Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Ni miaka 126 tangu kuuwawa kwa Mangi Meli Mandara ,kiongozi wa Old Moshi ,mtoto wa Mangi Mandara,
Raia wa Tanzania anayeishi nchini Ujerumani Mnyaka Sururu Mboro, amekuwa akitafuta fuvu lililotoweka la Mangi Meli kwa miaka zaidi ya 40.

Mangi Meli, chifu kutoka eneo la kaskazini ya sasa ya Tanzania aliuawa mwaka 1900 kwa kupambana dhidi ya utawala wa ukoloni wa Ujerumani.

Baada ya kuuawa mwili wake uliakatwakatwa na kichwa chake kikasafirishwa kwenda nchini Ujerumani.

Ujerumani yarejesha mafuvu ya watu iliowaua Namibia 1904
Lilipo fuvu lake bado haijulikani, lakini baada ya wakfu unaofahamika kama Prussian Cultural Heritage wa mjini Berlin kugundua mafuvu zaidi kutoka Tanzania, imempa Bw Mboro matumaini mengi.
Anatoka eneo sawa na alilokuwa akitoka Mangi Meli, na mwaka 1977, kabla hajaondoka kwenda kusoma Ujerumani alimuambia bibi yake kuwa angetafua fuvu hilo.

Watafiti wamegundua mabaki 200 kutoka Tanzania mengi yakiwa ni mafuvu ambayo yalichukuliwa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa Ujerumani.
1770369239407.jpg
 
Jengo la muda mrefu na lenye historia ndefu na likaitwa jina marufu kilema kubwa likitumika shule miaka hiyo sasa linaonekana kihistoria nchi za ulaya kwa watu waliopitia kilema na kusoma ebeo hili kujipatia elimu pia ata imani ya kikatoliki .Utambuzi wa kutaka kujua kilema ukiona jengo hili linakujulisha upo kilema na kunauwezekano wa kutumia nembo ya picha hii katia utambuzi ya kilema yetu kutambilika zaidi kihistoria na wageni wengi wanaofika kuhiji kilema huwa wanatembelea jengo hili na kuliona kihistoria . Na kujifunza wajenzi walivyotumia mawe kutengeneza jengo hili la gorofa .@kizione amesema grop la kilema yetu imeandika nayo historia ya kufungua barabara ya marangu kirefure imejiandikia historia kubwa kuwa grop hilo linafanya kazi na litapewa kipaumbele kwa kuinyanya kilema kimaendeleo kwa ushiriano mzuri
1770482054688.jpg
 
Ilikuwa ni miaka ya 90 kuelekea 2000. Pale Liberia kulikuwa na Rais mmoja mbabe sana, anaitwa Charles Taylor. Huyu jamaa alikuwa haambiliki, alikuwa anafadhili vita vya Sierra Leone wapigane wenyewe kwa wenyewe..
CIA walikuwa wanamtamani sana, lakini walikosa njia ya kuingia Ikulu kwake.

Sasa, CIA wakapiga hesabu Huyu mwanaume anapenda sana warembo. Hapo ndipo wakamvuta binti mmoja fundi, mrembo balaa na kichwa chake nihatari, anaitwa Alicia Macy.

Alicia aliingia nchini kama mfanyakazi wa kutoa misaada . Alijua kuvaa, alijua kuongea, na alijua namna ya kumfanya mwanaume yeyote ageuke shingo.

Haikuchukua muda, akajisogeza kwenye duru za karibu na Rais. Siku moja kwenye bonge la party, Charles Taylor akatupa jicho kwa Alicia. akatupa tabasamu moja la gharama. Taylor akaingia kingi, hakujua kuwa huyo mwanamke ni "sumu" iliyotumwa na Washington.

Alicia akawa mpenzi wa Rais. Alikuwa anakaa naye Ikulu, wanalala kitanda kimoja, na wanakula meza moja. Wakati Taylor anadhani amepata "tunda" la roho yake, Alicia alikuwa anapiga kazi.

Wakati Rais amelala fofofo, Alicia alikuwa anachukua muda huo kupekua makaratasi ya siri, kusikiliza mazungumzo ya siri ya biashara za silaha, na kujua ramani nzima ya jinsi almasi zinavyochimbwa na kuuzwa nje ya nchi. Kila kitu alichokiona usiku, asubuhi kilikuwa mezani kwa mabosi wa CIA.

Lakini unajua maisha ya kijasusi ni kama kutembea kwenye kamba? Baada ya muda, walinzi wa Taylor wakaanza kujiuliza "Huyu mzungu mbona anauliza sana maswali?" Hali ikawa tete.

Alicia akaanza kuhisi kuwa Charles Taylor anaanza kumshtukia. Siku moja usiku, akapokea ujumbe wa dharura kutoka kwa mabosi wake.
"Ondoka hapo mara moja, mchezo umegundulika!"

Ilibidi atumie mbinu za hatari kutoroka Liberia usiku wa manane kabla ya makomando wa Taylor hawajamkamata. Alirudi Marekani akiwa na siri zote ambazo baadaye zilitumika kumfunga Charles Taylor maisha kule mahakama ya The Hague kwa makosa ya kivita.
1770506912152.jpg
 
machifu wafuatao waliofanya safari hiyo:
Slyvanus Kaaya wa Kabila la Meru, Arusha
Sefania Sumlei wa Kabila la Arusha
Amri Boo Dodo wa Kabila la Gorowa, Wilaya ya Ibulu
Sabu bin Sabu wa Morogoro
Paul Norbert wa Lindi
Hivi huyu Sefania Sumlei ndo allirithi uchifu kutoka kwa chief Sabaya? au Chief mejoooli? kwa wakwe zetu
 
Ilikuwa ni miaka ya 90 kuelekea 2000. Pale Liberia kulikuwa na Rais mmoja mbabe sana, anaitwa Charles Taylor. Huyu jamaa alikuwa haambiliki, alikuwa anafadhili vita vya Sierra Leone wapigane wenyewe kwa wenyewe..
CIA walikuwa wanamtamani sana, lakini walikosa njia ya kuingia Ikulu kwake.

Sasa, CIA wakapiga hesabu Huyu mwanaume anapenda sana warembo. Hapo ndipo wakamvuta binti mmoja fundi, mrembo balaa na kichwa chake nihatari, anaitwa Alicia Macy.

Alicia aliingia nchini kama mfanyakazi wa kutoa misaada . Alijua kuvaa, alijua kuongea, na alijua namna ya kumfanya mwanaume yeyote ageuke shingo.

Haikuchukua muda, akajisogeza kwenye duru za karibu na Rais. Siku moja kwenye bonge la party, Charles Taylor akatupa jicho kwa Alicia. akatupa tabasamu moja la gharama. Taylor akaingia kingi, hakujua kuwa huyo mwanamke ni "sumu" iliyotumwa na Washington.

Alicia akawa mpenzi wa Rais. Alikuwa anakaa naye Ikulu, wanalala kitanda kimoja, na wanakula meza moja. Wakati Taylor anadhani amepata "tunda" la roho yake, Alicia alikuwa anapiga kazi.

Wakati Rais amelala fofofo, Alicia alikuwa anachukua muda huo kupekua makaratasi ya siri, kusikiliza mazungumzo ya siri ya biashara za silaha, na kujua ramani nzima ya jinsi almasi zinavyochimbwa na kuuzwa nje ya nchi. Kila kitu alichokiona usiku, asubuhi kilikuwa mezani kwa mabosi wa CIA.

Lakini unajua maisha ya kijasusi ni kama kutembea kwenye kamba? Baada ya muda, walinzi wa Taylor wakaanza kujiuliza "Huyu mzungu mbona anauliza sana maswali?" Hali ikawa tete.

Alicia akaanza kuhisi kuwa Charles Taylor anaanza kumshtukia. Siku moja usiku, akapokea ujumbe wa dharura kutoka kwa mabosi wake.
"Ondoka hapo mara moja, mchezo umegundulika!"

Ilibidi atumie mbinu za hatari kutoroka Liberia usiku wa manane kabla ya makomando wa Taylor hawajamkamata. Alirudi Marekani akiwa na siri zote ambazo baadaye zilitumika kumfunga Charles Taylor maisha kule mahakama ya The Hague kwa makosa ya kivita.View attachment 3540880
Sikulijua hili, lete makala kwa kirefu mkuu, maana ni bonge la stori!

Mambo ya kuishi na kimada Ikulu na uhuni huni mwingine, huyu Rais alikuwa msimbe?
 
machifu wafuatao waliofanya safari hiyo:
Slyvanus Kaaya wa Kabila la Meru, Arusha
Sefania Sumlei wa Kabila la Arusha
Amri Boo Dodo wa Kabila la Gorowa, Wilaya ya Ibulu
Sabu bin Sabu wa Morogoro
Paul Norbert wa Lindi
Ni kweli, SEFANIA SUMULEI alikuwa kiongozi wa Ukoo baadae kmwa kabila la Waarusha (Larusa)
 
Mashindano ya miguu mizuri zaidi huko Paris, Ufaransa, mnamo mwaka wa 1950 washiriki walisimama nyuma ya pazia, huku miguu yao pekee ikionekana kwa majaji na hadhira.

Tukio hilo lilikuwa aina ya shindano la urembo lililopendwa zaid katikati ya karne ya 20, wakati mwingine hujulikana kama "shindano la kifundo cha mguu".

Picha hii inamwonesha jaji wa kiume akiweka kadi ya nambari mbele ya jozi ya miguu.

Mashindano hayo yalifanyika sana katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Paris na London.

1770535195987.jpg
 
Back
Top Bottom