Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

FARID ATRASH (1910 - 1974)
Wangapi wanaonisoma hapa wamepata kumjua Farid Atrash?

Farid Atrash alikuwa muimbaji maarufu, Misri na pia muigizaji senema katika miaka ya 1950.

Naamini hapa watakuwa watu wachache sana waliopata kusikia jina hili lakini katika Dar es Salaam tuliokulia baadhi yetu Farid Atrash alikuwa akifahamika na nyimbo zake zilikuwa maarufu na zikipigwa katika radio.

Halikadhalika miaka hiyo maduka mengi mitaani ilikuwa ya Waarabu na radio zao muda wote wakitegesha Sauti ya Cairo na nyimbo zilizokuwa zikipigwa na za waimbaji maarufu wa Kiarabu mfano wa Farid Atrash, Um Kulthum kwa kuwataja wachache.

Katika kitabu cha Abdulwahid Sykes nimeandika maneno haya mwanzo wa kitabu nikimweleza baba yangu na rafiki zake wa nyakati zile miaka ya 1950, nimesema, ''Wakati mwingine waliwasikiliza waimbaji wa Kiarabu, Um Kulthum, Mohammed Abdulwahab, Farid Atrash, Abdul Halim Hafidh, Feruz na Sabah.''

Leo katika msikiti wetu wa mtaani, Masjid Noor, Magomeni Mapipa baada ya Swala ya Adhuhur nakwenda kuchukua viatu vyangu nje ya msikiti akanikabili bwana mmoja na akaniita kwa jina na kunitolea salamu.

Nimeitika salamu nimempa mkono nikamuuliza, ''Iweje wewe unanijua mimi sikufahamu?

Hapo ndipo mazungumzo yakaanza.

Akanitajia jina lake kuwa ni ''Farid Atrash,'' kabila Mmanyema.

Nikamuuliza, ''Farid Atrash yule muimbaji?''

Akanijibu kuwa ndiye.

Akaingiza mkono katika kanzu yake nyeupe nadhifu na kunionyesha kitambulisho chake.

Kitambulisho kimeandikwa, ''Farid Atrash.''

Huyu ndugu yangu akanieleza kuwa yeye amekuwa akifuatilia sana vipindi vyangu mitandaoni.

Tukazungumza kiasi cha kuzungumza na tukapeana simu zetu.

Hili jina lake kwa hakika limenishangaza sana.

Mfano wa kukutana na mtu akakuambia kuwa yeye jina lake ni ''Michael Jackson.''

Huyo hapo chini mwenye jina lake:
1769567647590.jpg
 
Dear Mzee Butiku;

Mzee mwenzako, my late GrandFather, Laurent Kibatala, knew the natural Order of things since many, many, many Years ago. Decades ago; to be exact.

That is why He made this mural;imprinted it for posterity.

1. UHURU. 2. KAZI. 3. AMANI.

#UshauriTumeukataa#.
1769696711078.jpg
 
FARID ATRASH (1910 - 1974)
Wangapi wanaonisoma hapa wamepata kumjua Farid Atrash?

Farid Atrash alikuwa muimbaji maarufu, Misri na pia muigizaji senema katika miaka ya 1950.

Naamini hapa watakuwa watu wachache sana waliopata kusikia jina hili lakini katika Dar es Salaam tuliokulia baadhi yetu Farid Atrash alikuwa akifahamika na nyimbo zake zilikuwa maarufu na zikipigwa katika radio.

Halikadhalika miaka hiyo maduka mengi mitaani ilikuwa ya Waarabu na radio zao muda wote wakitegesha Sauti ya Cairo na nyimbo zilizokuwa zikipigwa na za waimbaji maarufu wa Kiarabu mfano wa Farid Atrash, Um Kulthum kwa kuwataja wachache.

Katika kitabu cha Abdulwahid Sykes nimeandika maneno haya mwanzo wa kitabu nikimweleza baba yangu na rafiki zake wa nyakati zile miaka ya 1950, nimesema, ''Wakati mwingine waliwasikiliza waimbaji wa Kiarabu, Um Kulthum, Mohammed Abdulwahab, Farid Atrash, Abdul Halim Hafidh, Feruz na Sabah.''

Leo katika msikiti wetu wa mtaani, Masjid Noor, Magomeni Mapipa baada ya Swala ya Adhuhur nakwenda kuchukua viatu vyangu nje ya msikiti akanikabili bwana mmoja na akaniita kwa jina na kunitolea salamu.

Nimeitika salamu nimempa mkono nikamuuliza, ''Iweje wewe unanijua mimi sikufahamu?

Hapo ndipo mazungumzo yakaanza.

Akanitajia jina lake kuwa ni ''Farid Atrash,'' kabila Mmanyema.

Nikamuuliza, ''Farid Atrash yule muimbaji?''

Akanijibu kuwa ndiye.

Akaingiza mkono katika kanzu yake nyeupe nadhifu na kunionyesha kitambulisho chake.

Kitambulisho kimeandikwa, ''Farid Atrash.''

Huyu ndugu yangu akanieleza kuwa yeye amekuwa akifuatilia sana vipindi vyangu mitandaoni.

Tukazungumza kiasi cha kuzungumza na tukapeana simu zetu.

Hili jina lake kwa hakika limenishangaza sana.

Mfano wa kukutana na mtu akakuambia kuwa yeye jina lake ni ''Michael Jackson.''

Huyo hapo chini mwenye jina lake:View attachment 3535368
Credits: Mzee Mohamed Said maana hii ni C&P
 
Wapare waliamua kuishi milimani kwa sababu za kiulinzi na kujihami dhidi ya maadui wao,jamii za wamasai na wachaga ambao walikua wakipigana ,kwa usalama na kujihami ilibidi wakae milimani,

Baadae walipokuja wakoloni ndio kabisa ilipelekea wakae huko kujificha ili wasitawaliwe kirahisi
1770002095277.jpg
 
USIKU MUHAMMAD ALI ALIIONA AFRIKA KWA MACHO YAKE LAGOS, 1964 Limbwata au utamaduni

Ilikuwa ni usiku wa kipekee katika jiji la Lagos, usiku ambao kelele za muziki wa highlife zilichanganyika na historia.

Ndani ya klabu maarufu ya usiku eneo la Yaba Kakadu au Lido Nightclub macho yote yalielekezwa kwa mgeni mmoja wa kipekee

Bingwa wa Dunia wa masumbwi uzito wa juu, Cassius Clay, baadaye dunia ilimjua kama Muhammad Ali.

Lakini huu haukuwa usiku wa mapambano ya ngumi. Ulikuwa ni usiku wa mwamko wa kiakili na kihisia.

Akiwa amevalia vazi la asili la Kiafrika, lililobuniwa kwa ustadi wa kipekee na mrembo wa jamii ya Lagos, Joyce Obong, Ali alionekana si tu kama bingwa wa ulingoni, bali kama mwana wa Afrika aliyerudi nyumbani.

Muziki wa highlife ulipopiga, Ali alitabasamu, tabasamu la mtu aliyegundua kitu kikubwa kuliko ubingwa.

Ndipo akatoa kauli iliyosikika kote duniani:
“Nigeria has opened my eyes. Now I can see the indignity the Black man suffers in America.”

Nigeria imenifungua macho. Sasa ninaona udhalilishaji anaoupata Mtu Mweusi huko Marekani.

Kauli hiyo haikutoka kwa hasira, bali kwa ufahamu mpya. Lagos, kwa usiku huo mmoja, ilimpa Ali kile ambacho Amerika ilikuwa imemnyima kwa muda mrefu utu, heshima, na utambulisho.

Joyce Obong, mwanamke aliyekuwa pembeni yake usiku huo, hakuwa wa kawaida.

Alikuwa miongoni mwa wabunifu wa kwanza wa mitindo nchini Nigeria kuweka msisitizo mkubwa kwenye vitambaa vya jadi vya Kiafrika, akipinga fikra kwamba urembo lazima uigize Magharibi.

Falsafa yake ilikuwa wazi na ya kimapinduzi
“Be Nigerian, Live Nigeria.”
(Kuwa Mnigeria, Ishi Nigeria.)

Kwa kumvalisha Ali vazi la asili, Joyce hakumpamba tu bingwa wa dunia alimvalisha Afrika kwenye mwili wa wake.

Ni Agosti 1964. Kabla ya Ali kubadili rasmi jina, kabla ya mapambano mengi ya kihistoria, kabla ya kuwa sauti kubwa ya haki za Wamarekani Weusi Lagos tayari ilikuwa imemgusa moyo wake.
1770055487374.jpg
 
Mwaka 1993 Oliver Mtukudzi alishiriki katika filamu iliyokuwa inazungumzia madhira ya mwanamke mjane iliyokuwa na jina la Winds of Change.

Oliver Mtukudzi alipewa kusoma script ya filamu hiyo Ili aandae soundtrack maalumu kwa ajili ya filamu hiyo usiku huohuo aliweza kuandaa wimbo huo kwa kunakshi na jina la Neria, Director wa filamu hiyo aliupenda na kupelekea filamu hiyo kuitwa Neria badala ya Title ya mwanzo ya Winds of Change.

Oliver Mtukudzi alizaliwa Septemba 22, 1952 Highfield Harare nchini Zimbabwe, alikuwa mwimbaji maarufu kupitia bendi ya Wagon Wheels tangu miaka ya 1970.

Alifariki Januari 23, 2019, wakati wa uhai wake alitoa album zaidi ya 40 zilizomuwezesha kushinda tuzo nyingi ambazo hata yeye mwenyewe hakuweza kuzikumbuka.

Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni kama..

Neria
Todii
Wasakara na nyingine nyingi tu
1770076176422.jpg
 
Pichani ni daraja la mto wami pindi lilipofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Campihi Colas (kapico) ya nchini Dernmarck mwaka 1991 na pia ulikuwa ni mradi wa matengenezo ya barabara kutoka Chalinze mpaka Segera
1770076582865.jpg
 
katika miteremko ya milima ya Upare Kaskazini, iliyopo Mashariki ya Milima ya Usambaa; na Kusini Mashariki mwa mlima Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa historia kutoka katika machapisho mbalimbali, lugha inayozungumzwa na watu wa eneo hili, inajulikana kama Chasu. Wenyeji wakaitwa Vaasu, hivyo kabila hilo lilijulikana k ama kabila la Waasu. Historia inaeleza kuwa katika Karne ya 18, Waasu walikuwa wenyeji wa Kenya eneo la Taita na Taveta.baada ya kusikia habari za Mlima Kilimanjaro, walihamia ili waishi katika miteremko ya mlima huo. Waasu walipofika karibu na maeneo ya mlima Kilimanjaro, walielekea sehemu za Kaskazini ili waishi karibu zaidi ya Kilimanjaro, wakiwa na matumaini makubwa ya kuishi huko. Tofauti na matarajio yao, walikutana na wenyeji wa eneo hilo, Wachaga. Hata hivyo, hawakukata tamaa, waliendelea kuweka mazingira ya kujenga himaya hayo. Wachaga walipoona wanaingiliwa, waliitana na kuanza kuwafukuza huku wakipiga makelele wakisema “wapare…wapare”, ikiwa na maana wapige… wapige! Ili kuokoa maisha yao, Waasu walikimbia kuelekea sehemu za mteremko hadi eneo la Mwanga na Same, Kusini mwa mlima Kilimanjaro; na kupumzika hapo huku wakitafakari cha kufanya. Kuanzia wakati huo, Wachaga walipowaona Waasu, waliwanyooshea kidole la kusema “wapare”, jambo ambalo lilisababisha neno hilo kuwa maarufu; na ndio maana hadi leo wanaitwa Wapare, neno la Kichaga ambalo maana yake ni wapige. Simulizi za makabila, zinasema Wapare waliweka makazi ya kudumu katika eneo la Same, Kusini mwa mlima Kilimanjaro ili waweze kuangalia uzuri na maajabu ya mlima Kilimanjaro
1770206649527.jpg
 
JICHO LA ASKOFU KATIKA JAMII NA UCHAFU!

Wanaonekana katika picha hizi ni wanafunzi wa Shule ya Duke of York, Kenya wakiota jua na wengine wakiwa wanapumzika katika mabweni mwaka 1957. Fuatilia kwa umakini kisa hiki!

Kwa mujibu wa Odhiambo Levin Opiyo, Shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1949, Gavana wa Kenya wakati huo, Sir Philip Mitchell aliondoka Ikulu kwenda kuishi katika nyumba iliyokuwa Ngong kwa ajili ya kuwaruhusu wanafunzi wa kwanza kutumia makazi rasmi ya Ikulu kama mabweni hadi majengo ya shule yaliyokuwa yanajengwa yatakapokamilika.

Odhiambo anaeleza pia katika ukurasa wake ya kuwa shule hiyo ilikuwa kwa ajili ya wanafunzi wazungu (weupe) tu hadi mwaka 1960. Ilikuwa imeajiri watu kwa ajili ya kufanya kazi kama za kutunza majengo, kufanya usafi wa mazingira na kufua nguo za wanafunzi.

Chakula cha wanafunzi kilikuwa ni pamoja na nyama choma ya kondoo (roast lamb), piza na keki vilivyotayarishwa na mpishi aliyetakiwa kufuata kanuni ngumu za lishe katika kuandaa vyakula hivyo.

Baada ya Uhuru, Duke of York ilibadilishwa na kuwa Lenana School. Nilifika Lenana School mwaka 1999 kuhudhuria Mkutano wa Walimu na Watumishi wa Scripture Union of Kenya (Umoja wa Kujisomea Biblia nchini Kenya. Niliongoza ujumbe wa watu 4 kutoka Tanzania ambao ni Wilson Adam, Gloria, Asifiwe Aloyce na mimi mwenyewe. Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano ule alikuwa ni Waziri wa Elimu wa Kenya wakati ule, Mhe. Kalonzo Musyoka.

Lenana School ni shule maarufu sana nchini Kenya kwa miaka mingi. Ukitaka kujua ilikuwa ni shule ya aina gani, kwa hapa nchini Tanzania ingeweza kulinganishwa na shule kama Tabora Boys na Azania kwa shule za serikali au Minaki, Tosamaganga, Pugu, Mazengo, Rungwe hata Umbwe kwa shule zilizokuwa za misheni.

Ukiachia mbali mambo mengine yatakayoiacha wazi midomo yako, suala la kuajiri watu kwa ajili ya kutunza majengo ya shule ni jambo lililo muhimu sana katika uimara na ubora mzima wa majengo. Hao huitwa estate managers na ni wahitimu wa kozi maalum katika vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Ardhi.

Lakini sidhani kama wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi wameajiriwa kwa ajili ya kuyatunza mazingira ya majengo yote ya umma zikiwemo shule zetu. Ukienda Azania, Tambaza, Pugu na hata Zanaki unaweza kufikiri ni magofu ya kale.
Ukifika shule hizo na shule nyingine, usifanye kosa la kuingia chooni.

Kwa shule za wavulana kama Azania, zilikuwa na sehemu maalum ya haja ndogo ambapo kila wakati maji yalitiririka kutoka katika mabomba yenye matundu maalum ukutani ili kutiririshia mikojo katika mabomba maalum. Nilipokuwa Kidato cha Kwanza, niliukuta mfumo huo pale Azania ukiwa taabani ingawa ulikuwa unafanya kazi, lakini nilipoondoka Kidato cha Sita hali ilikuwa mbaya sana.

Hata 'Bwawa la Kisusulinge' 'the Amoeba Pond' pale Azania nililikuta likiwa na maji na samaki kadhaa. Lakini sasa, ninapowauliza wanafunzi wa pale wanasema limefukiwa na mchanga.

Lakini kilichonishangaza ni kuwa, nilipokuwa nchini Uingereza, mfumo huo unaendelea tena kwa ubora zaidi. Shule kama Azania au Zanaki wanaajiriwa wataalamu wafuatao: Watunza bustani (gardeners), wahandisi wa mifumo (engeneers), watu wa kufanya matengenezo, nk.

Chuo Kikuu cha Ardhi kinatoa wahandisi wa mazingira kila mwaka lakini wengi hawana ajira wakati majengo yetu ambayo yalijengwa kwa mabilioni ya mikopo ya fedha yanazidi kuoza kwa kukosa uangalizi. Mitaro ya Maji machafu katika Jiji la Dar es Salaam iliziba na njia zake zote hazifanyi kazi. Ukitaka kujionea kwa jinsi gani sisi ni wachafu, tembelea Barabara zote za katikati ya Jiji wakati mvua inanyesha kama Barabara ya Umoja wa Mataifa, nk.

Wakati wa mvua mifuniko ya maji machafu hufunguliwa ili kuruhusu maji machafu yenye kinyesi yatitirishwe na maji barabarani. Hali inakuwa mbaya zaidi kama mvua iliyonyesha ni kidogo na hivyo maji machafu yanaonekana.

Je, wewe ni mkazi wa Dar es Salaam? Je wewe ni miongoni mwa waliosoma shule zilizotajwa? Je, wewe ni mtumishi katika serikali na unaona hali ya majengo ya serikali? Je, maelezo hayo ya askofu katika maeneo hayo yana ukweli kwa kiasi gani? Je, unafikiri majengo yote ya serikali yameajiri wahandisi kama estate managers na kama environment engeneers? Je, unafikiri hili Jiji la Dar es Salaam limeajiri kweli wahandisi wa mazingira?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 6 Februari 2026; Saa 2:50 asubuhi
1770359530619.jpg
 
Back
Top Bottom