Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

SIMULIZI YA ZIARA YA MFALME WA POP DUNIANI MICHAEL JACKSON NCHINI NA ALIPOTEMBELEA SINZA MWAKA 1992

Februari 18, 1992, wananchi wa kitongoji cha Sinza, jijini Dar es Salaam, walipata mgeni ambaye wengi walimzoea kumuona kwenye televisheni: Michael Jackson, Mfalme wa Pop duniani.

Alitembelea shule ya watoto wenye mahitaji maalumu, akafurahi nao na walezi wao, kisha akatoka kuwasalimia wananchi waliofurika hapo kumwona.

Michael aliwasili Tanzania kwa ndege yake binafsi akitokea Ivory Coast, katika ziara iliyopangwa kuhusisha nchi 11 za Afrika akiwa Balozi wa Umoja wa Mataifa. Alipokelewa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, marehemu Hassan Diria, na alikutana na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Akiwa amefikia Hoteli ya Kilimanjaro pamoja na ujumbe wake wa watu 90, alikuwa na matembezi mengine yaliyomwacha mwenyeji mmoja mdomo wazi. Usiku wa manane, Michael alikwenda Empire Cinema, duka la kukodisha mikanda ya video. Hakutosheka kuchungulia dirishani; aliingia ndani, akachagua mikanda kadhaa ya vikatuni na kuondoka.

Muuzaji, kwa mshangao wa kumwona nyota huyo dukani kwake, alisahau hata kudai malipo, kwa butwaa ya kukutana uso kwa uso na Mfalme wa Pop.

Hata hivyo, maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje alioongozana nao, wakiongozwa na aliyekuwa Mkuu wa Itifaki, Cisco Mtiro, walilipa kwa niaba yake.

Februari 19, Michael aliondoka kwenda London, akikatisha ziara badala ya kuelekea Kenya kama ilivyopangwa.
1793508449924.jpg
1793508457821.jpg
1793508443537.jpg
 
Dancer aliyetamba miaka ya 1995s akiwa kama dancer mwenye umri mdogo lakini anakipaji kikubwa kwenye sanaa za jukwaani aliitwa Small Jobiso zaman ila kwa sasa ni Drago J Kunambi . Sasa ana studio iko Mabibo Loyola, anaimba, anatunga, anafundisha dance na anafanya production ( anatengeneza beat na kurekodi - audio record kwa wasanii wanaoimba )

Miaka hio 1990s
Aliweza kupanda jukwaani na wasanii nguli kutoka DRC CONGO 🇨🇩

1. KOFFI OLOMIDE
2. AWILO LONGOMBA
3. GENERAL DEFF DEFAO

Miaka ya 2005
Alikuwa kuongozi wa THT Tanzania house of talents kama mbunifu wa dance na mwalimu.
 
#makinikiayahabari: HEKAYA FUPI YA KARIAKOO: KUTOKA SHAMBA LA MJERUMANI, SHEREHE ZA KAIZARI HADI SOKO KUBWA LA BIASHARA

Kabla ya kuwa kitovu kikubwa cha biashara, Kariakoo ilikuwa sehemu ya mashamba ya minazi yaliyokuwa yakimilikiwa na Sultani wa Zanzibar mwishoni mwa karne ya 19.

Baadaye, mfanyabiashara mmoja Mjerumani aliyejulikana kwa jina la Schoeller alinunua takribani hekta 213 za eneo hilo, akiendesha kilimo na kupangisha sehemu ya ardhi kwa Waafrika. Kufikia mwaka 1913, eneo hilo lilikuwa na wakazi wapatao 15,000.

Mwaka 1914, Serikali ya Kikoloni ya Ujerumani ilinunua ardhi hiyo kwa takribani rupia 500,000 kwa ajili ya kuanzisha makazi yaliyopangwa kwa Waafrika.

Wajerumani walijenga jengo kubwa la chuma katika eneo lilipo soko la sasa. Baadhi ya simulizi za kihistoria zinahusisha eneo hilo na sherehe za kuzaliwa Kaiser Wilhelm II, Mtawala wa Ujerumani.

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, vilivyoanza mwaka 1914, vilikatisha mipango hiyo. Waingereza walipoiteka Dar es Salaam Septemba 1916, walitumia eneo hilo kama ghala la vifaa vya kijeshi vya Carrier Corps, jina ambalo wenyeji walilitamka Kariakoo.

Baadaye eneo hilo likawa soko, lililozinduliwa rasmi Agosti 15, 1923.

Soko la kisasa lililobuniwa na mbunifu Mtanzania Beda Amuli lilijengwa kuanzia mwaka 1971 na kuzinduliwa na Mwalimu Julius Nyerere Desemba 8, 1975 wakati ambapo Dar ilikadiriwa kuwa na wakazi 570,000!

Kwa mujibu wa Makinikia, miaka ya 1970 Dar es Salaam ilikuwa na wakazi wapatao 350,000 mwanzoni mwa muongo huo, idadi iliyoongezeka hadi zaidi ya 750,000 kufikia mwaka 1978. Katika kipindi hicho, Kariakoo ilikuwa tayari imejijengea nafasi kama kitovu muhimu cha biashara, huku jiji likikua kwa kasi kutokana na ongezeko la watu na uhamiaji kutoka mikoani.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, ambayo ndiyo sensa ya mwisho ya kitaifa hadi sasa, Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na wakazi 5,383,728, sawa na watu takribani milioni 5.4.
 
Back
Top Bottom