Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Mwanakosmonauti Sergei Krikalev alipokuwa kwenye kituo cha anga cha Mir mwaka 1991, alipokea ujumbe wa kustusha na kusikitisha kwamba hawezi kurudi nyumbani kwa muda ulopangwa kwa sababu Umoja wa Kisovieti ulikuwa umefutiliwa mbali.

Ujumbe huo ulisema, "You must remain in space, as the country that sent you no longer exists" ikamaanisha "Endelea kubaki anga za juu kwasababu nchi iliyokutuma haipo tena"

Hii ilikuwa ni kutokana na mabadiliko ya kisiasa na mgogano wa kiuchumi kufuatia kuvunjika kwa USSR.

Krikalev, anayejulikana kama "Raia wa Mwisho wa Kisovieti" (The last Citizen of Soviet) alibaki kwenye kituo cha anga cha Mir kwa siku 311, karibu mara mbili ya muda wake uliopangwa, kwa sababu hakukuwa na bajeti wala utulivu wa kisiasa wa kumpeleka mwingine angani ili kumrudisha duniani.

Hatimae alirudi duniani Machi 25, 1992, akitua katika jamhuri huru mpya ya Kazakhstan, ambapo wakati akiondoka misheni alitoka jiji lililoitwa Leningrad na kurudi katika jiji lililoitwa upya St. Petersburg.
1771574658690.jpg
 
Je, unaijua historia ya wimbo Stuck on You wa Lionel Richie?

Wimbo huu ulitoka mwaka 1984 ukiwa sehemu ya albamu yake maarufu Can't Slow Down.
Tofauti na nyimbo zake nyingi za R&B, “Stuck on You” ulikuwa na ladha ya country-pop, ukionyesha upande mwingine wa kipaji chake.

Lionel Richie aliuandika wimbo huu yeye mwenyewe, akielezea upendo wa kweli na kujitoa kwa mpenzi wake. Video ya wimbo huu ilionyesha mazingira ya vijijini nchini Marekani, jambo lililowavutia hata mashabiki wa muziki wa country.

wimbo huu ulifanikiwa ulifika nafasi ya 3 kwenye Billboard Hot 100 nchini Marekani. Albamu yake ilishinda tuzo ya Album of the Year kwenye Grammy Awards mwaka 1985.
“Stuck on You” unaendelea kuwa moja ya nyimbo za mapenzi zinazoendelea kutamba zaidi kutoka miaka ya 1980s.
1771685436190.jpg
 
HISTORIA YA WIMBO USINIPITE MWOKOZI. Tenzi namba 10

Wimbo huu wa usinipite ni moja kati ya nyimbo za kikristo maarufu sana Duniani. Na wimbo huu unaimbwa Na madhehebu karibu yote. Ni wimbo wa maombi, una ujumbe uliotulia, Na una tafakari itakayokuvuta kwa Mungu moja kwa moja.

Mwandishi wa wimbo huu maarufu anaitwa FRANCES JANE CROSBY na alizaliwa kaunti ya Putnam,New York,March 24,1820 na kufariki katika umri mwema wa miaka 95 mwaka1915.

Majuma kati ya sita hadi nane tu, baada ya kuzaliwa Daktari asiye na ujuzi alimfunika macho na plasta ya kemikali kimakosa, kitendo kilichomsababishia upofu wa kudumu. Upofu alioishi nao tangu akiwa Na wiki 6 mpaka maisha yake yote aliishi gizani, akuweza kuona tena, Na aliishi miaka 95. Kwa makosa ya daktari yalimsababishia asione maishani.

Pamoja na upofu aliokuwa nao bado Fanny Crosby aliweza kugundua kuwa alikuwa na karama ya kipekee ambayo Mungu alimjalia na alifurahia sana kuitumikia karama yake ya utunzi wa Nyimbo za tenzi na injili na mara nyingi alipendelea kusema,"Nina vitu vya thamani sana ndani yangu"

Alipokuwa na miaka tisa tu,aliandika maneno yafuatayo:
"Ni jinsi gani nafsi yangu ilivyo na furaha,Ingawa sioni,
Nimeridhika kuwa katika dunia hii, Nitaishi kwa furaha,
Ni baraka ngapi ninazifurahia,
Watu wengine wamezikosa?.
Kulia na kujuta Kwasababu ya upofu?,
Sitaweza,na wala sitathubutu."

Alipokuwa na umri wa miaka 15 alijiunga na taasisi ya watu wasioona ya New York, rekodi yake chuoni ilikuwa nzuri kiasi kwamba uongozi wa chuo ulimbakisha ili awe mwalimu pale chuoni,alidumu kwenye taasisi hiyo kwa miaka 11 akifundisha.

KISA CHA WIMBO

Mwaka wa 1868 William Doane mtunzi wa muziki na mfanya biashara maarufu wa Cincinnati,Ohio, Marekani , alipenda kuboresha kazi zake za utunzi kwa kushirikiana na watu wenye vipaji vya utunzi wa Mashairi ya nyimbo hivyo akamwomba Fanny Crosby kutunga Mashairi ya Wimbo utakaoanza na Usinipite Mwokozi .

Kazi hii ilimchukua Fanny Crosby majuma kadhaa mpaka siku moja alipokwenda kwenye gereza moja karibu na vitongoji vya Manhattan,New York kuhudumia wafungwa kwenye vipindi vya ibada,Ndipo aliposikia mmoja. wa wafungwa akipaza sauti na kusema ,“Bwana Mwema!Usinipite! Usinigeuzie mgongo,Nikumbuke" Mfungwa huyo alikuwa aliwaita wale wahudumu au askari wa magereza waliokuwa gerezani humu ili asije akasahauliwa.

Kilio hiki cha huyu mfungwa kilimwingia moyoni na kujaa kwenye fikra zake na kuwaza ni kwa namna gani wafungwa hawa walikuwa ni watu waliosahauliwa na jamii na kutohesabika kama watu wenye umuhimu.

Crosby alitafakari umuhimu wa kilio cha mfungwa huyu aliyekuwa akilia kwamba Bwana amkumbuke. Akawaza jinsi ambavyo watu wanavyoweza kumlilia Mungu Na pengine Mungu akafanya kwa wengine Na akawaacha wao. Ndipo alipoweza kupata wepesi wa kutiririka Mashairi Haya, kwamba siku Yesu atakapokuja Na majibu ya wengine basi namimi asinipite. Na baada ya kuyaandika akamkabidhi Bwana William Doane ili atengeneze muziki ambao ndiyo unatumika mpaka leo.

Hii ilikuwa ni kolabo yao ya kwanza na baada ya hapo waliweza kushirikiana kuimba nyimbo zingine nyingi, Fanny Crosby katika uhai wake alifanikiwa kuandika tenzi 8,000, nyimbo za kawaida 1,000 vitabu vinne vya Mashairi na vitabu viwili vya historia yake vilivyouzwa sana, mojawapo ya nyimbo alizoandika ni pamoja na "NDIYE DHAMANA YESU WANGU"

Wimbo huu wa "Usinipite Mwokozi" ulichapishwa rasmi mwaka wa 1870 kwenye orodha ya nyimbo za devotion na ulipata zaidi umaarufu baada ya kutambulishwa na L.Moody na Ira.D.Sankey kwenye mikutano yao ya uamsho huko London,Uingereza.

na kutokana na maelezo ya Dr.Young huu ni wimbo wa kwanza wa Fanny Crosby uliopata sifa nyingi Ulimwengu ni kote.

Haya ndiyo Mashairi ya wimbo
"USINIPITE MWOKOZI"

1. Usinipite Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Yesu,Yesu,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

2. Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.

3. Sina ya kutegemea,
Ila Wewe tu;
Uso wako uwe kwangu;
Nakuabudu.

4. U Mfariji peke yako;
Sina Mbinguni,
Wala duniani pote,
Bwana mwingine.

#ToGodBeTheGlory #FollowJesus
FB_IMG_1771704993206.jpg
 
Huwa natamani sana ni heri ningezakiwa miaka ya nyuma kabisa ili mwaka kama huu ningekua mzee kabisa...

Huwa naonea wivu sana watu wana a zamani.
Napenda sana life ya zamani na nachukia sana hi life ya sasa.

Natamani niende nikaishi mashambani huko mi kazi yangu iwe kulima tu..

Natamani sana sana sana natamani ile life. Ya 1900s...

Nawezaje kwenda mashambani nikajifiche huko nipate kipande cha ardhi maisha yaanze,

Niwe na acces ya
Umeme na Internet tuuu
 
SOKO LA WATUMWA ZANZIBAR ENEO AMBALO UTU ULIPIGWA MNADA:

Katikati ya Mji Mkongwe, Zanzibar, kuna kanisa. Lakini kabla ya utu Kabla ya maombi… Kabla ya msalaba. Kulikuwa na minyororo. Eneo hili lilikuwa moja ya soko kubwa la watumwa katika eneo la Afrika Mashariki. Wanaume, wanawake, na watoto wa Kiafrika walitekwa kutoka bara, kutoka Tanzania, Kongo, Malawi, Msumbiji, hata ndani kabisa ya Afrika ya Kati, waliandamana kwa wiki kadhaa, wakipigwa chapa, Wengine walikufa kwa njaa, walipigwa mijeredi… na kisha kuuzwa kama mifugo.

Familia zilisambaratika kwa sekunde. Watoto walibebwa kinguvu kutoka kwa mama zao. Binadamu kukaguliwa kama wanyama meno checked, misuli, bei mazungumzo. Na ulimwengu uliita hii ni biashara.

Leo Wacha tuseme ukweli: hii haikuwa biashara. Hii ilipangwa tu kuwafanyia ukatili waafrika. Hili lilikuwa soko la ubinadamu uliovunjika.

Maelfu walipitia soko la watumwa la Zanzibar kabla ya kusafirishwa hadi Mashariki ya Kati na kwingineko. Wengine walifia kwenye vyumba vya kuhifadhia watu, chini ya ardhi, wakikosa hewa gizani, wakingoja kuuzwa. Leo, Kanisa la Anglikana la Kanisa limesimama kwenye tovuti hiyo hiyo. Ilijengwa baada ya soko la watumwa kufungwa mwaka 1873 chini ya shinikizo la Uingereza.
1771783625033.jpg
 
tarehe 21 Juni 1982, katika mechi ya hatua ya makundi kati ya Ufaransa vs Kuwait, iliyochezwa mjini Valladolid, Hispania. Ufaransa walikuwa wakitawala mchezo huo na tayari walikuwa wanaongoza kwa mabao 3–1, hali iliyoonyesha wazi tofauti ya kiwango kati ya timu hizo mbili.

Dakika za mwisho za mchezo, mchezaji wa Ufaransa Alain Giresse alifunga bao la nne halali kabisa, halikuwa offside wala faulo yoyote.
Lakini cha kushangaza bao hilo lilipoingia, wachezaji wa Kuwait walisimama na kuanza kulalamika wakidai walisikia mlio wa kipenga (whistle) kutoka kwa watazamaji, wakidhani muamuzi alikuwa amesimamisha mchezo.

muamuzi wa mchezo huo alikuwa, Miroslav Stupar kutoka Umoja wa Kisovieti, muamuzi huyo awali alikubali bao hilo.
Lakini cha ajabu.
Sheikh Fahad Al-Ahmad Al-Sabah, ambaye alikuwa kaka wa mtawala wa Kuwait wakati huo na pia Rais wa Shirikisho la Soka la Kuwait, alishuka kutoka jukwaa la wageni maalum na kuingia moja kwa moja uwanjani akiwa na walinzi wake.
Alimfuata muamuzi, akaanza kumbishia uamuzi huo kwa shinikizo kubwa, na hata akatishia kuwaondoa wachezaji wa Kuwait uwanjani endapo bao halitofutwa.

Hali hiyo ilisababisha mkanganyiko mkubwa. Wachezaji wa Kuwait walianza kuondoka uwanjani taratibu, wakimfuata sheikh wao, huku mechi ikisimama kwa muda mrefu.
Chini ya shinikizo hilo lisilo la kawaida, muamuzi Stupar alibadilisha uamuzi wake na kulifuta bao la Ufaransa.
Matokeo yakarudi kuwa 3–1, na mchezo ukaendelea hadi mwisho bila mabadiliko.

Baadaye, tukio hili lilisababisha hasira kubwa katika ulimwengu wa soka.
FIFA ilimchukulia hatua kali muamuzi Miroslav Stupar na kumpiga marufuku kwa uamuzi huo, kwani ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kwa mtu asiye muamuzi kuingilia na kufanikisha kufutwa kwa bao. Sheikh Fahad, kwa upande mwingine, hakupata adhabu kubwa kutokana na nafasi na ushawishi wake mkubwa, hadi alipofariki mwaka 1990 wakati wa Vita vya Ghuba.

Naam uhuni kwenye mpira wa miguu haujaanza leo😁😁😁

1771920821677.jpg
 
Katika kipindi cha utawala wa Idi Amin Dada kati ya mwaka 1971 hadi 1979, uhusiano kati ya Uganda na Uingereza ulikuwa mbaya sana na ulijaa mvutano wa kisiasa na kihistoria. Amin alikuwa amejitangaza waziwazi kuwa mshindi wa Dola ya Uingereza, akijipa jina la “Conqueror of the British Empire” ( CBE )

Mnamo Julai 1975, kulifanyika hafla kubwa ya kidiplomasia katika moja ya maeneo ya serikali mjini Kampala, ambapo wawakilishi wa kigeni, mabalozi na wafanyabiashara walialikwa.
Hafla hiyo ilipaswa kuwa ya kawaida, lakini iligeuka kuwa tukio la kushangaza na la kihistoria.
Katika tukio hilo, Idi Amin aliwaamuru wafanyabiashara wanne Waingereza waliokuwa wanaishi na kufanya kazi Uganda kumbeba juu ya kiti cha kifalme, aina ya machela yaliyokuwa yakitumiwa na wafalme wa kale, wakimbeba juu ya mabega yao mbele ya wageni na kamera.

Kitendo hiki hakikuwa cha bahati mbaya wala cha mzaha.
Kilikuwa onyesho la wazi na la makusudi la kugeuza historia ya ukoloni.
Kwa karne nyingi, Waafrika walilazimishwa kubeba wazungu, kuwatumikia, na kudhalilishwa katika ardhi yao wenyewe.
Sasa, Amin alitaka dunia ione taswira tofauti kabisa: wazungu wakimbeba kiongozi mweusi wa Afrika, kama ishara ya kwamba madaraka yalikuwa yamebadilika.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Amin na wafuasi wake, tukio hilo lilikuwa jibu la kisiasa na kihistoria kwa ubeberu wa Uingereza barani Afrika.
Alisisitiza kuwa Waingereza waliwanyonya Waafrika kwa miaka mingi, waliwafanya watumwa, waliiba rasilimali zao na kujenga utajiri wa nchi zao juu ya mateso ya watu wa Afrika. Kwa hiyo, tukio hilo lililenga kuwafedhehesha hadharani na kuwaonyesha kuwa zama zile zilikuwa zimepita.

Baadhi ya vyanzo vya wakati huo vinaeleza kuwa wafanyabiashara hao walifanya hivyo kwa sababu ya shinikizo na hofu.
Waliishi Uganda katika kipindi ambacho Amin alikuwa na mamlaka makubwa, mali nyingi za wageni zilikuwa tayari zimetawaliwa, na laiti wangefanya upinzani wowote basi ungeweza kuleta madhara makubwa kwa maisha au biashara zao.

Tukio la namna hiyo lilitokea tena 1975, ambapo Waingereza kadhaa walipiga magoti mbele ya Idi Amin na kuapa uaminifu ili kupokea uraia wa Uganda.
Haya yote yalikuwa sehemu ya kile Amin alichokiita kuishinda Uingereza bila vita, akitumia maonyesho ya kisiasa badala ya mapigano ya kijeshi.

1771921514725.jpg
 
tarehe 21 Juni 1982, katika mechi ya hatua ya makundi kati ya Ufaransa vs Kuwait, iliyochezwa mjini Valladolid, Hispania. Ufaransa walikuwa wakitawala mchezo huo na tayari walikuwa wanaongoza kwa mabao 3–1, hali iliyoonyesha wazi tofauti ya kiwango kati ya timu hizo mbili.

Dakika za mwisho za mchezo, mchezaji wa Ufaransa Alain Giresse alifunga bao la nne halali kabisa, halikuwa offside wala faulo yoyote.
Lakini cha kushangaza bao hilo lilipoingia, wachezaji wa Kuwait walisimama na kuanza kulalamika wakidai walisikia mlio wa kipenga (whistle) kutoka kwa watazamaji, wakidhani muamuzi alikuwa amesimamisha mchezo.

muamuzi wa mchezo huo alikuwa, Miroslav Stupar kutoka Umoja wa Kisovieti, muamuzi huyo awali alikubali bao hilo.
Lakini cha ajabu.
Sheikh Fahad Al-Ahmad Al-Sabah, ambaye alikuwa kaka wa mtawala wa Kuwait wakati huo na pia Rais wa Shirikisho la Soka la Kuwait, alishuka kutoka jukwaa la wageni maalum na kuingia moja kwa moja uwanjani akiwa na walinzi wake.
Alimfuata muamuzi, akaanza kumbishia uamuzi huo kwa shinikizo kubwa, na hata akatishia kuwaondoa wachezaji wa Kuwait uwanjani endapo bao halitofutwa.

Hali hiyo ilisababisha mkanganyiko mkubwa. Wachezaji wa Kuwait walianza kuondoka uwanjani taratibu, wakimfuata sheikh wao, huku mechi ikisimama kwa muda mrefu.
Chini ya shinikizo hilo lisilo la kawaida, muamuzi Stupar alibadilisha uamuzi wake na kulifuta bao la Ufaransa.
Matokeo yakarudi kuwa 3–1, na mchezo ukaendelea hadi mwisho bila mabadiliko.

Baadaye, tukio hili lilisababisha hasira kubwa katika ulimwengu wa soka.
FIFA ilimchukulia hatua kali muamuzi Miroslav Stupar na kumpiga marufuku kwa uamuzi huo, kwani ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kwa mtu asiye muamuzi kuingilia na kufanikisha kufutwa kwa bao. Sheikh Fahad, kwa upande mwingine, hakupata adhabu kubwa kutokana na nafasi na ushawishi wake mkubwa, hadi alipofariki mwaka 1990 wakati wa Vita vya Ghuba.

Naam uhuni kwenye mpira wa miguu haujaanza leo😁😁😁

View attachment 3547910
🤣🤣
 
Back
Top Bottom