KIJICHO PEVU
Member
- May 4, 2024
- 69
- 49
"Tumeshampata!’ – Yombo Vituka Yamlilia Fulgence Lwiza Kabla ya Kura za CCM"
Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
Kata ya Yombo Vituka, Wilaya ya Temeke, imeingia katika hekaheka za uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku jina la mgombea mmoja likianza kung’ara kabla hata ya kura kupigwa. Ni jina la Mheshimiwa Fulgence Lwiza – mwanachama, mzalendo, na kiongozi anayejijengea heshima kubwa kwa matendo, si maneno.
Katika ziara ya mwandishi wetu aliyefika mitaa ya Machimbo, Mzambarauni, Vituka na Magogoni, alikuta hali ya matumaini na mshikamano isiyo ya kawaida. Wananchi na wajumbe waliokuwa kwenye mikutano midogo ya kijamii walionekana kuzungumza kwa sauti moja: “Fulgence ndiye chaguo letu!”
Wakazi wa Machimbo walimtaja kama kiongozi ambaye amekuwa karibu na jamii kwa miaka mingi. Walisimulia jinsi alivyosaidia ujenzi wa shule mpya ya sekondari ambayo imekuwa msaada kwa wanafunzi wanaomaliza Darasa la Saba katika kata ya Yombo Vituka
Katika Mtaa wa Mzambarauni, kijana mmoja alisema kuwa Fulgence aliwasaidia vijana wa eneo hilo kupata mafunzo ya ujasiriamali. Kwa sasa, baadhi yao wanaendesha biashara ndogondogo na kuweza kujitegemea. Alisema, “Huyu mtu hatusikii kwa vipeperushi, tunamwona kazini.”
Katika Mtaa wa Vituka, mama mmoja alisimama hadharani kwenye mkutano wa Vikoba na kusema kwa hisia kali: “Hatuhitaji kujaribu tena. Tumeshaona alivyotenda kabla ya kuwa kiongozi na baada ya kuwa kiongozi. Tunachotaka sasa ni CCM kutusikiliza.”
Kwa upande wa Mtaa wa Magogoni, msimamizi wa kikundi cha Wanawake na Vijana alieleza kuwa Fulgence alikuja na vifaa vya usafi kwa ajili ya eneo hili bila kutumwa, akijitolea kwa moyo wake mwenyewe kuhakikisha kikundi chetu cha usafi kinapata hivyo vifaa.
Mzambarauni pia kulisikika sauti ya mwanamama mzee aliyesema: “Kuna viongozi wanaahidi wakishachaguliwa. Lakini Fulgence anaahidi kwa vitendo hata kabla ya kura. Huyu si wa kupuuzwa.”
Wajumbe wa CCM kata ya Yombo Vituka pia walionyesha kufurahishwa na mwenendo wa Fulgence Lwiza, wakimtaja kama mtu anayefanya siasa kwa ustaarabu na hoja. Wengine walieleza kuwa amekuwa kielelezo cha mabadiliko ya kisiasa yaliyo na misingi ya huduma kwa jamii.
Huku mchakato wa ndani ya CCM ukisubiriwa kwa hamu, ishara zinaonesha kuwa endapo kura zitazingatia sauti ya wananchi wa Yombo Vituka, basi jina la Fulgence Lwiza lina nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2025 kwa nafasi ya Udiwani.
Kwa wakaazi wa Yombo Vituka, uongozi si heshima, ni huduma. Na kwao, huduma ina sura ya mtu mmoja – Fulgence Lwiza.