Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Shah Mohammad Reza Pahlavi wa Iran, mke wake Malkia Farah Pahlavi, na Mfalme Haile Selassie I wa Ethiopia wakati wa sherehe ya miaka 2,500 ya kuanzishwa kwa Dola ya Uajemi (Persian Empire), Oktoba 1971 katika picha ya pamoja.
.
Sherehe hiyo iliandaliwa na Shah wa Iran ili kuadhimisha miaka 2,500 tangu kuanzishwa kwa Dola ya Uajemi na Cyrus the Great.

Ilifanyika katika mji wa kale wa Persepolis na ilihudhuriwa na viongozi wengi wa kifalme na wakuu wa nchi duniani.

Uhusiano wao wa kinasaba

Shah Mohammad Reza Pahlavi
Alikuwa kutoka nasaba ya Pahlavi nchini Iran.
Baba yake, Reza Shah nasaba ya Pahlavi ilianza mwaka 1925 baada ya mapinduzi ya kifalme.

Hivyo ukoo wake haukuwa wa kale sana kifalme, ulikuwa nasaba mpya ikilinganishwa na falme nyingi za zamani.

Malkia Farah Pahlavi
alikuwa mke wa Shah na hakutoka katika familia ya kifalme ya zamani. alizaliwa katika familia ya kawaida Iran.

Baadaye akawa Shahbanu (Malkia wa Iran) baada ya kuolewa na Shah.

Haile Selassie I
Haile Selassie alikuwa kutoka nasaba ya kifalme ya Ethiopia ya Solomonic.

Nasaba hii ilidai kuwa inashuka moja kwa moja kutoka kwa
King Solomon na Makeda
kupitia mwana wao anayeitwa
Menelik I.

Kwa hiyo falme ya Ethiopia ilijiona kuwa na historia ya zaidi ya miaka 3,000.

Je walikuwa ndugu wa damu?
Hapana.

Hakuna ushahidi wa kihistoria kwamba familia ya Mohammad Reza Pahlavi na familia ya Haile Selassie zina uhusiano wa damu.

Uhusiano wao ulikuwa wa kidiplomasia, kifalme.na urafiki wa kisiasa kati ya falme mbili za zamani.

Katika sherehe hiyo ya 1971, viongozi hao wawili walionekana pamoja kwa sababu walikuwa watawala wa monarchies za kale duniani.
 
Chief's toka Tanganyika wakiwa London 1954.

Chief Sabu toka Uluguruni.

Liwali Paul Norbert.

Kaaya wa Meru.

Mollel wa Arusha.

Amri Dodo.
 
Ndege ya shirika la Pan Am aina ya Boeing 377 Stratocruiser miaka ya 1940 ilikuwa ikitoa huduma ya kiwango cha juu kwa abiria wake.

Wateja walikuwa wakifurahia chakula cha kama vile nyama ya kuku au Bata mzinga kamili wa kukaanga, kilichokatwa mbele yao na wahudumu wa ndege.

Huduma ya Pan Am ilikuwa ikijulikana kwa viwango vyake vya juu vya faraja, na ndege kama vile Boeing Stratocruiser zikiwa ndege kubwa maarufu zinazotumika.

Wahudumu wa ndege, ambao wakati huo walijulikana kama 'stewardesses' waliajiriwa kwa kuzingatia muonekano na tabia zao ili kuhudumia abiria.
 
Namjuwa na namkumbuka vizuri huyu mwamba
Sema alikuwa chapachapa sana voltage ⚡️ ilimuondoa

Sema hakuwa mnoko kivile sanaaa

Ova
 
Aliyekuwa mwanadiplomasia wa Ubelgiji, Etienne Davignon mwenye umri wa miaka 93, amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa kumfikisha mahakamani kuhusiana na mauaji ya mwaka 1961 ya kiongozi wa uhuru wa Congo, Patrice Lumumba, wakili wake alisema siku ya Ijumaa.

Akiwa mwanadiplomasia chipukizi wakati huo, Etienne Davignon ndiye pekee aliye bado hai kati ya Wabelgiji 10 wanaotuhumiwa na familia ya kiongozi huyo wa Congo kushiriki katika mauaji yake.

 
TUMETOKA MBALI SANA : Pichani hapo ni fundi wa zamani wa Kandanda wa MECCO YA MBEYA, Abeid Kasabalala, akiwa amesimama mbele ya gari yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…