Tumesahau alichofanywa Dkt. Ulimboka, Mwangosi na Said Kubenea. Nchi hii ni ya kinafiki sana

Tumesahau alichofanywa Dkt. Ulimboka, Mwangosi na Said Kubenea. Nchi hii ni ya kinafiki sana

Na aliyehusika kumteka na kumtesa leo hii ni mbunge. CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.
Mbona sasa hivi unaiunga mkono kupitia Samia?

Na 2025 nasikia unamtupa kapuni Lisu uko na mama
 
Mwangosi aliuawa na askari kwa sababu ya mob psychology tu ya maaskari, huwezi kumtuma askari akaue mtu kwa bomu la machozi.

Ulimboka huyo alipewa kibano kidogo tu cha kumshikisha adabu maana alikuwa anaendesha migomo isiyokoma ya madaktari ya kuparalyse huduma za Afya kwa wananchi, kwanza alipaswa ashitakiwe kwa kusababisha vifo vya watu wengi sana sababu ya kuendesha migomo kinyume cha taaluma ya utabibu

Sasa tuambie hawa wafuatao
Maiti za kwenye viroba
Ben Saananei yuko wapi
Simon Kanguye yuko wapi
Kamanda mawazo vipi?
Aliyempiga risasi tundu Lisu
Aliyemteka Roma mkatoliki
Aliyemteka Mo
Achilia mbali waliokufa kwa presha sababu ya uporaji wa pesa zao
Au waliokufa kwa mshtuko wa moyo kwa kuvunjiwa nyumba zao
Au waliokufa kwa msongo wa mawazo kwa kuporwa korosho zao
Na Dr Sengondo Mvungi je?

Na kubenea na Boss wa GSM na sakata la tindikali je?
 
Na Dr Sengondo Mvungi je?

Na kubenea na Boss wa GSM na sakata la tindikali je?
Huo ni uhalifu kama uhalifu mwingine ni kama vile alivyouawa padri Zanzibar
Uchunguzi wa waliomuua Mvungi ulifanyika, watuhumiwa walipatikana walihukumiwa kunyongwa hadi kufa, sasa niambie lini kulifanyika uchunguzi wa kupotea Ben Saanane au waliompiga risasi Lissu
 
Namkumbuka ulimboka. Aliongoza madaktari wagome watu wasifanyiwe upasuaji wala kutibiwa akaitwa ikulu akagoma raisi akaamua awaachie usalama wa nchi wazungumze nae.
Nakumbuka kulikuwa na mzungu alipewa kazi ya kusimamia menejimenti, Ulimboka akawaongoza madaktari kumtoa ofisini mzungu yule.

Alifanya fujo akisahau kuwa JK alikuwa kashika mpini. Picha yake akiwa amelala kitanda cha hospitali iliwatia huruma watu wengi walioitazama.
 
Mbona sasa hivi unaiunga mkono kupitia Samia?

Na 2025 nasikia unamtupa kapuni Lisu uko na mama
Utakuwa na ukurutu kwenye ubongo wewe si bure.Mimi naunga mkono mambo mazuri anayofanya Samia,akifanya ya ovyo napiga spana. Kamwe siwezi kuiunga mkono CCM.
 
Utakuwa na ukurutu kwenye ubongo wewe si bure.Mimi naunga mkono mambo mazuri anayofanya Samia,akifanya ya ovyo napiga spana. Kamwe siwezi kuiunga mkono CCM.
Basi kwa kuwa Samia anafanya vizuri mi 10 tena kwake!

Alafu uache hasira na kutukana hovyo hiyo ni dalili ya mtu mwenye msongo wa mawazo
 
Nakumbuka kulikuwa na mzungu alipewa kazi ya kusimamia menejimenti, Ulimboka akawaongoza madaktari kumtoa ofisini mzungu yule.

Alifanya fujo akisahau kuwa JK alikuwa kashika mpini. Picha yake akiwa amelala kitanda cha hospitali iliwatia huruma watu wengi walioitazama.
Funzo kubwa lile.
Sipati picha mipango yake ingefanikiwa baada ya muda gani wangegoma tena maana mshahara hautoshagi.
 
Wakukumbukwa na kuenziwa nchi hii ni Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere tu, hao wengine wote wametuingiza kwenye matabaka mabaya kabisa, hebu msikilize kwa makini Chipukizi huyu, he was the only President I can dare to call Hero of the Nation

Nyerere aliitwa Ndugu
Huyu hakumuona Magu, angemuona angemuingiza kwenye kundi la Mwl. Nyerere 🤔!
 
Huyu hakumuona Magu, angemuona angemuingiza kwenye kundi la Mwl. Nyerere 🤔!
Magu hana sifa ya kuingizwa kwenye kundi la akina Nyerere,Kaunda,Mandela Nkwame Nkrumah n.k bali kundi lake ni akina Sabaya,Makonda,Nkurunzinza,Kagame,Mabotu,Idd Amin,Mseveni na wengine wanaofanana na hizo tabia za umimi.
 
Huo ni mtazamo wako! Mtazamo wangu na kwa waliowengi tunajua yupo kwenye kundi la Mwl J. K. Nyerere! Kundi hili halimhusu Mandela, maana yy aliwasaliti wazanzi!
 
Huo ni mtazamo wako! Mtazamo wangu na kwa waliowengi tunajua yupo kwenye kundi la Mwl J. K. Nyerere! Kundi hili halimhusu Mandela, maana yy aliwasaliti wazanzi!
Kwa lipi??? Nyerere kawaunganisha Watanzania,Magufuli kawagawa Watanzania.
 
Basi kwa kuwa Samia anafanya vizuri mi 10 tena kwake!

Alafu uache hasira na kutukana hovyo hiyo ni dalili ya mtu mwenye msongo wa mawazo
Wewe uliyeachwa mjane ndiyo una msongo wa mawazo kwani yule dhalim mumeo anabanikwa kama mshikaki huko jehanam. Sisi huku ni vicheko na bata sana kuondokewa na mtesi wetu
 
Kwa lipi??? Nyerere kawaunganisha Watanzania,Magufuli kawagawa Watanzania.
Kwa mtazamo wa akina Kambona, Mwl. Nyerere aliwagawa watz! Kama ww Kambona wa leo😜! Ni mtazamo hasi wako tu hakuna lolote la maana! Kipindi cha Mwl, hilo kundi lenu la akina Kambona lilikuwa dogo sana, awamu zilizofuata baadaye zimelikuza na sasa na mnamuona Mh. Dr. JPM (may his precious soul rest in eternal peace and power, amen) kuwa mwiba sana kwenu kwa kuvuruga agenda zenu za upigaji😜!
 
Back
Top Bottom