Wadau kuna binti tumefahamiana kupitia mtandao wa kijamii Instagram ,ana miaka 17 yupo kisiwa cha Malta, tulianzisha mahusiano kupitia huo mtandao na hatimaye tukabadilishana namba za sim tukawa tunachat WhatsApp na kupigiana video call
Ni mwanafunzi wa chuo na wazazi wake ni wafanyabiashara
Binti alishanitambulisha kwa Dada yake ambaye yupo UK ni mwandishi wa habari na shangazi yake ambaye wapo naye chuoni na wananitaka niende
Hivi vihela vidogo vidogo binti na shangazi yake huwa wananitumia na nikiwauliza hela wanatoa wapi na wapo chuo wanasema wazazi wao wanawapa pocket money
Na wananipenda hatari
Tumefahamiana kama miezi 5 imepita juzi kanitumia dola 2720 niende kumtembelea nchini kwake kisiwa cha Malta.
Naomba nisaidiwe yafuatayo
Nauli kwenda Malta ni dola ngapi?
Vipi kuna usalama hapo? Na vipi maisha ya Malta yakoje anayejua
Vipi sheria za Malta kudate na miaka 17
Au nimzime hii hela na niblock