Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

1781598841000.jpg
 
Rais wa Msumbiji Samora Machel anakaribishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum na Rais wa Sudan Gaafar Mohamed Nimeiry mnamo Julai 19, 1978, kabla ya Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika.
Rais wa Msumbiji Samora Machel anakaribishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum na Rais wa Sudan Gaafar Mohamed Nimeiry mnamo Julai 19, 1978, kabla ya Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika.
1784219954120.jpg
 
Kumbukizi mwaka 2009 Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Marehemu Willium Lukuvi akiwa na RPC wa Dsm alivyokutana na Dereva Tax jijini humo wakati wa ukaguzi wa Taxi ambazo zilikuwa hazijasajiliwa.

1784271835571.jpg
 
Sasa amekuwaje mmanyema tena??
FARID ATRASH (1910 - 1974)
Wangapi wanaonisoma hapa wamepata kumjua Farid Atrash?

Farid Atrash alikuwa muimbaji maarufu, Misri na pia muigizaji senema katika miaka ya 1950.

Naamini hapa watakuwa watu wachache sana waliopata kusikia jina hili lakini katika Dar es Salaam tuliokulia baadhi yetu Farid Atrash alikuwa akifahamika na nyimbo zake zilikuwa maarufu na zikipigwa katika radio.

Halikadhalika miaka hiyo maduka mengi mitaani ilikuwa ya Waarabu na radio zao muda wote wakitegesha Sauti ya Cairo na nyimbo zilizokuwa zikipigwa na za waimbaji maarufu wa Kiarabu mfano wa Farid Atrash, Um Kulthum kwa kuwataja wachache.

Katika kitabu cha Abdulwahid Sykes nimeandika maneno haya mwanzo wa kitabu nikimweleza baba yangu na rafiki zake wa nyakati zile miaka ya 1950, nimesema, ''Wakati mwingine waliwasikiliza waimbaji wa Kiarabu, Um Kulthum, Mohammed Abdulwahab, Farid Atrash, Abdul Halim Hafidh, Feruz na Sabah.''

Leo katika msikiti wetu wa mtaani, Masjid Noor, Magomeni Mapipa baada ya Swala ya Adhuhur nakwenda kuchukua viatu vyangu nje ya msikiti akanikabili bwana mmoja na akaniita kwa jina na kunitolea salamu.

Nimeitika salamu nimempa mkono nikamuuliza, ''Iweje wewe unanijua mimi sikufahamu?

Hapo ndipo mazungumzo yakaanza.

Akanitajia jina lake kuwa ni ''Farid Atrash,'' kabila Mmanyema.

Nikamuuliza, ''Farid Atrash yule muimbaji?''

Akanijibu kuwa ndiye.

Akaingiza mkono katika kanzu yake nyeupe nadhifu na kunionyesha kitambulisho chake.

Kitambulisho kimeandikwa, ''Farid Atrash.''

Huyu ndugu yangu akanieleza kuwa yeye amekuwa akifuatilia sana vipindi vyangu mitandaoni.

Tukazungumza kiasi cha kuzungumza na tukapeana simu zetu.

Hili jina lake kwa hakika limenishangaza sana.

Mfano wa kukutana na mtu akakuambia kuwa yeye jina lake ni ''Michael Jackson.''

Huyo hapo chini mwenye jina lake:
 
Back
Top Bottom