Tumepoteza kijana huko Houston, Texas. RIP Humphrey Magwira

Hapa kwetu tatizo upatikanaji wa pesa ni mgumu! Kazi hamna yani inakulazimu ufanye biashara hata kama huna kipaji hiko mambo yanazidi kuwa hobela hobela tu!

Marekani kutengeneza pesa kwa kupitia shughuli rasmi hata kama sio ya ofisini kwenye ac ni rahisi mno ndio maana wengi wanaona bora wakimbilie huko. Imagine unafanya mishe ambayo unalipwa $25 kwa lisaa limoja. Ni equivalent ya 52,000 kwa saa kama utaigeuza hio pesa kwa madafu! Ukifanya hio kazi masaa 10 tu maana utatengeneza 520,000 kwa siku.

Bongo ili uweze kutengeneza hii pesa labda uwe dalali mwenye pete za majini 😅 ama uwe mfanyabiashara wa fast moving goods na kisha uwe na mtaji mkubwa. Yani asilimia kubwa watu wa kipato cha kati hapa bongo wanatengeneza kati ya 10,000-40,000 kwa siku.

Sasa utamfikia mtu wa marekani saa ngapi hata kama anabeba box? Mwenzio kwa siku 10 tu anatengeneza almost 10M ya kibongo. Hata kama kapanga nyumba ya $2000 still atalipa rent na bills zake na chenchi anabakiwa nazo za ku save na kufanya mambo Afrika huku.
 
Mkuu si kweli ni mfanyakazi gani wa kawaida Marekani analipwa USD 25 kwa saa, na ni mji gani wanalipa kiasi hicho, pia tumeona pale yakitokea matatizo ya msiba bakuli linatembezwa hadi Bongo, kungekuwa na pesa nyingi namna hiyo basi bakuli lisngetembezwa, ni wachache wanaoishi huko kwa Biden ambao utasema hata huko Bongo nako wamejiwekeza, muulize Le Mutuz atakuambia vizuri hali ya maisha ya ughaibumi hasa US.
 
Kwa hivyo hamna watu wanaolipwa hivyo mkuu? Tupige ration ya $15 tu kwa masaa 8 ni bei gani!? Almost 35k kwa lisaa ukipiga times 8 ni kama 280K hivi!

Nani anaingiza hio hela kwa siku kwa sie wa mtaani kama sio sadali wa ngada au ndumu labda uwe dalali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…