetu wa "top down", mtu kama rais Magufuli alikuwa na nafasi kubwa ya kuonesha mfano wa maadili na kuirudisha nchi kwenye mstari, hata kwa kauli zake tu. Hafanyi hivyo. Anatukana tukana ovyo, anaropoka ovyo kwa namna ambayo haimfai rais, anachochea siasa za kugawa watu mafungu kivyama.

Sasa watu wanaona kama huyu rais tunayetakiwa kumuona ni mfano wa maadili anaongea ovyo hivi, basi kuongea ovyo ni ruhusa kwa kika mtu.

Kama mtu kazuia mikutano ya kisaiasa ambayo imeruhusiwa na katiba, wanasema bora afe wapate uhuru wao.

Kwa hiyo kuna tatizo kwa wananchi kukosa maadili, lakini pia kuna tatizo kubwa zaidi kwa viongozi kutoweka kipaumbele kwenye kuonesha mfano wa uongozi wenye maadili.
Umemaliza yote!! Kongole, nitaongeza kidogo;
At least raia wameonyesha kilichopo ndani ya mioyo yao. Mkipuuza na hilo mtakua ni zaidi ya majuha. Ni muda wa kuangalia ni nini kimelifikisha taifa hapa lilipo.
Kujimwambafai haisaidii, the hate is real.
Mdharau mwiba, mguu huota tende.
 
Nimejifunza kwa usalama wa Taifa hawalali, na wanafanya kazi kubwa sana kwa nchi yetu.
Kama wameweza kuwapoteza maboya akina Kigogo
 
Nimejifunza kitu kuwa watanzania wanapenda kitu gani na wanatamani kitu gani kitokee ili furaha yako itimie...!
 
Asante ni ushindi mkubwa kuona Rais wetu ana afya nzuri, sasa kuanzia leo nitaanza kumwombea Rais Magufuri rasmi pale napokumbuka katika sala au maombi
 
  • Thanks
Reactions: nao
Naona mtoa mada ni mpumbavu,rais ni wa watz wote na wala si kosa watz kujua afya yake.
 
Mi mapema tu niliona watu wanajibebesha gunia la misumali
Chadema hawapaswi hata kupata mbunge mmoja! Subiri tu,
Mi nimegundua hali si nzuri inatisha! Nyumbu ni wengi.
Nimejifunza kiongozi huyu hapendwi kabisa na wananchi wake! Walifurahia sana kuwa bora anaewanyanyasa na kujiona mungumtu kaondoka!
Nimejifunza kuwa Iziraeli anajimwambafai anafaa kutumbuliwa
 
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii.

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu!

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!

Pitia hiki nilichosema zaidi ya miaka 2 iliyopita.

Is this Chess or Checkers?
 
Hayo Matango mwitu mtalishwa sana mpaka mpate akili.

Idadi ya nyumbu inaongezeka sana.
 
Tuwe wakwelii tu kuwa kudorora kwa afya ya Rais haukuwa uvumi ; ni kweli Afya iliyumba na ziara kukatishwa ; sio Jambo la Ajabu mwanadamu kuugua
Tatizo ni namna Taifa lilivyopokea katika hali inaonyesha umoja wa kitaifa umekufa

Kimsingi huwezi kusema 100%!kuwa Kigogo ni muongo
Rais ni Mgonjwa na hata leo hakua kwenye ubora wake
Ni bora azingatie muda wa kupumzika

I thought it that way. Unapokuwa mpinzani na agenda ikawa kufa kwa Rais, wewe ndio umekula? Au chama chenu kinawakilisha Gamboshi?
Sisi sote kama binadamu yanayotuzunguka yanafanana. Sijapenda kabisa baadhi ya wana siasa na walivyochukulia haya mambo.
Sisi waumini, Rais ametupa Mwenyezi Mungu. Inakera sana mambo aliyozushiwa
 
Mshana, sky scalet, kigogo mkuje uku 🏃🏃🏃🚴🚴🚀🚀🚶🚶MJOMBA yuko fit .............over
 
Asante ni ushindi mkubwa kuona Rais wetu ana afya nzuri, sasa kuanzia leo nitaanza kumwombea Rais Magufuri rasmi pale napokumbuka katika sala au maombi
Iko wapi afya nzuri pale? WaTanzania kwa kujidanganya??
 
Chadema na ACT vimekuja kuwa vyama vya ovyo haijawahi pata kutokea, vimekua ni vyama vya mihemuko na udaku bila hoja, falsafa au sera za msingi.
Ebu peleka ujinga wako huko kwa wavuta Bangi wenzako, nini kazi ya upinzani? Kazi ya upinzani ni kuikosoa Serikali kwa kila mapungufu yake pasipo kuacha dogo wala kubwa, huwezi kuwapangia eti udaku au mihemuko wao wakosoa kila mapungufu na kama vingekuwa vyama vya hovyo CCM wangeviacha vijifie vyenyewe vipotee, lakini Mbona kutwa kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwahujumu kwa kila hali?
 
Back
Top Bottom