Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

RAIS IDI AMIN AKIMFARIJI MGONJWA, KAMA BINADAMU WENGINE ALIKUWA NA HURUMA PIA

Idi Amin alikuwa mwiba mkubwa kwa wakoloni wa kigeni waliotaka kudhibiti mali za Uganda kinyume cha sheria.

Alisimama kwa uthabiti dhidi ya unyonyaji wa kikoloni na kuchukua hatua jasiri kulinda uhuru wa Uganda.

Mojawapo ya hatua zake zinazostahili pongezi ilikuwa ni kuwatimua wanajeshi wa kikoloni wenye tabiae za ubaguzi wa rangi kutoka nchini kwake, hatua ambayo ilimpa sifa na pia lawama.

"Jinsi pekee ya kosa lake" ilikuwa ni kuamini kwamba matatizo ya Afrika yanahitaji suluhisho la Kiafrika.

Kama sehemu ya mpango wake wa kuondoa alama za kikoloni nchini Uganda, Amin alianzisha kampeni ya kihistoria ya kubadilisha majina ya maeneo ili kufuta urithi wa kikoloni.

Miongoni mwa mabadiliko makubwa yalikuwa:...,.....

1. Hifadhi ya Taifa ya Queen Elizabeth ikawa Hifadhi ya Taifa ya Rwenzori
2. Maporomoko ya Murchison & Hifadhi ya Taifa ya Murchison yakaitwa Maporomoko ya Kabalega & Hifadhi ya Taifa ya Kabalega (Kwa heshima ya Mfalme wa Bunyoro aliyeipinga Uingereza)
3. Ziwa Albert → Ziwa Mobutu (HESHIMA kwa Rais Mobutu Sese Seko wa Zaire)
4. Ziwa Edward likaitwa Ziwa Amin Dada
5. Ziwa Victoria likarejeshwa jina lake la Kiganda, Nalubaale
6. Harcourt Avenue → Kimathi Avenue (heshima kwa Dedan Kimathi, shujaa wa Kenya)
7. Queen’s Road → Lumumba Avenue ( Patrice Lumumba, kiongozi mkubwa wa Pan-Afrika na kupinga ukoloni)
8. Salisbury Road → Nkrumah Road (Kwame Nkrumah, mtaalamu wa Umoja wa Afrika)
9. Rosebury Road → Nasser Road (Gamal Abdel Nasser, kiongozi wa Misri aliyeipinga ukoloni)
10. Hunter Road → Luthuli Avenue (Kiongozi Albert Luthuli, mpigania haki za watu wa Afrika Kusini)
11. Borup Avenue → Malcolm X Avenue (Malcolm X, mwanamapinduzi shujaa wa Marekani wa asili ya Afrika)
12. Kings Road → Sukarno Road (Dr. Sukarno, rais wa kwanza wa Indonesia na kiongozi wa kupinga ukoloni)
13. Kings Avenue → Nehru Avenue (Pandit Nehru, Waziri Mkuu wa kwanza wa India aliyeipinga Uingereza)
Stanley Road → Akii-Bua Road (John Akii-Bua, mwanariadha wa kwanza wa Uganda aliyeshinda medali ya dhahabu Olimpiki)

Wakati wa kubadilisha jina la Queen’s Road kuwa Lumumba Avenue Januari 18, 1973, Idi Amin alisema..........
"Ni wakati wa kuchunguza nafsi zetu kwa lengo la kurejesha urithi wetu wa kitamaduni, heshima ya binadamu, na heshima, mazingatio ambayo wakoloni walitutetea.

Ili kupigana dhidi ya ukoloni na Zionism, lazima tukumbatie uungwana wa taifa kama kanuni yetu ya msingi."

Aliwaonya Waafrika wasisahau kwamba wakoloni walikuja Afrika kwa maslahi yao binafsi, si ya Waafrika.

Amin pia alitaka kubadilisha jina la Mlima Elgon kuwa Mlima Masaba na alipendekeza jina jipya la Ziwa Victoria, huku akisubiri makubaliano na Kenya na Tanzania.

Ingawa jina la ziwa halikubadilishwa kwa sababu za kiufundi, Mlima Elgon baadaye ulipatiwa rasmi jina la Mlima Masaba kwa idhini ya Kenya.

"Kubadilisha majina ya barabara, hifadhi za taifa, na milima ni mwanzo tu wa kampeni kubwa ya kuondoa majina ya kikoloni na ukoloni kote Uganda.

Ninawahimiza mamlaka zote za mijini na za mitaa kubadilisha majina yasiyo na maana ya kigeni na kuyachukua ya Kiafrika yenye maana."

Baada ya amri hii, barabara za Uganda pia zilipewa majina ya viongozi wa ndani, kama Barabara ya Karegyesa katika Wilaya ya Rukungiri na Barabara za Nadiope, Luba, na Gabula katika Wilaya ya Jinja.

Kwa bahati mbaya, baada ya kuanguka kwa Amin mwaka 1979, majina mengi ya kikoloni yalirejeshwa, kitendo kilichorudisha nyuma maendeleo ya kweli ya kuondoa ukoloni nchini Uganda.

Amin Idi Amani Aendelee Kutulia kwa Haki.
Urithi wake, licha ya migongano yake, unabaki ushuhuda wa upinzani wa Afrika dhidi ya ukoloni.
FB_IMG_1775524736359.jpg
 
Picha za kihistoria za Zanzibar : Kwaride la Wanamaji wa India likipita mitaani kwenye Mji Mkongwe , wakati wa ziara yao katika miaka ya 1950s ( Picha kwa hisani kubwa ya @Bw. Taria )
1775725584622.jpg
 
JULIUS KAMBARAGE NYERERE AHUKUMIWA kwa "KASHIFA" dhidi ya MaDC Wawili wa Kikoloni 1958.
‎
‎Tarehe 13 Agosti 1958 ilikua ni siku ya kukumbukwa katika historia ya TANU. Siku ambayo Nyerere alihukumiwa kwa Mashitaka mawili mazito ya kuwaita watawala "Washenzi na Maharamia"

‎Chama Cha TANU kilichukua tahadhali kubwa kuwaandaa watu wasije wakafanya Ghasia. hata kama Hukumu hiyo itakuwa kufungwa, Chama kilifahamu kwamba kitendo chochote cha Ghasia kufuatia uamuzi wa kesi hiyo, kingeweza kutumiwa na Maadui kuikandamiza TANU.
‎
‎Maelfu ya Wananchi hasa akina Mama wakiongozwa na Bibi Titi Mohamedi Mwanasiasa maarufu wa wakati huo na kiongozi shupavu wa akina Mama walijaa ufukweni wengine wakiwa watoto kungojea jambo litakalo mpata kiongozi wao.
‎
‎Dakika chache kabla ya Mahakama kuanza Nyerere akiandamana na Hayati John Rupia Makamu wa TANU wa wakati huo waliwasili Mahakamani. Pritt alikwisharuka kurejea London Uingereza.
‎
‎Polisi wengi walikuwepo Mahakama ya Hakimu Mkazi maeneo ya Bara bara ya kivukoni Front yalizingirwa na Askari hao, ambao inasemekana kwamba ilibidi baadhi yao waletwe kutoka Majimbo jirani kungojea pengine kungezuka Ghasia.
‎
‎Nyerere aliingia Kizimbani kama kawaida kusikiliza Hukumu yake katika kesi ya kwanza ya aina yake katika Tanganyika.
‎
‎Hakimu Davies akitoa Hukumu yake alisema;
‎
‎"Katika Kesi hii Nyerere mwenyewe alikiri alipiga chapa maneno hayo ya Kashifa dhidi ya DC Scott katika Sauti ya TANU Na. 29 ya Tarehe 27 mei 1958.
‎
‎Davies aliendelea kusema kuwa kwa kuchapisha habari hizo Gazeti la Standard halikua na nia ya kuidhuru Mahakama.
‎
‎"Lakini nikiri hapa kwamba kitendo hicho Kwakweli kiliathiri kwa kiwango fulani maendeleo ya kesi hii"
‎
‎Ushahidi wa Hasani Nila uliyumba sana ulikua hauaminiki. Na ni Shahidi huyo tu ambaye alitoa ushahidi dhidi ya Scott kwa upande wa Utetezi. Kwa Upande mwingine upande wa utetezi, ulikiri kwamba maneno hayo ya Kashifa kuhusu Scott yalichapishwa na Nyerere na kutawanywa kwa idhini ya Nyerere mwenyewe.
‎
‎Kama Kiongozi wa Chama cha Umma Nyerere alikua nazo sababu za kuandika habari hizo ambazo alitaka Serikali ifahamu hususani matatizo yaliyojitokeza Kusini mwa Tanganyika.
‎
‎Lakini zilitawanywa isivyostahili Nakala za TANU kwa watu binafsi ambao baadhi yao hawastahili kuzipata wala kuhusika na mambo hayo.
‎
‎Ingawaje Pritt alishikilia hapa Mahakamani kuwa Nyerere kwa kuandika na kutawanya habari hizo alifanya kwa nia njema, Lakini ni lazima niseme hapa Nyerere hawezi kulindwa na Sheria chini ya mwamvuli wa kichwa hicho cha maneno.
‎
‎Hakimu alitamka Nyerere hakuwa na haki kisheria kwa njia yoyote Ile wala kuwajibika kijamii, alipoamua kuandika maneno hayo ya kashfa dhidi ya Scott. Nyerere alikiri katika ushahidi wake kwamba alifahamu Scott hakufunga Tawi la TANU. Lakini alikua akitekeleza Sheria alipokataa kuliandikisha Tawi la hilo la TANU kwahiyo Nyerere hakufanya hivyo kwa nia njema isipokua aliandika maneno hayo ya kashfa hadharani.
‎
‎Haukutolewa ushahidi wowote mbele yangu kuthibitisha Nyerere alichukua jukumu lolote kupeleleza Madai dhidi ya Scott. Nyerere alikiri katika ushahidi wake kwamba alifahamu kuwa Scott alikataa kuliandikisha Tawi hilo la TANU.Kwahiyo aliandika maneno hayo ya Kashifa kwa sababu ambazo anazifahamu mwenyewe.
‎
‎Siwezi kuridhika kabisa ikizingatiwa kwamba hakuwa na upendeleo wa aina yoyote kuandika maneno yake.

‎Hakimu alimaliza kusoma Hukumu yake na akasema Nyerere ana hatia kama alivyo shitakiwa.
‎
‎Hakimu Davies akitoa Hukumu yake alisema amegundua kwamba Nyerere ni Mtu mwenye Busala nyingi ni mtu mwajibikaji katika Jamii
‎
‎"Halikua jambo la kawaida kutoa adhabu ya kifungo kwa Makosa kama hayo, Na Mimi sitaki kujitenga na desturi hiyo, namtoza Mshitakiwa Faini ya Sh. 3,000/= au kwenda Jela Miezi Sita. Nampa Mshitakiwa muda wa siku mbili kulipa Faini hiyo.
‎
‎Baada ya Hukumu hiyo kutolewa, Nyimbo na Nderemo ziliikumba Mahakama ya Hakimu Mkazi. Kina Mama ambao wengi walikua wamezoea kuzingira jengo hilo kufuatilia kesi hiyo, Walishangilia kwa msisimko na Nderemo wakiongozwa na Bibi Titi Mohamedi.
‎Baada ya kupeana mikono na Mawakili wake, Nyerere aliingia katika Gari kurejea Nyumbani akifuatana na Makamu wa Rais wa wakati huo, Hayati John Rupia na Viongozi wengine wa Chama.
‎
‎Huu ukawa Ndio mwisho wa kesi hiyo ambayo kama Hukumu yake ingekua kifungo Moja kwa moja huenda ingeanzisha Machafuko makubwa kubadili historia ya Siasa ya Nchi hii.
1775969909276.jpg
 
London.

Mkoloni ana njia nyingi za kuwaweka katika mstari ulionyoka.

Machief wa Tanganyika ziarani Uingereza 1951.View attachment 3534951
Tanganyika haikuwa koloni la mwingereza, mwingereza alikuwa "baby sitter" kazi aliyopewa na Legue Of Nations(United Nations Organization ) UN hivi sasa. Chini ya jukumu hilo usimamizi wake ulitakiwa ukome Watanganyika watakapo elimika na kuonekana wanao uwezo wa kujiongoza na kuidhinishwa na UNO, hiyo ndiyo sababu ya Mwalimu Nyerere kwenda UNO kujieleza ili tukabidhiwe nchi.
 
Tanganyika haikuwa koloni la mwingeza, mwingereza alikuwa "baby sitter" kazi aliyopewa na Legue Of Nations(United Nations Organization ) UN hivi sasa. Chini ya jukumu hilo usimamizi wake ulitakiwa ukome Watanganyika watakapo elimika na kuonekana wanao uwezo wa kujiongoza na kuidhinishwa na UNO, hiyo ndiyo sababu ya Mwalimu Nyerere kwenda UNO kujieleza ili tukabidhiwe nchi.
Shukrani kwa ufafanuzi mkuu💪🏿
 
Idi Amin na mke wake wa kwanza, Mariam Amin, ambaye alimuoa mwaka 1962. Amin alimpa talaka Mariam mwaka 1974 na akaagiza akamatwe katika mpaka wa Kenya na Uganda eneo la Tororo kwa tuhuma za magendo.
Jina lake halisi lilikuwa Sarah Mutesi Kibedi, lakini baadaye alichukua jina la Malyamu (au Mariam) baada ya kusilimu na kuwa Mwislamu. Alitoka katika familia mashuhuri ya Busoga, na kaka yake, Joshua Wanume Kibedi, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya Amin.
Mariam aligundua tabia ya Amin ya kutokuwa mwaminifu, hasa uhusiano wake na Kay Adroa, na alishuhudia jinsi Amin alivyoendelea kuongeza wake wengine kwa haraka.
Mwaka 1974, alikamatwa Tororo karibu na mpaka wa Kenya kwa madai ya kufanya magendo, lakini baadaye alikimbilia nchini United Kingdom kwa msaada wa Makamu wa Rais wa Kenya wa wakati huo, Daniel arap Moi.
Alifariki mjini London mwaka 2015.
1777002285832.jpg
 
Wavulana Waafrika-Wamarekani wakiwa asubuhi ya Easter katika eneo la Southside, Chicago, jimbo la Illinois, mwezi Aprili mwaka 1941. Picha hiyo ilipigwa na mpiga picha Russell Lee.
Kati ya wavulana watano waliopo kwenye picha hiyo, aliyefahamika rasmi ni kijana mrefu asiyevaa kofia aliyesimama katikati, aitwaye Spencer Lee Readus Jr., ambaye alikuwa na umri wa miaka 14 wakati picha ilipopigwa.
Baadaye, Spencer Lee alienda kuhudumu katika Jeshi la Marekani wakati wa World War II na kujenga kazi kama msimamizi wa kazi za plasta.
Kwa mujibu wa binti yake, alikumbuka siku hiyo akisema: “Nilikuwa naenda kuangalia sinema siku ya Pasaka, na mwanaume mzungu alinifuata kuniuliza kama angeweza kunipiga picha mimi na hawa wavulana wengine.”
1777004289552.jpg
 
TUMETOKA MBALI SANA: Wakongwe hao wa soka la TANZANIA wakutanapo huwa ni furaha tu, Pichani hapo ni Twaha Hamidu "Noriega" aliyevaa (T-shirt) na Iddi Pazi "Father" aliyevaa (Shirt ).
1777018262733.jpg
 
Back
Top Bottom