Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

MAJI MAJI YA SONGEA : JUU (KUSHOTO) NI Golikipa Shaibu Kambangwa, David Mjanja, Omar Kapilima, Godfrey Kikumbizi, James Mhagama, Steven Mapunda "Garrincha" John Alex Lwena, Kelvin Haule (RIP) na Golikipa Doyi Moke (RIP). . . CHINI (KUSHOTO) NI Fortunatus Dello Ntumba, Omar Hussein, Willy Martin, Said Mshamu, Samson Paul, Hamisi Ngwena na Amri Said "Stam"
1779966789649.jpg
 
MAJI MAJI YA SONGEA : JUU (KUSHOTO) NI Golikipa Shaibu Kambangwa, David Mjanja, Omar Kapilima, Godfrey Kikumbizi, James Mhagama, Steven Mapunda "Garrincha" John Alex Lwena, Kelvin Haule (RIP) na Golikipa Doyi Moke (RIP). . . CHINI (KUSHOTO) NI Fortunatus Dello Ntumba, Omar Hussein, Willy Martin, Said Mshamu, Samson Paul, Hamisi Ngwena na Amri Said "Stam"View attachment 3596337
 
Udongo mwekunduu
 
Wengi wetu tunalijua hili duka wakati linaitwa Tanzania Elimu Supplies.Lilikuwa katikati ya iliyokuwa Salamander hotel na Posta ya zamani.

Duka lilikuwa kubwa la stationery na wenyewe walikuwa the Kanti brothers.

Ghafla katika miaka ya sitini hawa ndugu na familia zao walipewa masaa 48 waondoke nchini.

Sababu zilizozagaa mtaani ni kwamba wakishirikiana na ubalozi fulani walikuwa wanaingiza bidhaa bila kulipa kodi.

Sababu ingine ambayo ilishika kasi

Kawawa aliingia kwenye hili duka akitaka kununua pen aina ya Parker ambayo ni expensive.Kukatokea mzozo haijulikani kama Kawawa alitaka kuichukua bure au wenye duka walileta dharau.

Kilichofuata wahindi waliwekwa ndani na kesho yake na familia zao wakapakiwa kwenye ndege kuelekea Uingereza.

Duka likawa la umma Tanzania Elimu Supplies.
1780681368526.jpg
 
Duka likawa la umma Tanzania Elimu Supplies.View attachment 3601850
Duh ni zamani sana miaka ya 60🙌
 
KWA NINI TUZIKE HISTORIA YA TANGANYIKA?

Baada ya kuanzishwa TANU, Rais wa TANU wa wakati huo, Julius Nyerere alizunguka katika eneo lote la Tanganyika kuwaomba watawala wa maeneo mbalimbali wajiunge na Shirikisho la Tanganyika. Unajua kwa nini Nyerere alifanya hivyo?

Eneo lote la Tanganyika lilikuwa ni nchi moja chini ya Wajerumani. Ila baada ya Wajerumani kushindwa na Waingereza katika Vita Kuu ya I ya Dunia mwaka 1919, eneo lote hili liliwekwa chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa kwa masharti kwamba Watanganyika watakapofika wakati wa kujitawala wapewa nchi yao. Hivyo, Uingereza ilipewa kuwa mwangalizi tu.

Hivyo masharti ya kupata uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni lazima uwe uhuru wa nchi moja kwa taifa zima la Tanganyika. Ndio sababu Mangi Marealle wa Moshi alipokwenda kule Umoja wa kudai Uhuru wa Wachagga (Kilimanjaro) pekee alikataliwa pamoja na ukweli kuwa Kilimanjaro ilikuwa na sifa zote za kuwa nchi inayojitawala.

Lakini pia, kama baadhi ya maeneo yangekataa na kusema kuwa hayakuwa tayari kwa uhuru, Uingereza isingetoa uhuru kwa Tanganyika. Hii ndio sababu iliyomfanya Julius Nyerere kupita kila eneo kushawishi machifu (watawala wa makabila) mbalimbali kuweka mamlaka yao kwa TANU. Ndio maana baada ya uhuru watoto wengi wa machifu walipewa nafasi serikalini kwa sababu ilikuwa sehemu ya makubaliano kati ya Nyerere (TANU) na baba zao ya kuwa watoto wao watapewa uchifu katika maeneo mengine.

Milki (tawala) zote mbili za Chifu Mwamakula, Utawala wa Mwaya chini ya Chifu Mwakalukwa Mwamakula na Utawala wa Kajunjemele chini ya Chifu Korosso Mwamakula tulitoa mamlaka yetu kwa TANU chini ya Rais Julius Nyerere.
Nyerere alichukua sahihi za machifu wote na kuziwasilisha kwa watawala wa Kiingereza na pia Umoja wa Mataifa kuwa Watanganyika kwa umoja wao wako tayari kujitawala. Hiyo ndiyo njia iliyotumika kudai Uhuru wa Tanganyika bila ya kumwaga damu kama Kenya na kwingineko.

Leo nilikuwa naangalia sarafu tatu za shilingi ya Tanzania: sarafu ya shilingi mia moja, sarafu ya shilingi mia mbili na pia sarafu ya shilingi mia tano. Nilibaini kuwa sarafu hizo kuna iliyo na picha ya Julius Nyerere na pia kuna iliyo na picha ya Sheikh Abeid Amani Karume.

Kilichonishangaza ni kuwa Julius Nyerere yeye kuelezwa kuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania wakati Karume kaelezwa kuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar. Historia yetu imefukiwa chini ya ardhi mchana kweupe. Sijajua unyama huo wa kuifukia na kuizika historia yetu ulifanywa kwa makusudi au ilikuwa ni 'umbumbumbu' wetu.

Kwa sababu ya kufukiwa kwa historia hiyo, leo kuna watu wananyanyapaliwa kwa wao kutaja majina ya Tanganyika na Zanzibar. Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza kaelezea katika ukurasa wake jinsi alivyotukanwa kwa kutumia historia hiyo.

Lakini pia ni makosa makubwa kuufuta kabisa utambulisho na historia ya nchi iliyo kwenye muungano au shirikisho. Historia inaonyesha kuwa mashirikisho mengi duniani zikiwemo nchi za muungano viliparaganyika na watu wa nchi zilizokuwa katika muungano, mashirikisho au umoja wakarudia mipaka yao na pia historia zao. Mifano hiyo ni kama Muungano wa Nchi za Kisovieti (USSR au Urusi), Muungano wa Nchi za Yugoslavia, Muungano wa Nchi za Sudan, Muungano wa Nchi Ethiopia, nk.

Wakati muungano wa nchi za Yugoslavia ukiwa katika hali kusambaratika kulitokea mapigano makali sana kwa sababu maeneo mengine pia yalikuwa na utata wa kihistoria na mipaka. Ni vizuri historia ya Tanganyika isiharibiwe, lakini pia ni vizuri historia na mipaka ya nchi ambazo ziliunda shirikisho la Tanganyika visiharibiwe.

Lakini pia, wakati Uganda walipoandika katiba yao kwa upya na kuitambua mipaka ya asili na tawala za asili, haukuwa shida kutambua pia mipaka ya tawala za Baganda, Banyoro, nk. Muungano ulio imara ni ule ambao kila mmoja anajua asili na historia yake. Lakini leo sehemu moja ya huu Muungano wa Tanzania hawaijui kabisa historia yao wakati sehemu nyingine wanaijua na wanafufua kila kitu cha kwao!

Kuyanyamazia haya ni kuahirisha matatizo ili kuyaacha yawe makubwa zaidi. Mzazi mwema na aliye na hekima ni yule anayehakikisha ya kuwa matatizo ya wakati wake anayatatua yote ili asiwarishishe watoto wake matatizo yake.

Leo tumefika mahali viongozi kutoka upande mmoja wa Muungano wanaongea hadharani kuwa ajira zote zilizo katika upande wa nchi yao ziwe kwa ajili wazawa wa sehemu ile tu wakati ajira za upande mwingine hutolewa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi. Wakati upande mmoja wa Muungano wanajuana hadi kifamilia lakini upande mwingine wanaijua historia ya Chifu Mkwawa wa Wahehe, Mtemi Mirambo wa Tabora na Kinjikitile Ngware wa Ngarambe tu.

Historia nyingine za tawala zetu zimefukiwa kiasi kwamba watoto wetu wakiambiwa juu watemi na machifu wa Tanganyika wanafikiri kuwa unawaambia kuhusu waganga wa jadi, wachawi, wapiga ramli na waaguzi. Wenzetu huko Ulaya wametunza historia za watawala wao wa tangu kabla ya Yesu, lakini sisi huku tunaifukia historia ya miaka 60 iliyopita. Je, huu ni ustaarabu gani wa kuua historia? Lakini huu ni uongozi gani wa kufukia misingi ya historia iliyounda nchi yetu?

Lakini kulikuwa na dhambi gani kuweka sarafu moja itaje Rais wa Kwanza wa Tanganyika? Na huo si ndio ukweli wenyewe? Tunamdanganya nani kwa maslahi ya nani? Je, tunamridhisha nani kwa maslahi ya nani hasa? Kuyafumbia masuala madogo haya kunajenga hisia, chuki na wivu wa vuguvugu la kujikomboa upande ambao unaona kuwa historia yake inafukiwa na vuguvugu hilo linaweza kuwa na athari mbaya sana kwa muungano wetu. Kile kitu ambacho tunafikiri tunakilinda, tutajikuta tunakibomoa kwa mikono yetu wetu kama yule mwanamke mpumbavu wa kwenye Biblia (Mithali 14:1).
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 9 Juni 2026; Saa 8:00 usiku wa manane
1781017524259.jpg
 
Itunge, Dar es Salaam; 9 Juni 2026; Saa 8:00 usiku wa mananeView attachment 3604458

Shukrani sana kaka mshana kwa kuendelea kutukumbusha.
 
Pauline Lundokisi, mjane wa mwanamuziki nguli Pépé Kallé, aliaga dunia Jumamosi, Februari 23, 2019 huko Kinshasa, karibu miaka 20 baada ya kifo cha mumewe.

Hakuwahi kuolewa tena baada ya kifo cha Pépé Kallé. Katika mahojiano mbalimbali ya vyombo vya habari, kila mara alithibitisha upendo wake usioyumba na uaminifu kwake, akisema:
"Siwezi kuolewa tena, kwa heshima na heshima kwa marehemu mume wangu Pépé Kallé. Siwezi kufanya kosa kama hilo na kumkatisha tamaa mtu aliyenifanya kuwa hivi leo. Ikiwa ninaheshimiwa kila mahali nchini na duniani kote, ni shukrani kwake."

Hiyo ilikuwa wakati wa programu iliyoandaliwa kuadhimisha miaka 20 tangu kifo cha mume wake.
Roho yake ipumzike kwa amani.

Maman Pauline alikuwa mwanamke mzuri ambaye daima alidumisha uhusiano bora na wazee wa Empire Bakuba, wanamuziki wengine wa Kongo, na familia ya marehemu mumewe. Alikuwepo mara kwa mara kwenye mazishi na sherehe za heshima kwa wasanii wenzake.

Pépé Kallé (Kabasele Yampanya) aliaga dunia mnamo Novemba 28, 1998. Mnamo 2019, alikuwa ameondoka kwa miaka 20 haswa. Aliwaacha watoto kadhaa, akiwemo Mamy Mbula, ambaye alimtoa katika moja ya nyimbo zake maarufu.
Aliyezaliwa Machi 30, 1957, Marehemu Pauline Kabasele Lundokisi ameacha watoto watatu. Maombolezo hayo yalifanyika katika makazi ya familia hiyo eneo la Adoula, wilaya ya Bandalungwa.
Wimbo "Lundokisi" wa Papy Tex na Empire Bakuba uliwekwa wakfu kwake.

Wapumzike kwa amani ya milele wote wawili
1781429582444.jpg
 
Wakati hapakuwa na E-mail:
Salim Ahmed Salim ni Mtanzania pekee aliyekuwa anaandikiana Barua na Marais wa USA. Yeye na George Bush Sr walikuwa marafiki. Kwenye barua hii Utaona Bush akiwa Makamu wa Rais anamwambia Salim kama kuna kitu chochote anachotaka awasaidie watoto wa Salim wanaosoma USA amuambie.
Tumetoka mbali!
1781441853154.jpg
 
Imekuwa wiki mbaya zaidi kwa Sekta ya Anga Ulimwenguni kufuatia msururu wa ajali mbaya za ndege 03 zilizogharimu vifo vya watu 23 zilizotokea nchini Brazil, Marekani na India mwishoni mwa wiki hii.

𝗠𝘂𝗵𝘁𝗮𝘀𝗮𝗿𝗶 𝘄𝗮 𝗠𝗮𝘁𝘂𝗸𝗶𝗼:

𝗥𝗶𝗼 𝗱𝗲 𝗝𝗮𝗻𝗲𝗶𝗿𝗼, 𝗕𝗿𝗮𝘇𝗶𝗹
Helikopta mbili ziligongana angani asubuhi ya Jumapili. Watu wote 6 waliokuwa ndani walifariki, na mabaki ya ndege yaliwaka moto kwenye duka la magari.

𝗠𝗶𝘀𝘀𝗼𝘂𝗿𝗶, 𝗠𝗮𝗿𝗲𝗸𝗮𝗻𝗶:
Ndege ya kubeba wamichezo wa kuruka na miamvuli (skydiving) ilianguka na kuwaka moto muda mfupi baada ya kupaa.
Watu wote 12 waliokuwa ndani walipoteza maisha.

𝗔𝘀𝘀𝗮𝗺, 𝗜𝗻𝗱𝗶𝗮
Ndege ya kijeshi ya usafirishaji ilianguka wakati ikijaribu kutua.
Maafisa 5 wa jeshi la anga walifariki, huku rubani msaidizi mmoja akiokolewa akiwa hai.

View: https://www.facebook.com/share/v/1CqgCwQffA/
 
𝗔𝗗𝗗𝗜𝗦 𝗔𝗕𝗔𝗕𝗔 - Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu nchini Ethiopia unaoratibiwa na Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) unaendelea kwa kasi kubwa ya utarayarishaji wa ardhi ya ujenzi.

Usanifu wa uwanja huo mkubwa unaongozwa na kampuni maarufu ya Zaha Hadid Architects.

Mradi huo uliozinduliwa rasmi mwezi Januari 2026 haujakabidhiwa mkandarasi mmoja wa jumla, na badala yake, Ethiopian Airlines inatekeleza mradi huu kwa awamu, ikitumia mfumo ambapo ujenzi unaogawanywa katika mikataba na makampuni tofauti ili kuhakikisha ubora.

Mradi huo unaogharimu shirika hilo la ndege dola bilioni 12.5 unalenga kuifanya Ethiopia kuwa kitovu kikuu cha usafiri wa anga barani Afrika, ukichukua nafasi ya Uwanja wa Bole unaokabiliwa na msongamano.

Awamu ya kwanza itakamilika mwaka 2030 na kuhudumia abiria milioni 60 kwa mwaka, huku mradi mzima utakapokamilika ukitarajiwa kuhudumia abiria milioni 110.

Eneo la Bishoftu liko chini kwa mita 400 kulinganisha na Addis Ababa, hali inayoruhusu ndege kubwa kupaa kwa urahisi na kutumia mafuta kidogo kutokana na uzito wa hewa (High density)

Uwanja huo uliobuniwa na kampuni ya Zaha Hadid Architects utakuwa na barabara nne za kupaa, sehemu ya ndege 270, na mji wa uwanja wa ndege utakaounganishwa na reli ya mwendo kasi.

Shirika la Ndege la Ethiopia linagharimia asilimia 30 ya mradi huo, huku asilimia 70 ikitokana na mikopo ya kimataifa inayoratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
1781540506139.jpg
 
Back
Top Bottom